Dream Touch
Member
- Mar 26, 2023
- 21
- 33
ACHA UJINGANimehitimu chuo kikuu cha Dodoma hivi punde, lakini mazingira tuliyokuwa tunaishi pale chuoni hakika yanasikitisha.
Colleges nyingi za pale UDOM kuna changamoto kubwa ya usafi chooni na ukiachilia mbali suala la usafi ila maintenance kwenye vyoo vya UDOM ni hovyo kabisa. Wanafunzi wanalipa ada na kutimiza majukumu yao mengine ila nashangaa Sana kwanini uongozi hauzingatiii maeneo nyeti Kama maliwatoni.
Ukiwa mgeni ukaanza kutembea kwenye viunga mbalimbali kwa nje utavutiwa na majengo lakini ukiingia kwenye vyoo vya hosteli hali ni mbaya Sana. Yaani hadi hosteli zinanuka mikojo na mavimavi tu. Hii sio sawa hata kidogo na ni aibu kwa chuo kikubwa kama kile kushindwa kuhimili na kukarabati vyoo mara kwa mara.
Ukienda chooni kwanza sahau kuhusu kukuta maji, yaani maji ni hadi utoke hosteli uende kuchota mita kadhaa toka umbali wa hosteli zilipo upande ngazi na ndoo yako ndio ukanye au ukafanye mengine. Nahisi dada zetu huwa wanapata kadhia sana kuhusu usafi wao binafsi wanapotumia vyoo.
UDOM mnakera aisee, mmekanusha la kunguni na hili najua mtakanusha ila chuo chenu kina vyoo VICHAFU
"We embracing knowledge" knowledge my foot wakati hata knowledge ya kukarabati vyoo hamna.
Sipingi ulichokizungumza
Ila umekosa busara kwenye uwasilishaji wa hoja yako
1.Ulikuwepo UDOM kwa miaka kadhaa,ulifanya nini kuboresha hilo??
2.Mbona umetumia lugha ngumu Sana, ni kweli hali iko hivyo au umeamua kuichafua serikali?? Kwa nini nisiamini kuwa unahoja uliyonayo nje ya hoja uliyoiwasilisha??
3. Kama mtanzania mzalendo unatambua madhala ya hiyo post ndani na nje ya nchi??
4.Hivi Kama maji yanapatikana mita kadhaa toka jengo la hostel ni chanzo Cha uchafu vyooni kweli? Nilisoma UDSM nilikuwa pale mabibo hostel block C second floor. Bafuni hakukuwahi kuwa na maji. Maji tulichota kwenye matank yaliyopo nje ya mabweni lakini tulizingatia usafi.
Kuwa Muungwana bro, Hapo hujengi bali unabomoa.
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app