Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,867
Kamwe siwezi kuwasifia watu weupe kwa usafi, ni wachafu sana lakini wameweza kuvuka kigezo cha uchafu wa jumuiya na kubaki kwenye uchafu wa mtu mmoja mmoja.
Hawaogi kila siku kama sisi tena zaidi ya maramoja kwa siku, hawatumii maji kutawaza, si watu wa kufua kila siku lakini wametuzidi kwenye uchakataji, uhifadhi na utunzaji wa takataka na mazingira kwa ujumla.
Mipangilio ya miji, na mipango miji vinazingitiwa kwa asilimia 100, nini kikae wapi, kipi kiwekwe wapi, uchafu gani uwekwe kwenye pipa gani!
Sisi tumefeli pakubwa kwenye usafi wa jumla, usafi wa jumuiya, usafi wa pamoja, mipangilio na mipango miji, uchakataji utunzaji na uhifadhi wa taka pamoja na mazingira.
Sisi bado tuko kwenye enzi pangu pakavu tia mchuzi. Nikioga mimi na kusafisha nyumba yangu inatosha kabisa, vingine havinihusu.
Kama kuna uchafu nitatupa mtaroni au pembezoni mwa barabara ama kwenye jalala la wabeba uchafu lakini bila utaratibu wala mpangilio.
Mbebataka sio makini anajibebea tu, na anakwenda kutupa bila mpangilio, yeye mwenyewe mchafu, vifaa anavyotumia ni duni na ni vichafu, gari ni chafu bovu, pengine kuzidi uchafu wenyewe.
Kwenye gari ya taka hujui uchafu ni upi, gari ni ipi, dereva ni yupi na wahudumu ni wepi. Unachoona ni uchafu unaotembea, maana hakuna tofauti.
Wazibua mitaro na wasafisha barabara hali kadhalika, mtaro unazibuliwa kwa vifaa duni uchafu unawekwa pembeni na kama utazolewa kwa wakati hauzolewi wote! Wasafisha barabara vivyo hivyo kingo na bustani za barabara zimetengeneza miinuko kutokana na uchafu unaozolewa kuwekwa huko na ukichukuliwa hauchukuliwi wote.
Kama janga la kunguni likivamia Tanganyika hatutaathirika sana, maana kunguni chake ni uchafu. Penye uchafu kunguni atanenepa na kunawiri.
Sisi wenyewe tu wasafi sana; tunaoga maratatu kwa siku, tunafua kila siku, baadhi haturudii nguo, nyumba zetu ni safi, tunafagia na kudeki kila siku, hapo kunguni atakaa wapi!?
Kimbembe ni kwenye mazingira yetu hayana mipangilio, ni machafu, hayahudumiwi ipasavyo, hatuyajali, kama kunguni wakija watakimbilia huko.
Kilichowaponza Ufaransa ni uchafu wa miili, mazingira ni safi sana lakini miili ni majanga. Tofauti na sisi miili ni misafi sana lakini mazingira ni machafu sana.
Je, tunadhani hii ni sifa? La hasha! Tatizo la kunguni Tanganyika lipo ila linafunikwa kuficha aibu. Sehemu nyingi za jumuiya kunakokutanisha watu wengi hili tatizo lipo kwenye shule hasa shule za bweni, Vyuoni (UDOM wamevunja ukinya), hospitalini, kwenye usafiri wa umma (hasa baadhi ya mabasi ya mikoani) vituo vya mabasi nk.
Pengine tunaweza kuteswa na kunguni wetu wenyewe wa kienyeji lakini sio ma broiler toka ufaransa. Kikubwa sasa ni kubadili mitazamo yetu, Mazingira yako ni yangu na ni yetu sote..
Namna tunavyotunza miili na nyumba zetu ndio tunavyopaswa pia kutunza mazingira yanayotuzunguka kwa wakati husika, iwe kwenye chombo cha usafiri, eneo la wazi, sehemu ya mapumziko, barabarani nk.
Mazingira yakiwa safi, nyumba zikiwa safi, miili ikiwa safi si kunguni tu atakosa pa kukaa pamoja na magonjwa mengine yote yatokanayo na uchafu.
Good afternoon Tanganyika