DOKEZO Songea: Shule ya Msingi Mshangano ina vyoo vichafu sana. Ina wanafunzi 914 na matundu 10 ya vyoo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Hakuna anayejali

JF-Expert Member
Jun 3, 2023
258
269
Ndani ya Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma, inapatikana Shule ya Msingi Mshangano. Shule hiyo ina vyumba 6 vya madarasa na wanafunzi zaidi ya 900.

Pamoja na kuwa imeanzishwa miaka michache iliyopita, changamoto za uzembe zinajitokeza katika shule hiyo, kama vile ukosefu wa maji ambao huwalazimu watoto kwenda kuchota maji mtoni, ambapo kuna hatari ya kusukumana au hata kutoweka wakati wakifanya hivyo.

Licha ya hilo, kuna matundu 10 ya vyoo, ambapo vyoo 4 ni vya kike na 6 ni vya kiume. Kila vyoo kuna tundu moja lililoibiwa au kutokuwa safi kutokana na uhaba wa maji, hali ambayo inaleta hatari ya kuenea kwa magonjwa.



==

Mwalimu wa Shule ya Msingi Mshangano amesema ni Kweli shule ina matatizo mengi kukiwemo tatizo la Vyoo.

Amesema shule ina Wanafunzi 914 ila Matundu ya Vyoo yapo 10 tu. Vyoo vinajaa kila baada ya wiki mbili. Sababu ya Vyoo kujaa haraka ni havikujengwa Vizuri kwa sababu mabomba ya majitaka ni madogo hayapitishi Uchafu. Pili vyoo vimejengwa karibu na Madarasa hivyo hata kusoma kwa watoto ni changamoto.

Pia vyoo vya Walimu ni vidogo kiasi kwamba kama mwalimu ni Mnene hauwezi kuingia ukaenea sababu vyoo hata ndoo ya maji haikai. Ndo inakaa nje mwalimu ndo unaingia ndani.

Kuchakaa na Uchafu wa Vyoo unasababishwa pia na Shule kutokuwa na maji. Wanafunzi wanapeana zamu kwenda mtoni kuchota maji ya kutumia chooni na kufanyia Usafi(Maji si safi wala Salama). Maji yanayochotwa huko mtoni hayafai kutumia, hivyo maji ya kunywa na Kupikia wanaazima kila siku kwa majirani waliozunguka Shule hiyo kwa sababu Wanafunzi wanakula Shuleni. Wanafunzi wanapokula wanakunywa na maji kutoka kwa Majirani.

Mwalimu ameongeza vyoo havijajengwa kitaalamu kwa sababu watoto wa kike na kiume wanatumia mlango mmoja hata vyoo vya Walimu.

Hivyo Mwalimu Fatuma ametumia Hela yake kutenganisha vyoo. Pia Shule haina hela ya kuita gari kila Wiki mbili kutoa maji taka, kuna mtu anawasaidia kuja kuzibua kila baada ya wiki na Mwalimu Mkuu anampa 25000 kutoka Mfukoni mwake kwani Tangu Mwezi wa Kwanza hawajapata hela kutoka Serikalini ya kuendesha Shule.

Kaomba kuvutiwa maji kama haiwezekani Wachimbiwe kisima na kuvutiwa umeme ili waweze kuweka Pump ya kuvuta maji sababu Shule ipo mjini. Wiki iloisha kaitisha kikao cha Wazazi ili wasaidie kuvuta maji na kubadilisha mabomba ya majitaka vyooni ili kusilipuke magonjwa kutokana na mvua zinazonyesha.

---
Dokezo limefanyiwa kazi, zaidi soma Songea: Vyoo vya shule ya Msingi Mshangano vyazibuliwa na kubadilishwa sink

IMG_20240222_132256.jpg
IMG_20240222_132136.jpg
IMG_20240222_132136.jpg
IMG_20240222_132125.jpg
 
Ndani ya Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma, inapatikana Shule ya Msingi Mshangano. Shule hiyo ina vyumba 6 vya madarasa na wanafunzi zaidi ya 900. Pamoja na kuwa imeanzishwa miaka michache iliyopita, changamoto za uzembe zinajitokeza katika shule hiyo, kama vile ukosefu wa maji ambao huwalazimu watoto kwenda kuchota maji mtoni, ambapo kuna hatari ya kusukumana au hata kutoweka wakati wakifanya hivyo. Licha ya hilo, kuna matundu 10 ya vyoo, ambapo vyoo 4 ni vya kike na 6 ni vya kiume. Kila vyoo kuna tundu moja lililoibiwa au kutokuwa safi kutokana na uhaba wa maji, hali ambayo inaleta hatari ya kuenea kwa magonjwa.
View attachment 2912424View attachment 2912426View attachment 2912465View attachment 2912466
Hatari kubwa sana hii halafu kiranja mkuu anavaa saa ya million mia na uchafu.
 
Naomba kukumbushwa jina la hiyo shule tafadhali.

Jina la shule ndio hali niliyonayo kwa sasa.
 
nyonge mnyongeni lakini haki yake ....

vyoo ni vya kisasa hilo liko wazi shida ni usimamizi
Kiukweli ukiangalia tu hizi picha unajua shida ipo kwenye usimamizi wa shule huu ni uchafu wa hari ya juu hata wakiwekewa nini bado kutakuwa na shida tu nashauri wasimamie usafi kwanza wakati wakisubiri msaada na sio kuzidi kuharibu ili wasaidiwe.
 
Back
Top Bottom