Acha Kumwibia Mwajiri Wako

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,514
22,000
Moja ya sababu kuu kwa nini biashara ndogo ndogo hufungwa ni wizi wa wafanyakazi.

Unapomwibia mwajiri wako, unakausha mkondo ambao umekuwa ukimwagilia maisha yako na familia yako.

Ikiwa unaomba hongo na pesa kwa kutumia wadhifa wako serikalini, ujue unaibia umma. Ipo siku , wewe pia utateseka wakati majambazi, vibaka ama panya road watakapovamia gari ama nyumba yako ili wajipatie mali zako waondokane na umaskini uliowasababishia kwa wizi uliofanya hapo nyuma.

Amri ya 8 katika Biblia inaonya : Usiibe.

Na Waefeso 4:28 inasema, “Ikiwa wewe ni mwizi, acha kuiba.”

Tafadhali ripoti risiti kwa usahihi.

Acha kumdharau mwajiri wako.

Ripoti zawadi zote zinazotolewa na wateja.

Acha kuchukua vifaa kutoka ofisini kwako na kuvitumia kwa matumizi yako binafsi.

Acha kutumia kadi za mkopo za kampuni kwa manunuzi ya kibinafsi.

Acha kughushi saini.

Acha kughushi hesabu.

Mungu atakuwajibisha kwa mikataba ya siri yenye kukupatia manufaa binafsi.

Kumbuka ukiwa mwaminifu kwa machache, Mungu atakukabidhi mengi

Luka 16:10. Uwe mwaminifu kama Yusufu na utapandishwa cheo.

Fanya kazi kana kwamba unamtumikia Mungu, si mwajiri wako - Wakolosai 3:23.

Utabarikiwa ukiachana na wizi. .
 
Alisema TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
 
Hivyo vitabu vyote vilikuja kwa malengo maalumu; kwa ajili ya utumwa, ukiwajengea hofu watu ni rahisi kuwatawala.
Ulishawahi kujiuliza swali, 'huko vitani watu wanavyouliwa, kwa nini Mungu hatokei?'​
 
Binadamu kwa silika ni mbinafsi.

Kwa serikali au taasisi za umma kutegemea uaminifu wa waajiriwa ni kutwanga maji kwenye kinu. Hata kama si wote, watakuwepo wengi tu wa kutafuta fursa za kujineemesha kwa kukosa uaminifu.

Inatakiwa mifumo inayomlazimisha mwajiriwa kutenda ipasavyo. Asipoifuata anakamatika hima.
 
Walau mtu kaandika kitu Cha maana leo,lakini thread hii yaweza kukosa wachangiaji wengi kwakuwa kwa Sasa nadhani wizi umeshaingia hadi kwenye DNA ya watanzania.Wizi unarudisha nyuma maendeleo ya biashara aisee.Mwaka juzi nilimwajiri single mother Mmoja kwenye biashara yangu.Aisee Kila siku tulikuwa tunagawana mauzo na yule Mbwa .Nilimgunduaje?Haikuwa rahisi.

Mie huwa naamkia kwenye ajira yangu rasmi serikalini,baadaye muda ukiisha wa serikali nakwenda kwenye biashara.Kwahiyo ilikuwa rahisi kwake kurekodi baadhi ya mauzo na mengine akaacha.Mie na wife tulihisi kutokana na mabadiliko ya mavazi na lifestyle ya yule mfanyakazi.Lakini tulijua kuwa kumfukuza mtu KAZI kwa hisia tu si sawa.Mwezi wa nne mwaka huu nikafunga CCTV camera.Nilizifunga mchana kweupe na yeye akiwepo na nilimwambia ili ajue na arekebishe mwenendo,lakini mwizi ni mwizi tu.Hakuacha kutorekodi mauzo.Baada ya mwezi tu,tulimuonyesha live anachofanya tukiwa hatupo.Hapohapo nikamfukuza kazi.Sasa anazurura tu kama mbuzi asiye na mchungaji.
 
Kambi ya Fisi ni kamtaa fulani tu hapa chuga wala hakunaga fisi wezi mkuu 😂
Ni Kweli WAAJIRIWA waache wizi,

Wakati huo huo, waajiri watoe mikataba ya ajira Kwa watumishi Hasa sekta binafsi.

Waeza Kuta mtumishi ana miezi Hadi sita bila mshahara, akinunua shati jipya tu, anaonekana ameanza wizi.

HAKI na WAJIBU huenda sambamba.
 
Ni kweli kabisa
 
Back
Top Bottom