Acha Kumwibia Mwajiri Wako

Acha Kumwibia Mwajiri Wako

Moja ya sababu kuu kwa nini biashara ndogo ndogo hufungwa ni wizi wa wafanyakazi.

Unapomwibia mwajiri wako, unakausha mkondo ambao umekuwa ukimwagilia maisha yako na familia yako.

Ikiwa unaomba hongo na pesa kwa kutumia wadhifa wako serikalini, ujue unaibia umma. Ipo siku , wewe pia utateseka wakati majambazi, vibaka ama panya road watakapovamia gari ama nyumba yako ili wajipatie mali zako waondokane na umaskini uliowasababishia kwa wizi uliofanya hapo nyuma.

Amri ya 8 katika Biblia inaonya : Usiibe.

Na Waefeso 4:28 inasema, “Ikiwa wewe ni mwizi, acha kuiba.”

Tafadhali ripoti risiti kwa usahihi.

Acha kumdharau mwajiri wako.

Ripoti zawadi zote zinazotolewa na wateja.

Acha kuchukua vifaa kutoka ofisini kwako na kuvitumia kwa matumizi yako binafsi.

Acha kutumia kadi za mkopo za kampuni kwa manunuzi ya kibinafsi.

Acha kughushi saini.

Acha kughushi hesabu.

Mungu atakuwajibisha kwa mikataba ya siri yenye kukupatia manufaa binafsi.

Kumbuka ukiwa mwaminifu kwa machache, Mungu atakukabidhi mengi

Luka 16:10. Uwe mwaminifu kama Yusufu na utapandishwa cheo.

Fanya kazi kana kwamba unamtumikia Mungu, si mwajiri wako - Wakolosai 3:23.

Utabarikiwa ukiachana na wizi. .
Mafisi yameshiba kwenye kambi yao yanaanza kuleta ujuaji na kujidai kwamba yenyewe hayaibi 😂😂😂
 
Nyie lieni, imbeni shaurini mtakavoweza ila mi nikipata upenyo wa hela ya maana siachi hv hv! Mambo ya kusema utalipwa/ utalipwa ni uongo mteule


Unaweza jinyima vyote ukaishia kua maskini na wakati kuna wanyagu daily wanachezesha hesabu/ wanadanganya bei kwenye risiti na Wana ukwasi wa maana
 
Hahaha labda kambi ya upinzani ila kambi ya fisi akija simba wote mnatawanyika😂😂
Fisi ndio hupora mlo wa Simba na sio Simba kupora mlo wa fisi.

Tuendelee kujadili namna ya kuacha kuiba, hili ni kwetu binadamu hususani watanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom