Accidents at Kibaha: A Scientific Reason?

Yote hayo unayosema yanaweza kuwa ni kweli.. lakini hayajibu kwanini ni Kibaha? Kwanini ajali hizi zisitokee Kimara au eneo lolote kabla ya kufika Kibaha?

Wahusika wafanye Safety Audit.........................pleeeeaaaaase na ripoti iwekwe wazi.......unajua compromise nyingi zinafanyika na wataalamu wetu they get away with it easily.......................halafu zikitokea ajali wanaanza kudai.....ohh madereva si makini (which could be the reason).......but lets check these basics....za design halafu ndio tuanze kunyoosha vidole..........
 
Inasemekana hiyo gari haikuwa na break, kama hili ni kweli basi haikustahili kuwepo barabarani. Mpaka hapo owners wa magari watakapokuwa wanapigwa faini kubwa na hata kupewa kifungo ili kuhakikisha magari yasiyo kuwa na ubora wa kuwa barabarani hayaingii barabarani basi ajali za kutisha kama hii ya jana zitaendelea mara kwa mara kuwaangamiza Watanzania kwa miaka mingi ijayo. Pia madreva wengi hawastahili kuwa barabarani.

Majuu hupewi leseni mpaka upimwe macho yako kuona kwamba unaona vizuri na kama huoni vizuri basi itakulazimu ununue miwani ya kukuwezesha kuona vizuri, hili bongo halipo maana rushwa mtindo mmoja hata hujui sheria za barabara unaweza kuwa na leseni au kuendesha bila leseni.

Gari kuwa au kutokuwa na break ni one thing...............design ya barabara pia can be a factor........ule mtaro pale kibamba unatisha aisee.....au nyie wenzangu mnauonaje..............hata kama gari lilikosa break....ule mtaro/mfereji nauona ni chinja chinja..........inasikitisha sana

Mkuu Lole Gwakisa/Fundi Mchundo/Morani75/Webby.......tupeni shule tafadhali..........
 
Jamani kuna suala la "fatigue" usingizi kwa madereva pia, hili nalo inatakiwa lipewe umuhimu wake katika suala zima la usalama barabarani. Je nafasi yake ni ipi? Kwa ajali ya jana, mie nahisi na usingizi pia huenda ulichangia kusababisha ajali kwa upande wa dereva wa lori.
 
Matatizo yafuatayo yanaweza kuchangia



1. Fatigue, kwa wanaotoka mikoani, kibaha ni almost kama umeshafika DSM

2. Haraka ,kwa wanaoenda mikoani, Kibaha ni sehemu nzuri sana ya kuanzia vurugu ya kuendea mikoani



Haya nimezungumza ukiondoa factors zingine za rushwa, uchakavu wa vyombo n.k na tabia zetu

Je ajali huwa zinatokea mahali ambapo barabara imenyoka sana? if so ,that is a big dead problem!
 
Can somebody articulate why it seems there is some kind of a pattern or a logical explanation of why some of the most grisly accidents have happened in or near Kibaha for many many years now? Is there any scientific reason for these occurrences that our rulers have overlooked?
Nakubaliana na wewe MKJJ kwa hii scientific approach to solving a nagging problem.
Suala la barabara kati ya DSM na Mlandizi linaanza kuwa na utata kutikana na sababu za kisayansi.
Naleta sababu kama tatu kuu
  1. Barabara ni FINYU SANA na kila maboresho ya barabara hii yana kumbwa na kelele kubwa za fidia toka kwa wananchi, kitu ambacho kinanyima fursa ya hata kuwa na 4 lane 2way highway.Tukumbuke kuwa hiki kipande ndio mlango mkubwa kuliko yote nchini kuingia jijini DSM
  2. TOPOGRAPHY-cheki miinuko na mabonde toka Kimara hadi Mlandizi. Maboresho yote yamekwepa kukata vilima na kujaza mabonde katika juhudi za kukwepa gharama.Sasa hivi kuna vikona vya ajabu na vimiinuko/vimteremko vya kuudhi hasa kwa magari makubwa, bila kuongeza upana wa barabara kama ilivyo Chalinze -Morogoro(3lane,2 way)
  3. Kutokana na kuboreka kwa teknolojia ya magari, mengi yanabeba mizigo mikubwa zaidi na hata madogo yanakwenda spidi kubwa zaidi , hivyo kuongeza uwezekano zaidi wa kuwa na ajali, tena mbaya zaidi.(severity of accidents increase with better roads)
MKJJ ukiondoa masuala ya uzembe wa madereva, gari kupata hitilafu za ghafla kama breki kufeli, ukweli unabakia pale pale kuwa barabara hii kipande cha DSM- Mlandizi sasa hivi kimepitwa na wakati na ni vyema tukaanza kuipanua au kama ambavyo serikali imeanza, kujenga barabara mbadala kama ya Bagamoyo-Msata.
Naomba kutoa hoja!!!!
 
Dogo yuko right kabisa... umeweka kwenye jukwaa la siasa!!! Politicizing everything may not be the best thing!!!

kumbuka baadhi yetu tuna interest kwasababu tunaishi au tumewekeza maeneo hayo

This just goes to show that there is politics in everything. It's unavoidable!
 
Tatizo ninaloliona ni kwamba magari yooote yanayotoka bara (ukiondoa Lindi na Mtwara) lazima yapite Kibaha. Kwa hiyo utakuta tuna barabara moja tu ya kuingia mjini tangu uhuru (karibu miaka 50 sasa) wakati magari yameongezeka mara dufu na mahitaji ya kuja mjini yanaongezeka.

Pia nadhani serikali ingekubali kuhamia Dodoma, tungepunguza msongamano kwa kiasi fulani kama walivyofanya nchi nyingine mfano Nigeria, Uturuki, Kenya , tukaiacha Dar kwa ajiri ya wafanya biashara tu.
 
Huu mjadala safi sana. Ila kwa wengi waliojadili hapa, wanafanya makosa yaleyale ya wanasiasa. Hii kitu nitaiandika siku zote. Traffic Engineering ni somo gumu sana na linalohitaji uzoefu wa hali ya juu. Matatizo ya kuvamia hii kazi ya watu huwa ni ajali hizo zisizo na kichwa wala miguu. Kwenye ujenzi, kuna sheria zake ambazo wanasema "structure iwe nzuri, economical na iweze kuhimili mzigo (load) na kazi yake inayotakiwa kufanya".

Kwenye Traffic Engineering, inabidi Wahandisi wafuate matakwa ya watu na akili zao za kufikiri. Kwa kuangalia akili zetu hapa Tanzania, nchi ambayo viongozi na watu wenyewe hatuheshimu sheria, inabidi traffic engineer wajue hii kitu na wanapochora/kujenga barabara basi iwe akilini kuwa sisi tuna tabia hiyo.

Unaweza kupanua barabara na kuziweka kama wengi wanavyodai ila ikija semekana nyumba ya mjomba/wakwe/shangazi nk iko barabarani na inabidi ibomolewe, wewe utakuwa wa kwanza kuja hapa kulia na kuweka picha jinsi ndugu zako walivyonyanyaswa.

Njia ya pili ni KUWALAZIMISHA watumiaji barabara kupunguza mwendo mara wanapofika maeneo kama hayo na ikibidi kupunguza mwendo. Huwa kuna njia nyingi sana za kulazimisha dereva apunguze mwendo kabla hajafika sehemu hii (kwa aliyesomea highway/road design anafahamu). Labda niandike tatu:
1. Kuweka Kamera na warning kibao mapema kuwa kwenye mteremko/kilele cha mlima, kuna kamera inayorekodi kila kitu (hii kwa Tanzania haitasaidia sana).
2. Kuweka/kujenga zig zag (S shape) ya barabara kabla ya kufika eneo hilo ambapo huwafanya madereva wawe macho na kuongeza concentration zao kabla ya kufika eneo la hatari (hii nayo huhitaji eneo kubwa zaidi na inaanza kupandisha bei.
3. Kuharibu kwa makusudi kipande cha barabara mita kadhaa kabla ya kufika eneo la hatari. Hii inaweza pia kufanywa kwa kujenga kabarabara ya mawe au lami na juu kuweka kokoto (zikiwa zimeshikiliwa na lami). Hizi zitafanya dereva akifika hapo, matairi yanaanza kupiga kelele sana kutokana na kuzipitia kokoto/mawe na moja kwa moja inamshutua (inaudhi/kusumbua sana) na kumfanya aamke na kuweka concentration kwenye kuendesha na kuchunga alama za barabarani.


Labda mwisho niseme kuna njia nyingine wanatumia wenzetu, ni kuwa wanaweka vyuma vinavyong'aa nyekundu katikati mwa barabara (lanes), si ndefu sana ila kwa Tanzania inabidi viwe vingi na kila anayedhubutu kuingia upande wa mwenzake, matairi yataipata habari yake yaana hadi unayahurumia na mwenyewe atarudi upande wake. Ila zaidi ya makelele, sidhani kama yanaleta madhara kwenye gari.
attachment.php
 

Attachments

  • Traffic sign.jpg
    Traffic sign.jpg
    20.9 KB · Views: 85
Can somebody articulate why it seems there is some kind of a pattern or a logical explanation of why some of the most grisly accidents have happened in or near Kibaha for many many years now? Is there any scientific reason for these occurrences that our rulers have overlooked?

Kwa sababu siamini kama ni wingi wa magari au ufinyu wa barabara tu unaweza kuelezea ajali hizi. Kuna kitu kinasababisha na nina uhakika siyo cha kishirikiana lazima kuna sababu ya kisayansi ya matukio haya.

Tembeleeni tovuti ya "Bobo" ina picha za ajali mbalimbali za vyombo vya usafiri hasa Bongo.. na mnaweza kupata picha ya jinsi gani kuna mahali kuna tatizo ambalo linaweza kuelezeka kisayansi na kutatulika kwa kiasi kikubwa kisayansi.

hicho kipande(in or near kibaha) ni BOTTLE NECK
nafikiri mtanielewa namaanisha nini nikisema bottle neck,sasa ukichanganya na
FATIGUE,UZEMBE,UBOVU WA MAGARI,POOR ROAD DESIGN AND SIGNS,LIGHTS matokeo yake ni DISASTER.
 
HAKUNA MTU ANAJALI...Ajali bongo zimezidi mno na Watanzania wengi wanaamini ni kazi ya Mungu.
Mpaka siku kiongozi maa hiri atakapojitokeza na kulivalia njuga hili swala....tutaendelea kuuwa kwa ajali kama inzi
 
Huu mjadala safi sana. Ila kwa wengi waliojadili hapa, wanafanya makosa yaleyale ya wanasiasa. Hii kitu nitaiandika siku zote. Traffic Engineering ni somo gumu sana na linalohitaji uzoefu wa hali ya juu. Matatizo ya kuvamia hii kazi ya watu huwa ni ajali hizo zisizo na kichwa wala miguu. Kwenye ujenzi, kuna sheria zake ambazo wanasema "structure iwe nzuri, economical na iweze kuhimili mzigo (load) na kazi yake inayotakiwa kufanya".

Kwenye Traffic Engineering, inabidi Wahandisi wafuate matakwa ya watu na akili zao za kufikiri. Kwa kuangalia akili zetu hapa Tanzania, nchi ambayo viongozi na watu wenyewe hatuheshimu sheria, inabidi traffic engineer wajue hii kitu na wanapochora/kujenga barabara basi iwe akilini kuwa sisi tuna tabia hiyo.


Labda mwisho niseme kuna njia nyingine wanatumia wenzetu, ni kuwa wanaweka vyuma vinavyong'aa nyekundu katikati mwa barabara (lanes), si ndefu sana ila kwa Tanzania inabidi viwe vingi na kila anayedhubutu kuingia upande wa mwenzake, matairi yataipata habari yake yaana hadi unayahurumia na mwenyewe atarudi upande wake. Ila zaidi ya makelele, sidhani kama yanaleta madhara kwenye gari.
attachment.php

You are right, tunapodiscuss hapa engineers have arleady discussed this again and again, Undegraduare projects, masters researches etc zimefanyika sana, infact most of engineering problems Tanzania local engineers wana majibu . Problem inakuja kwenye implementation, ufinyu wa bajeti na politics.
 
Gari kuwa au kutokuwa na break ni one thing...............design ya barabara pia can be a factor........ule mtaro pale kibamba unatisha aisee.....au nyie wenzangu mnauonaje..............hata kama gari lilikosa break....ule mtaro/mfereji nauona ni chinja chinja..........inasikitisha sana

Mkuu Lole Gwakisa/Fundi Mchundo/Morani75/Webby.......tupeni shule tafadhali..........

Mkuu Ogah,

Wataalamu Tanzania wapo. Ila tatizo kubwa kama walivyosema wengi ni SIASA kuingizwa hapa. Kazi za ujenzi ni kazi zenye hela nyingi sana. Na kwenye hela nyingi sana ni kama mzoga, na fisi siku zote hawatakosekana.

Sasa hivi nasikia kumbe Mrema wa TANROAD aliajiriwa kinyemela. Sasa unafikiri huyu atakuwa huru kwenye kazi zake na hasa ukifikiria aliyemuajiri ni Chenge na Chenge ndiye Boss wake? Pesa za kuweka vizuizi vya barabarani na alama za aina mbali mbali ndiyo wanaweka ndani. Kuna njia nyingi sana za kupunguza ajali hapa Tanzania. Ila kama hatulalamiki na kuandamana, tutakufa kama nzi na hakuna atakayelalamika.

Kama ingelitokea siku watu wa Dar na Pwani wanaandamana hadi kwa waziri wa Miondombinuna kuzuia barabara hakuna kitu kupita, wangelianza kufanya kazi zao inavyotakiwa. Ila UZURI kwao Tanzania ni kuwa Gawanya uwatawale imefanikiwa kwa kipimo cha hali ya juu, zaidi ya hata Wazungu walivyofanya.

Kazi za ujenzi zote ziko hivyo. Punguza gharama wakati wa ujenzi. Wasipolalamika, tunamaliza term moja na tunapata cha kuahidi uchaguzi ujao. Tusipojifunza kulalamika na kuandamana/kugoma kama sheria/katiba inavyoturuhusu, milele tutabaki kuwa samaki na machozi yetu ndani ya maji. Hivi hata hao waliofiwa sasa hivi wangelijikusanya hadi kwa Waziri, wangeliungwa mkono na watu kibao. Ifike hatua watu wafungue macho.
 
Mzee mwanakijiji inaelekea una hamu ya kupata jibu hili. Kwa sababu wewe ndio umelianzisha nakushauri fanya uwezalo hata kama itachukua mwaka au zaidi upate jibu sahihi la swali lako la msingi. Hebu tafuta kwenye tovuti neno hili 'ROAD ACCIDENT AND BLACK SPOT', toka hapo utaona sehemu mbalimbali duniani wanavyojaribu kutatua tatizo hili. Si Tanzania tu.
FANYA UTAFITI
 
Kwa sababu siamini kama ni wingi wa magari au ufinyu wa barabara tu unaweza kuelezea ajali hizi. Kuna kitu kinasababisha na nina uhakika siyo cha kishirikiana lazima kuna sababu ya kisayansi ya matukio haya.

......talking of factors, one of them is.....watu kuendelea kufanya mambo kihovyohovyo tu. Breakdown ya rule of law ndiyo sababu mojawapo. Barabara kujengwa bila kuzingatia viwango, kwa maana kifisadi ikichanganywa hiyo na madereva kuendesha hovyo hovyo tu barabarani na mambo mengine kufanywa hovyo hovyo tu, matokeo yake ni pamoja AJALI nyingi. Siyo barabarani tu! Hata kwenye mahospitali wagonjwa are being butchered by surgeons! Angalia other sectors, nako hivyo hivyo. Mambo ya hovyo tu!

Jana wale askari walofika pale hata gloves hawana. Tumeona wali-improvise kwa kuvaa mifuko ya rambo instead. What a dreadful scene that was katika kutoa mabaki ya ile miili! Halafu mijitu mingine inatembelea migari ya mamilioni kwenye misafara ya migari hiyo isopungua 30 kwend eapoti kumpokea mtalii flani! Disgusting.

Matokeo ya kuongozwa na directives au mbinu watoazo toboa tobo!
 
Tunapoongelea ajali barabara tunatakiwa kuangalia vitu vikuu vitatu

1. Road Factors: Hapa tunaangalia vitu kama road design (Structural & Geometric designs)- Katika hili tunaagalia uwezo wa barabara kubeba mzigo (Load carrying capacity), Upana wa barabara, number of lanes, adverse camber etc

2. Vehicle Factors: Hapa tunaangalia vehicle design and maintenance, ubora wa gari kuwa barabarani, vehicle camber etc

3. Driver Factors/ Behaviour: Hapa tunaangalia zaidi human factor, Je drivers wanakuwa trained vya kutosha kabla ya kukabidhiwa leseni?, Kuna programme za kuwaandaa madereva kutambua hatari kabla haijatokea (hazards perception), Madereva kuwa na sound mind not under influence of drugs/ Alcohol, fatique (Kuchoka kwa kendesha kwa muda mrefu au kuwa na usingizi). HILI NI MUHIMU SANA KWANI RESEARCH ZINAONESHA KUWA 93% OF ACCIDENTS HUWA NI HUSABABISHWA NA (DRIVERS FACTOR/BEHAVIOUR)

Back to Mwanakijiji's question: Ajali inaweza kusababishwa na any or combinations of the above factors. The worse scenario ni pale kunapokuwa na combination of all of the above factors, Kwa kuwa hawa madereva waendesha magari hayo hayo wakiwa ni wao wenyewe sehemu mbalimbali za nchi barabarani, Kuna Chance kubwa sana kuwa Eneo la Kibaha likawa na combination of all three factors (Yaani Road + Vehicles + Driver factors):

My take: Kwa kuwa serikali inasema haina uwezo wa kusimamia vizuri ubora wa madereva na magari yao ni dhahiri kabisa kuwa Tunaweza kupunguza ajali kwa kuimarisha UBORA WA BARABARA ZETU: Badala ya wanasiasa kuendekeza ufisadi kwa kula dili na makandarasi kujenga low standard roads at overstated prices, Tuimarishe hizi barabara angalau kwa kuzipanua yaani kuwe na Njia mbili kwenda, njia mbili kurudi (Two ways four lanes roads) Kama ilivyo kwa UBUNGO-MLANDIZI au UBUNGO-MWENGE(SAMNUJOMA) Kwa kuanzia iwe DAR mpaka CHALINZE.
 
My Conclusion: Kwa kuwa serikali inasema haina uwezo wa kusimamia vizuri ubora wa madereva na magari yao ni dhahiri kabisa kuwa Tunaweza kupunguza ajali kwa kuimarisha UBORA WA BARABARA ZETU: Badala ya wanasiasa kuendekeza ufisadi kwa kula dili na makandarasi kujenga low standard roads at overstated prices, Tuimarishe hizi barabara angalau kwa kuzipanua yaani kuwe na Njia mbili kwenda, njia mbili kurudi (Two ways four lanes roads) Kama ilivyo kwa UBUNGO-MLANDIZI au UBUNGO-MWENGE(SAMNUJOMA) Kwa kuanzia iwe DAR mpaka CHALINZE.

yep! mabo yale nlotaja...common denominator being, mambo kufanyika hovyo hovyo! Kubobea kufanya mavitu ya hovyo hovyo!
 
sehemu nyingi Tanzania magari yanapishana, milimani, mabondeni, kwenye kona n.k lakini hakuna mahali panapovutia ajali zaidi kama Kibaha why?

Pamoja na ufinyu wa barabara, kuna mapepo ya ajali hapo. Ushirikina haukwekepi katika jambo hili. Madreva huamua kuchua maamuzi ambayo kama amepona ukimuuliza kwanini alikuwa anaovateki kwenye kona au mlima anaweza kukupa jibu la ajabu sana.
 
Je.. tuanzishe kampeni ya kusajili upya madereva wote baadaya kutimiza defensive driving course? Yaani, tuanza moja tena na madereva wetu katika kampeni mpya ya kitaifa kwa sababu ukiondoa hizo ajali za sehemu kama Kibaha kuna hizi ajali ambazo zinatokana na "aggressiveness" ya watu kama kuchomekeana n.k hasa katikati ya jiji na miji.
 
Back
Top Bottom