Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,060
hahaaa Ogah, mie niliishia kuwa Fundi Mchundo. Majaribio kadhaa ya kutaka kupandisha grade, yamekwama katika dakika ya mwisho na nikaamua kabisa kuachana na haya mambo ya barabara. Ila kumbukumbu imebaki kidogo.
Nafikiri hapo sijui kama utapata michoro yake. Wanaweza kuwa walilipua tu na mtu akachukua hela zake kwa kudesign barabara. Matokea yake ndiyo hayo.
Unafahamu miaka ya 90 nikiishi nchi za watu, kulikuwa na jamaa mmoja akiwa na Masters. Juu yake kulikuwa na Dr na Profesa mmoja. Ila hawa jamaa pamoja na shule kubwa zaidi ya jamaa, walikuwa siku zote wanakuja kumuuliza na walikuwa wanakiri kabisa kuwa wao wana makaratasi na jamaa ana KIPAJI na Uzoefu zaidi yao.
Ndiyo maana siku zote nawaasa watu kuwa Traffic Engineering, si kitu cha kusema "tujenge fly-over, tutenge barabara, tupanue barabara, tuongeze lane......." Ni zaidi ya hiyo. Unaweza kufanya vitu vyote na bado ajali zikaongezeka. Kuna trick nyingi sana hutumika kwa kucheza na tabia za binadamu. Ndiyo maana jamaa wengi walikuwa wakija na planing zao, yule mzee mwenye Master anaanza kucheka na kusema "ohhhhhh, hapa umetengeza MACHINJIONI".
Hebu jaribu kuwasiliana na watu wa Tanroad mkoa wa Pwani na Makao Makuu, wanaweza kuwa msaada mkubwa kwako. Ila kwa haraka haraka, Waziri na watu wa Tanroad, wangeliweka vile vyuma vya kutenganisha barabara/lane haraka sana sehemu zote zinazotokea ajali. Si wote watafuata ila usumbufu watakaoupata, utafanya wengi wawe na subira ya kutokuvuka upande mwingine ili ku-overtake. Sidhani kama vile vyuma ni aghali. Ukifanikiwa basi tujulishe ili tufurahi wote kwa kuwa kazi yako inaweza kuokowa maisha ya watu wengi kama si hata ya kwangu/ya kwako au ndugu zetu.