Accidents at Kibaha: A Scientific Reason?

Pamoja na kuwa magari ni mabovu na uzembe wa madereva, sababu kubwa ya ajali kati ya Kibamba - Chalinze ni miundombinu, magari ni mengi na barabara ni nyembamba, hiyo barabara wakiweka double roads ajalio zaitapungua kwa kiwango kikubwa mno. Badala serikali ishighulikie miundombinu na sababu halisi za ajali wao wanategemea hospitali ya Kibaha izidi kupokea maiti nyingi na majeruhi wengi wa ajali
 
kwa sisi wa kiroho zaidi tunajua hayo ni malango ya kuzimu. Lazima maombi makubwa ya kuvunja ngome hizo yafanywe maeneo hayo. Maeneo ya kikavu ilikuwa hivyo hivyo lakini baada ya walokole kufanya maombi na kuandika zaburi mbali kule kwenye mawe mtoni pale kikavu mashetani yakakimbia na malango yale yakafungwa.
Tukae kiroho zaidi. Amen
 
Kama kawaida "Reactionary Government", baada ya watu kusahahau kutakuwa kimya nothing will take place-mwaka wa uchaguzi huu.

Serikali yafikiria kuitanua barabara ya Morogoro

SERIKALI ipo katika mazungumzo na wahisani ili kuweza kupanua barabara ya Morogoro kuanzia Dar es Salaam hadi Chalinze, kwa kiwango cha njia mbili zitakazosaidia kurahisisha usafiri na kuondokana na ajali zisizo za lazima.

Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari Ruvu mkoani Pwani, kabla ya Rais Jakaya Kikwete kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Ruvu iliyopo Ruvu Darajani.

Alisema ajali nyingi zinazotokea katika eneo hilo hazitokani na wembamba wa barabara hiyo kama inavyofikiriwa, bali zinatokana na uzembe wa madereva ambapo wengi wao wameonekana wakiendesha kwa kukiuka kanuni za usalama barabarani ikiwemo kwenda mwendo kasi kupita kiasi, kulewa na madereva wengine hupitiwa na usingizi wakiwa waneendesha magari.

Dk Kawambwa amezungumza hayo ikiwa ni siku chache baada ya kutokea ajali mbaya katika eneo la Kibamba Darajani jijini Dar es Salaam, ambako watu 10 akiwamo mama mjamzito aliyepasuka tumbo, walifariki dunia papo hapo baada ya lori la mafuta kuiangukia daladala.

“Wembamba wa eneo ilipotokea ajali ya juzi na kuua watu wote kwenye daladala ni changamoto kwa serikali kutanua barabara hiyo, lakini ajali zinazotokea katika eneo hilo hazitokani na wembbama wa barabara, kwani ajali zinazotokea katika eneo hilo zinatokana na uzembe wa madereva,’’ alisema Dk Kawambwa.

Akizungumzia kuhusiana na mradi wa ujenzi wa barabara ya Bagamoyo, Dk Kawambwa alisema mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka huu na utaanzia kutanua eneo la Mwenge hadi Tegeta kwa ngazi ya njia mbili za kuingia na kutoka ili kusaidia kuondokana na msongamano wa magari katika barabara hiyo.

“Tunajua tutapata changamoto kubwa kwa wananchi waliojenga kandokando ya barabara hizo tunazotaka kuzitanua, lakini tutajitahidi kwenda na wakati kwa kuendelea na ujenzi huo huku mazungumzo na wananchi hao katika maeneo mengine ambayo yatakuwa bado hatujayafikia yakiendelea ili kuhakikisha ujenzi huo unafanikiwa kwa kiwango cha njia mbili, alisema Dk Kawambwa.

Pia Dk Kawambwa alisema ili kuondokana na tatizo kubwa la msongamano wa magari ndani ya jiji la Dar es Salaam, kupitia mradi wa kutanua barabara 10 za jiji hilo la Dar es Salaam utafanyika kwa lengo la kurahisisha usafiri katikati ya jiji hilo.

Alisema mradi huo utafanya kazi kwa kutumia barabara tofauti na zilizo zoeleka katika usafiri wa daladala kama barabara ya Morogoro na Mandela.

Tunatarajia kutumia njia nyingine na hazitamlazimisha dereva kutumia barabara moja ya Morogoro ili afike Posta ama Ubungo bali ataweza kupita ya kutokea Kigogo na kumuwezesha kufika ubungo ama Posta hiyo ikiwa ni malengo ya kuondokana na msongamano wa foleni katika barabara hizo.
Aliongeza kuwa mradi huo pia utasaidia kuondoa mrundikano wa malori kuwa katika foleni moja na magari madogo hasa katika barabara ya Jangwani, ambapo imeonekana malori yakiitumia pamoja na magari mengine madogo ambapo mradi huo ukianza malori na magari mengine hayatakuwa katika barabara moja.

Mwananchi NP
 
Can somebody articulate why it seems there is some kind of a pattern or a logical explanation of why some of the most grisly accidents have happened in or near Kibaha for many many years now? Is there any scientific reason for these occurrences that our rulers have overlooked?

Kwa sababu siamini kama ni wingi wa magari au ufinyu wa barabara tu unaweza kuelezea ajali hizi. Kuna kitu kinasababisha na nina uhakika siyo cha kishirikiana lazima kuna sababu ya kisayansi ya matukio haya.

Tembeleeni tovuti ya "Bobo" ina picha za ajali mbalimbali za vyombo vya usafiri hasa Bongo.. na mnaweza kupata picha ya jinsi gani kuna mahali kuna tatizo ambalo linaweza kuelezeka kisayansi na kutatulika kwa kiasi kikubwa kisayansi.
Its true that the problem is technical.

Something to do with road alignment particulary the section between Kibaha and Chalinze. Research nyingi zimefanywa na wahandisi wa UDSM lakini sina uhakika kama policy makers wamepitia matokea yake kuweza kurekebisha tatizo hili.

Solution ya hili ni full reconstruction of that road section.
 
kwa sisi wa kiroho zaidi tunajua hayo ni malango ya kuzimu. Lazima maombi makubwa ya kuvunja ngome hizo yafanywe maeneo hayo. Maeneo ya kikavu ilikuwa hivyo hivyo lakini baada ya walokole kufanya maombi na kuandika zaburi mbali kule kwenye mawe mtoni pale kikavu mashetani yakakimbia na malango yale yakafungwa.
Tukae kiroho zaidi. Amen

Hayo malango ya Kikavu/ Kikafu yamefungwa lini kwa sababu mimi ni mhanga wa ajali ya ajabu sana iliyotokea hapo
 
Kama kawaida "Reactionary Government", baada ya watu kusahahau kutakuwa kimya nothing will take place-mwaka wa uchaguzi huu.

Serikali yafikiria kuitanua barabara ya Morogoro

SERIKALI ipo katika mazungumzo na wahisani ili kuweza kupanua barabara ya Morogoro kuanzia Dar es Salaam hadi Chalinze, kwa kiwango cha njia mbili zitakazosaidia kurahisisha usafiri na kuondokana na ajali zisizo za lazima.

...........................
Alisema ajali nyingi zinazotokea katika eneo hilo hazitokani na wembamba wa barabara hiyo kama inavyofikiriwa, bali zinatokana na uzembe wa madereva ambapo wengi wao wameonekana wakiendesha kwa kukiuka kanuni za usalama barabarani ikiwemo kwenda mwendo kasi kupita kiasi, kulewa na madereva wengine hupitiwa na usingizi wakiwa waneendesha magari.

...........................................

Mwananchi NP
i don't buy the idea ya uzembe wa madereva pekee.....Mh Waziri....acha hizo shenanigans.......get real

kuna sababu zinatolewa hapa eti barabara ni nyembamba
Jamani hebu wahandisi mtusaidie tunaposema barabara ni nyembamba mna maana gani.........10ft, 15ft, 20ft, 25ft and so on ...........je ni standard ft gani ya upana wa barabara inaweza kujustify ile ajali?..............
 
Mengi yamesemwa kuhusu upanuzi wa barabara ya Chalinze - Tanga, ikiwa ni pamoja na ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara ya Kilosa - Dumila - Handeni - Msata.

Mojawapo ya hayo mengi ni kuwa " Waziri wa Fedha ndugu M. Mkullo mbunge wa Kilosa, Waziri wa Miundo Mbinu ndugu S. Kawamba mbunge wa Bagamoyo ikiwemo Msata, Katibu mkuu Miundo Mbinu - Chambo kutoka Tanga, wote wana mikono yao katika miradi hii, wakiivutia ngozi upande wao"

Baadhi ya wabunge walifikia hatua ya kuwaambia watawala wetu ikiwa hawajui kufa basi wakachungulie makaburi. Mimi nawasogezea makaburi hayo hapahapa mjionee kisha fikra zenu potofu zilizojaa upendeleo zifunguke.

Barabara ya Chalinze - Dar (Morogoro Road) inakusanya karibu magari yote yanayotoka mikoani na nchi za jirani kuingia jijini. Sasa ni kipi kilichowafanya waipe kipaombele ile ya Tanga na kuacha ya Dar? Huu ni ulevi wa Madaraka?

Suala la watumishi kuchelewa makazini, kutumia nishati kubwa ya mafuta na muda mwingi kwenye foleni vimeshindwa kuzibua vichwa vyenu. Sasa ni Imani yangu kwamba hili la Kibamba litawazibua vichwa vyenu na mtachukua hatua. Mkishindwa basi tusuburi wawekezaji wenye akili zenu.
 
Nimeishasema ACHENI upuuzi wa kuweka picha hizi za wenzetu waliotangulia. Hivi hamna akili nini angalia MOscow wamelipuliwa analia walivyowasitiri wenzao kwenye picha .
http://news.bbc.co.uk/2/hi/in_pictures/8592322.stm
Hivi ungekuwa wewe ungependa upigwe picha katika hali hii. Tuwasitiri wenzetu badala ya kuwaweka katika hali hii. ACHENI UPUMBAVU WENU naomba wengine waongelee hili pia ni upuuzi tuache ()*^&*%^£%&*(+_)*&^^"£$%
 
Hali inasikitisha sana pole watanzania wenzetu ipo siku mambo haya yatakuja kupungua sana tumwombe mungu atuongoze nakutupa busara na hekima kuipenda nchi yetu na watu na kuenzi kwani hatuna pengine pa kwenda ni hapahapa tu ,Mungu Ibariki Tanzania
 
Nimeishasema ACHENI upuuzi wa kuweka picha hizi za wenzetu waliotangulia. Hivi hamna akili nini angalia MOscow wamelipuliwa analia walivyowasitiri wenzao kwenye picha .
http://news.bbc.co.uk/2/hi/in_pictures/8592322.stm
Hivi ungekuwa wewe ungependa upigwe picha katika hali hii. Tuwasitiri wenzetu badala ya kuwaweka katika hali hii. ACHENI UPUMBAVU WENU naomba wengine waongelee hili pia ni upuuzi tuache ()*^&*%^£%&*(+_)*&^^"£$%

Haya bwana mwerevu, nadhani wewe ungekuwa katika hali kama hiyo usingependa na ungewazuia watu wasikupige picha. Acha sisi wapumbavu tujadili issue za watawala wetu ni vipaombele vya Taifa letu.

Ili kuweza kukabiliana na ajali hizi zasizokoma tunahitaji wabia wa kizungu kwenye vichwa vya watawatala wetu.
 
i don't buy the idea ya uzembe wa madereva pekee.....Mh Waziri....acha hizo shenanigans.......get real

kuna sababu zinatolewa hapa eti barabara ni nyembamba
Jamani hebu wahandisi mtusaidie tunaposema barabara ni nyembamba mna maana gani.........10ft, 15ft, 20ft, 25ft and so on ...........je ni standard ft gani ya upana wa barabara inaweza kujustify ile ajali?..............

Ogah,

Kuna siku nilipigwa swali hili:
"Ili kuongeza driving confort, inabidi ufanye nini barabarani?"

Moja ya jibu ni kuongeza radius katika curve za barabara (ila gharama zinaongezeka) na pia kuongeza upana wa LANE za barabara. Kwa kawaida nyingi ziko kwenye mita 3 hadi 3.5m. Ila kwenye Express na Highwah (Tanzania hatuna highway (autodtrade kwa Kiitaliano) huwa zinakuwa na 3.75m

Hizi zote huongeza urahisi wa kuendesha. Ila kwa kiwango gani unapunguza ajali, hilo ni swala jingine. Kuna maelezo niliandika nyuma kuwa Wahandisi na vyombo vya dola wasaidie kuwalazimisha Madereva kufuata sheria. Waweke Camera ikibidi na taa na kuwapiga faini madereva wote wanaofanya overtake sehemu hatari na ikibidi waweke vyuma vinavyotumika kutenga lane moja na nyingine. Kila atakayeingia upande mwingine, itabidi avipitie hivi vyuma ambavyo kwa kweli vinasumbua sana na mwenyewe utarudi upande wako.

Member mmoja aliandika kuwa sasa hivi kuna Mkonga, hizi Camera zinaweza kuwa zinapiga picha na kupeleka moja kwa moja kwa Saidi Mwema na Kikwete na pia huyo Waziri Kawambwa kama atataka. Pesa za faini zitumike kuendesha hiyo mitambo. Polisi wanunuliwe magari yenye camera na rada. Nina uhakika kila siku watakuwa wanaingia Euro 10,000 kwa uzembe wa madereva wa Kibongo kwa gari moja. Baada ya miezi sita, pesa yote imerudi na faida.
 
Bill,
Kweli hii inauma. Lakini ninachoweza kukuambia hata uwe na dual carriage the whole country bado ajali zitakuwepo na zitakuwa mbaya kama hivi hivi (yaani lives consuming). Kama ningepata nafasi ya kuishauri serikali na nikasilikilizwa, infrastructure ni kitu cha mwisho nitakachowashauri (in terms of priority). Ningekuwa na uwezo wa kufanya execution, tunaweza kupunguza ajali hizi kwa wingi sana bila hata serikali kusubiri kupata mabilioni ya kujenga barabara....we can still do something for whatever we have!!

Priority number 1: Change of driving behavior through training of drivers (on the focus on attitude/bahavior change, not how how to engage or disangage the gear as that all the drivers know about it). Drivers need to know how much his actions will have an impact in the society starting with his own life, lives of his family or immediate dependants, society, lives of those who would not reach home or permanently incampacitated because of the drivers actions; what he could do to be a defensive driver, to know that he is the only good driver and no one else, to know that the hero is the one who goes back home safely and by not causing any accident, by letting them know that the law may not be strict on them by his actions is known by God or Allah and has the final judgement, let the driver understand that his safety and safety of other road users is on his own hands....for sure the 80-90% of drivers will make informed decisions when driving. They can decide on which speed to drive at, at what time to overtake, at what time to apply breaks, etc. It is all about attitude and behavior!!! For now, I will stop here, tomorrow I will give priority number two!!! But it will not be the road!!
 
Nchi za wenzetu,magari yanakaguliwa na gereji zilizoidhinishwa na serikali .
Kama UK wana M.O.T sio kama bongo,kila mwenye gari ana gereji yake,so hakuna independent mechanic scrutinity ya gari.Pia madereva wetu wengu wanatumia ulezi kiasi fulani.

Zaidi ni barabara.Ajali ya kimamba tungekuwa na barabara pana zenye dual carrige hakuna kupishana ,mambo haya yangewisha.Angalia barabara ya Dar -Dodoma ilivyo finyu!!!!
Haya baada ya uhuru ,ndio yangekuwa muhimu zaidi .Sasa tumechelewa,hatuna leaders ambao wanacare !Wakati wa Mrema Home Affairs,alijitahidi kubadili usafiri wa mabasi kuwa mchana,kuliko usiku ,hii hatua ilipunguza kiasi ajali,lakini long term solution ni barabara tu,pana na hakuna kupishana,one way roadS!
 
Nimeishasema ACHENI upuuzi wa kuweka picha hizi za wenzetu waliotangulia. Hivi hamna akili nini angalia MOscow wamelipuliwa analia walivyowasitiri wenzao kwenye picha .
http://news.bbc.co.uk/2/hi/in_pictures/8592322.stm
Hivi ungekuwa wewe ungependa upigwe picha katika hali hii. Tuwasitiri wenzetu badala ya kuwaweka katika hali hii. ACHENI UPUMBAVU WENU naomba wengine waongelee hili pia ni upuuzi tuache ()*^&*%^£%&*(+_)*&^^"£$%

Mkuu nyati, kwani lazima tuwaige wazungu kwa kila wanachofanya? na hata kama hii ingekuwa kweli? kwa nini tusiwaige kwenye ujenzi wa barabara nzuri na mipango yenye kueleweka?

Wewe hapa labda ndiye mpumbavu na wala sio bill aliyeleta hii mada.
 
Nchi za wenzetu,magari yanakaguliwa na gereji zilizoidhinishwa na serikali .
Kama UK wana M.O.T sio kama bongo,kila mwenye gari ana gereji yake,so hakuna independent mechanic scrutinity ya gari.Pia madereva wetu wengu wanatumia ulezi kiasi fulani.

Zaidi ni barabara.Ajali ya kimamba tungekuwa na barabara pana zenye dual carrige hakuna kupishana ,mambo haya yangewisha.Angalia barabara ya Dar -Dodoma ilivyo finyu!!!!
Haya baada ya uhuru ,ndio yangekuwa muhimu zaidi .Sasa tumechelewa,hatuna leaders ambao wanacare !Wakati wa Mrema Home Affairs,alijitahidi kubadili usafiri wa mabasi kuwa mchana,kuliko usiku ,hii hatua ilipunguza kiasi ajali,lakini long term solution ni barabara tu,pana na hakuna kupishana,one way roadS!
Kaka look into SA, they have very good compared to ours, the number of accidents is much more than ours, there so many example, look on our Mandela Road, we experienced very fatal accidents previously, etc. The road or the vehicle doesn't cause accident. It is the person who make the use of that vehicle that causes accident. Studies shows that more than 90% of accident are caused by driving behaviors and not by defect equipments or road being used. They may have their influence as it happened for Toyota but very little (lets address 90% faster, we can make a progress) Brothers, if you a driver think of how many times did drive unsafely (cross-cutting, harsh braking, u-turns, overspeeding above speed limit, using service road for driving, not respecting pedestrians, driving under influence of alchol or drugs (even if medical drugs), driving while fatigued, etc) All these are main causative of accident.!!
 
Mkuu wangu Nanu ... jinsi ulivyochinja lugha hiyo hapo juu ... imebidi nitamani kurudi darasa la tatu kujifunza tena kidhungu. .......naomba tafadhali useme kuwa unatania.
 
Ogah,

Kuna siku nilipigwa swali hili:
"Ili kuongeza driving confort, inabidi ufanye nini barabarani?"

Moja ya jibu ni kuongeza radius katika curve za barabara (ila gharama zinaongezeka) na pia kuongeza upana wa LANE za barabara. Kwa kawaida nyingi ziko kwenye mita 3 hadi 3.5m. Ila kwenye Express na Highwah (Tanzania hatuna highway (autodtrade kwa Kiitaliano) huwa zinakuwa na 3.75m

Hizi zote huongeza urahisi wa kuendesha. Ila kwa kiwango gani unapunguza ajali, hilo ni swala jingine. Kuna maelezo niliandika nyuma kuwa Wahandisi na vyombo vya dola wasaidie kuwalazimisha Madereva kufuata sheria. Waweke Camera ikibidi na taa na kuwapiga faini madereva wote wanaofanya overtake sehemu hatari na ikibidi waweke vyuma vinavyotumika kutenga lane moja na nyingine. Kila atakayeingia upande mwingine, itabidi avipitie hivi vyuma ambavyo kwa kweli vinasumbua sana na mwenyewe utarudi upande wako.

Member mmoja aliandika kuwa sasa hivi kuna Mkonga, hizi Camera zinaweza kuwa zinapiga picha na kupeleka moja kwa moja kwa Saidi Mwema na Kikwete na pia huyo Waziri Kawambwa kama atataka. Pesa za faini zitumike kuendesha hiyo mitambo. Polisi wanunuliwe magari yenye camera na rada. Nina uhakika kila siku watakuwa wanaingia Euro 10,000 kwa uzembe wa madereva wa Kibongo kwa gari moja. Baada ya miezi sita, pesa yote imerudi na faida.

Sikonge Asante sana kwa ideas

Nitaanza na...........................
lets assume hiyo 3.75m ndio imejengwa plus lets pia assume kuwa sehemu ile iko kwenye curve na hivyo inahitaji transitions curves PAMOJA na ongezeko la upana wa barabara i.e. 3.75 + depending na design speed nk..........assume pia jamaa anatumia maximum attainable speed on that road........with that kind of a dicth kuna mtu atapona kweli?
Kweli gharama ya maisha ya watu KUMI NA MOJA plus vessels inaweza kuwa justified kwa kutoongeza upana wa lane of which it would have given those guys atleast room/zone ya ku-escape............kwa kweli kuwalaumu madereva pekee haitoshi......kuna kitu zaidi inabidi tuangalie.........mind you hizi barabara tumetumia pesa nyingi sana sana (ni madeni),...................

Kuhusu technology za ku-monitor traffic barabarani............pia naunga mkono mawazo yako.................hizi technology wala sio expensive kulinganisha na matukio ya kila siku ya barabani.............na kama ulivyosema huwa zinajilipa zenyewe in a short and/or long run..............tena siku hizi minara ya mawasiliano iko kila sehemu............sijui ugumu uko wapi

.......kuhusu vyuma vya kutenganisha lanes nakubaliana na wazo lako pia.........nakumbuka wali-install vitu kama hivyo ile Kawawa Highway (from Mkwajuni kuelekea magomeni i.e pale bondeni......utaona wametumia vile vyuma.......) nilikuw aniki-drive garai yangu ndgo kwa kweli nilikuwa najiuliza mara mbili mbili kabla sijahama lane.......vinasaidia sana............
 
did you notice kwamba wamesema watu zaidi ya 180 wamekufa kwenye junction hiyo miaka michache tu iliyopita?
 
Ogah,

Nafurahi kuwa mambo ya barabara unayafahamu. Maana baada ya kuona neno transition curves, nimeona kuwa kuna kalufundi ka barabara hapa.
Kwanza nianzie kuwa sijui kama nimekuelewa au wewe umenielewa. Ninaposema Lane ya barabara ni kuwa kipande kimoja cha barabara ambacho magari yanapita kwenda upande mmoja. Sasa upana wa 3.75m wa lane, huo uko kwenye high way pekee na Express Roads. Hizi nyingine zinakuwa chini ya hapo. Hii ni barabara maeneo ya Mikumi. Kama sikosei itakuwa na upana wa 3.5m kwa lane moja na upana wa barabara nzima ni 7.0m.
TanMikumiZebra.jpg

Ukiangalia hii kwa eneo hili inatosha sana. Kujenga double road hapa inakuwa kuongeza gharama za bure maana magari ni machache sana. Ila tu, hiyo inakwenda na kupunga speed kwa magari. Nafikiri kwa barabara kama hii inatakuwa kuwa 90km/hrs (maximum). Ila sitashangaa kusikia watu wanakwenda 150km/hrs speed ambayo nchi nyingi duniani hata kwenye highyway huruhusiwe. Ni Wajerumani pekee kama sikosei kwenye baadhi ya highway zao, unaweza kwenda speed ambayo ni akina Veyron, Ferrari, Porsche et el wanaruhusiwa kutumia lane ya ndani maana huko hakuna limit ya speed. Ukiingia wewe na sijui akina Toyota Celica, utawasikia jamaa wanavyokupigia horn, uondoe hilo tractor lako huko kwenye lane ya BIG BOYS.

Sasa ili wapunguze speed, hapo huwa hata Traffic wanasema wazi kabisa wakikumata "una bahati mbaya maana tunafahamu kuwa woote wanavunja max. speed limit". Sanasana wanaangalia nani kazidisha sana kile kiwango na huyo ndiyo wanamfukuza. Na magari yao Polisi ni kichekesho sana. Kuna kipindi kwenye TV nilishawahi kuangalia, gari la Polisi Opel Corsa ikaanza kuifukuza Ferrari. Jamaa akaona leo ngoja awaache kwenye mataa POLISI. Mama yangu, kile Ki-Opel kilikuwa kinakwenda hadi 350km/hr. Jamaa alivyosimama, akatoka nje na kuanza kuwauliza Polisi kama ile kweli ni Opel :)

Nakubaliana na wewe kitu kimoja, NI MARUFUKU kuweka kona kwenye bonde au mlima. Hapa wala haihitaji kuongeza upana wa barabara kwani HURUHUSIWI kulipita gari kwenye kona au mlima. Lile eneo la ile ajali, kuna bonde na kuna kona. Nashindwa kuelewa Mhandisi aliyeruhusu ujenzi wa hiyo barabara. Walau wangelizitenga kabisaaa hizo barabara kwa kuweka ukuta au fance katikati ili milele kuzuia watu ku-overtake kwenye maeneo hayo. Hiyo ya pili hapo chini ni nzuri sana kwani mnaweza kuindoa kwa muda na kuruhusu magari kutumia upande mmoja tu. Kuongeza upana wa Lane kunaongeza tu comfort ya kuendesha, ila hakusaidii sana kuongeza usalama. Lile eneo inatakiwa WALAZIMISHE madereva wafuate sheria. Kila njia itumie kuwalazimisha madereva. Hili la eti madereva wetu wazembe, si kweli. Binadamu ni kama Wanyama. Ukimpa mita moja, atachukua km1. Sasa dawa ni kumpa nini ili achukue 1m?

3491584609_92ca7aba50.jpg

wire_rope_dividers.jpg
 
did you notice kwamba wamesema watu zaidi ya 180 wamekufa kwenye junction hiyo miaka michache tu iliyopita?

Mkuu hiyo idadi nimei-note.............ndio maana nasema.................kusema uzembe wa madereva pekee si sababu inayojitosheleza.................hebu msome Mkuu Sikonge hapa chini................

Ogah,

Nafurahi kuwa mambo ya barabara unayafahamu. Maana baada ya kuona neno transition curves, nimeona kuwa kuna kalufundi ka barabara hapa.
Kwanza nianzie kuwa sijui kama nimekuelewa au wewe umenielewa. Ninaposema Lane ya barabara ni kuwa kipande kimoja cha barabara ambacho magari yanapita kwenda upande mmoja. Sasa upana wa 3.75m wa lane, huo uko kwenye high way pekee na Express Roads. Hizi nyingine zinakuwa chini ya hapo. Hii ni barabara maeneo ya Mikumi. Kama sikosei itakuwa na upana wa 3.5m kwa lane moja na upana wa barabara nzima ni 7.0m.
TanMikumiZebra.jpg

Ukiangalia hii kwa eneo hili inatosha sana. Kujenga double road hapa inakuwa kuongeza gharama za bure maana magari ni machache sana. Ila tu, hiyo inakwenda na kupunga speed kwa magari. Nafikiri kwa barabara kama hii inatakuwa kuwa 90km/hrs (maximum). Ila sitashangaa kusikia watu wanakwenda 150km/hrs speed ambayo nchi nyingi duniani hata kwenye highyway huruhusiwe. Ni Wajerumani pekee kama sikosei kwenye baadhi ya highway zao, unaweza kwenda speed ambayo ni akina Veyron, Ferrari, Porsche et el wanaruhusiwa kutumia lane ya ndani maana huko hakuna limit ya speed. Ukiingia wewe na sijui akina Toyota Celica, utawasikia jamaa wanavyokupigia horn, uondoe hilo tractor lako huko kwenye lane ya BIG BOYS.

Sasa ili wapunguze speed, hapo huwa hata Traffic wanasema wazi kabisa wakikumata "una bahati mbaya maana tunafahamu kuwa woote wanavunja max. speed limit". Sanasana wanaangalia nani kazidisha sana kile kiwango na huyo ndiyo wanamfukuza. Na magari yao Polisi ni kichekesho sana. Kuna kipindi kwenye TV nilishawahi kuangalia, gari la Polisi Opel Corsa ikaanza kuifukuza Ferrari. Jamaa akaona leo ngoja awaache kwenye mataa POLISI. Mama yangu, kile Ki-Opel kilikuwa kinakwenda hadi 350km/hr. Jamaa alivyosimama, akatoka nje na kuanza kuwauliza Polisi kama ile kweli ni Opel :)

Nakubaliana na wewe kitu kimoja, NI MARUFUKU kuweka kona kwenye bonde au mlima. Hapa wala haihitaji kuongeza upana wa barabara kwani HURUHUSIWI kulipita gari kwenye kona au mlima. Lile eneo la ile ajali, kuna bonde na kuna kona. Nashindwa kuelewa Mhandisi aliyeruhusu ujenzi wa hiyo barabara. Walau wangelizitenga kabisaaa hizo barabara kwa kuweka ukuta au fance katikati ili milele kuzuia watu ku-overtake kwenye maeneo hayo. Hiyo ya pili hapo chini ni nzuri sana kwani mnaweza kuindoa kwa muda na kuruhusu magari kutumia upande mmoja tu. Kuongeza upana wa Lane kunaongeza tu comfort ya kuendesha, ila hakusaidii sana kuongeza usalama. Lile eneo inatakiwa WALAZIMISHE madereva wafuate sheria. Kila njia itumie kuwalazimisha madereva. Hili la eti madereva wetu wazembe, si kweli. Binadamu ni kama Wanyama. Ukimpa mita moja, atachukua km1. Sasa dawa ni kumpa nini ili achukue 1m?

3491584609_92ca7aba50.jpg

wire_rope_dividers.jpg

Mkuu Sikonge.............shukrani kwa maelezo mengine yanayoangalia upande mwingine wa hii ajali...........hii ajali na nyingine zimenifanya niwaulize ma-consultant ninaopambana nao mara kwa mara.............nikawaonyesha picha na kuwapa maelezo jinsi eneo la ajali lilivyo............wakaniambia wanaweza kunisaidia ku-analyse that area in particular wakipewa data za kutosha..............ndio maana huko nyuma kwneye moja ya post nimesema kama kuna mtu anaweza kunipatia details za designs iliyofanyika ya barabra hii wanaweza kunifanyia design audit........nami ningemlipa jamaa........."vijisenti" toka mfukoni mwangu..............the person is qualified Transportation Professional Engineer PE na pia ni Fellow wa ICE UK..........yaani katimia..............ni member wa bodi kadhaa either kama Chartered/Fellow ikiwamo Australia, na Canada...........huyo ndio alinielezea kuhusu hizo "transition curves"...............elimu yangu ni ya kuunga unga kwenye mambo ya procurement................sikufanikiwa kama nyie wenzangu hapa JF...........wenye BScs, BAs, BLs, MAs, MLLs,MScs and PhDs..............

Kuhusu lane nilikuelewa vizuri sana.............nina imani wahusika wanakusoma...............asante kwa self descriptive pichas
 
Back
Top Bottom