ACACIA ni wezi, tukiungana hawana uwezo

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
10,496
13,565
GTs,
Nawashauri tusiwe waoga ktk kulinda rasimali zetu. Tulitishwa hata kipindi kile eti wauza madawa wana nguvu, ila mpaka sasa kila mmoja anajua kinachoendelea. Sasa hata kwa hawa mafia wezi wa ACACIA na kundi lao, hawana nguvu kabisa, maana ni wezi na wao wanajitambua, ingawa wanajikosha bado ni wezi.

Kwa tulioishi ulaya pamoja na wazungu tunajua jinsi walivyo wanafiki na wachoyo. Na kibaya zaidi wamekuwa wakituibia kupitia misaada, rasilimali zetu n.k., sasa ktk hili wataalamu wetu wamesema ukweli, na litasimama hivyo hivyo.

Tusimame tuungane, maana mafia hawa huwa na tabisa ya kuanzisha/kufadhili vikundi vya wapiganaji ili kuleta machafuko, ila najua kwa Tz hawawezi kwa sababu Taifa hili Mungu analipenda na Usalama wa taifa wetu wapo fiti ile mbaya.

Niwasihi tu wale wanafiki wanaopewa hela na mafia wasidhani kuwa wapo salama, utaifa kwanza utanzania kwanza!
 
Naungana na wewe kuwa tupiganie Rasilimali zetu mkuu, tatizo nao ACACIA sio kwamba walikuja kwa kificho, au kwamba tulishtuka tayari wapo mgodini, la hasha...... Walikuja kupitia mlango wa mbele, wakakaa na viongozi wetu wa Serikali ya CCM, wakaongea wakasaini mikataba na kuafikiana......kama kuna sehemu kwenye mikataba wamekiuka tuna haki sana ya kuwafanya tutakavyo........Mimi napendekeza tuanze na hawa waliotufikisha hapo..........Mafia huko CCM, tuwamalize nao kisha turukie hao wa nje.
 
Tujiandae na za kuwalipa.
Wao ndiyo watatulipa, hii kitu anaifanya Dkt Magufuli imepigiwa mahesabu ya mbali sana. Na kingine nikujuze tu ni kuwa wazungu linapokuja suala la udanganyifu investors wao huwa hawana mzaha, na ndiyo maana kwa sisi tunaojua mambo ya wazungu in and out hii kitu Dkt Magufuli ashikilie kabisa asiachie na watatulipa.
 
Vipi za samaki hakupiga mahesabu ya Mbali?
 
Wakati wa kuingia mkataba ccm huwa mnakuwa mbogo!
Mambo yakiharibika anasema tuungane!
Acheni unafiki nyie watu......
Nani asiyejua Wabunge kama tundulissu Na zitto walikuwa wanapiga kelele juu ya ufichwaji wa mkataba ya madini?
 
Kwenye hili namuunga mkono Magufuli.

Mtanzania mwenye akili timamu hawezi kupingana na hizi juhudi za rais.

Hawa kupe wanatunyonya halafu wanatucheulia vimisaada uchwara na sisi tunawaona kama ni miungu vile.
Watanzania tuwe wazalendo, tuipende nchi yetu pamoja na watu wake kwanza.
 
Tujiandae na za kuwalipa.
Wao ndiyo watatulipa, hii kitu anaifanya Dkt Magufuli imepigiwa mahesabu ya mbali sana. Na kingine nikujuze tu ni kuwa wazungu linapokuja suala la udanganyifu investors wao huwa hawana mzaha, na ndiyo maana kwa sisi tunaojua mambo ya wazungu in and out hii kitu Dkt Magufuli ashikilie kabisa asiachie na watatulipa.
 
Wachawi wa rasilimali zetu ni sisi wenyewe. Sheria zetu mbovu, ubinafsi na siasa kila mahali hata kwenye mambo ya msingi yasiyo hitaji siasa vitatutafuna hadi Yesu arudi. Maneño matupu bila vitendo ni kazi bure.
 
GTs,
Nawashauri tusiwe waoga ktk kulinda rasimali zetu. Tulitishwa hata kipindi kile eti wauza madawa wana nguvu, ila mpaka sasa kila mmoja anajua kinachoendelea. Sasa hata kwa hawa mafia wezi wa ACACIA na kundi lao, hawana nguvu kabisa, maana ni wezi na wao wanajitambua, ingawa wanajikosha bado ni wezi.

Kwa tulioishi ulaya pamoja na wazungu tunajua jinsi walivyo wanafiki na wachoyo. Na kibaya zaidi wamekuwa wakituibia kupitia misaada, rasilimali zetu n.k., sasa ktk hili wataalamu wetu wamesema ukweli, na litasimama hivyo hivyo.

Tusimame tuungane, maana mafia hawa huwa na tabisa ya kuanzisha/kufadhili vikundi vya wapiganaji ili kuleta machafuko, ila najua kwa Tz hawawezi kwa sababu Taifa hili Mungu analipenda na Usalama wa taifa wetu wapo fiti ile mbaya.

Niwasihi tu wale wanafiki wanaopewa hela na mafia wasidhani kuwa wapo salama, utaifa kwanza utanzania kwanza!
Nimeitoa humu JF. Itafakari bila u-Lumumba kwa kina. Kuna ukweli? Be calm please when reading this.
Hotuba ya jana ya Rais Magufuli ni ushahidi mwingine, kama bado kuna shaka, ya rule of state lawlessness ambayo mtukufu anatuingiza kama taifa. Natumia marufuku yake ya kusafirisha mchanga wenye madini nje ya nchi kama mfano.

Zaidi ya dhahabu, mgodi wa Bulyanhulu unazalisha pia madini ya fedha (silver), cobalt, copper na cadmium (ya mwisho kama sikosei!). Bulyanhulu ni mgodi pekee nchini wenye madini yote hayo na mchanga unaosafirishwa nje unatoka Bulyanhulu. Madini yote hayo, kwa mujibu wa Sheria ya Madini na Mikataba ya Uendelezaji Madini (MDAs) waliyopewa na Rais Ben Mkapa na kurudiwa na Jakaya Kikwete, ni mali ya wawekezaji.

Mgodi wa Bulyanhulu unafanya smelting ya dhahabu tu (takriban 70% ya processing yote). 30% iliyobaki inafanyikia Japan ambayo ina hiyo capacity ya smelting ya hayo madini mengine.

Ndio maana mchanga huo umekuwa unasafirishwa kwenda Japan tangu 2001. Sasa a smart president angewaelekeza wawekezaji wajenge kwanza hiyo capacity ya smelting ndani ya nchi kabla ya kupiga marufuku export ya mchanga. Kwa kuzingatia kwamba wawekezaji hawa wanalindwa kisheria na kimkataba, a smart president would've renegotiated the MDAs or changed the relevant law ili kufanya processing yote ifanyike internally.

Badala ya a smart president, tuna JPM anayeamini kwamba ametumwa na Mungu kuinyoosha nchi hii na neno lake ndio sheria. Matokeo yake, atagombana na wawekezaji na serikali zao na mabwana wakubwa wa kifedha duniani ambao ndio wamiliki halisi wa rasilmali zetu.

Watampeleka kwenye arbitral tribunals za kimataifa ambazo Mkapa na Kikwete walizikubali kuwa ndio mahakama za migogoro kati yetu na hao tuliowapa rasilmali zetu. Na tukipelekwa huko hatuponi kwa sababu tutakuwa tumevunja mikataba na sheria zinazolinda wawekezaji. More importantly, hatapata hicho anachokifikiria, i.e. internal capacity ya mineral processing yote kwa sababu we simply don't have that capacity currently.

Na, kwa taarifa ya wale wasiojua mambo haya, huo mchanga unaosafirishwa nje sio magwangala. Magwangala ni rock waste yanayotupwa pembeni ya migodi baada ya dhahabu kutolewa. Yana madini kiasi kidogo sana ambayo sio commercially viable kwa wawekezaji kuyavuna. Hayo ndio madini Magufuli 'aliyowagawia' wananchi jana. Ni makapi yanayoachwa nyuma baada ya karamu ya wawekezaji. Hiyo, kwa busara za John Pombe Magufuli, ndio stahili ya waTanzania waliomchagua.

Evo Morales wa Bolivia alikuwa na mikataba kama ya kwetu alipochaguliwa in December ya 2006. Cha kwanza alichofanya ni kuiondoa Bolivia kwenye MIGA Convention na kwenye bilateral investment treaties (BITs) zilizokuwa zinalazimisha international arbitration kwenye migogoro ya uwezekaji. Baada ya hapo ndio akabadilisha sheria na mikataba ya uwekezaji iliyoipa Bolivia sehemu kubwa ya umilikaji wa gesi na mafuta ya nchi yake. Of course, Morales is a Bolivarian na rafiki wa Castro, marehemu Hugo Chavez na wakushoto wengine. Magufuli is none of the above. He's a proto-fascist who believes in nothing but violent state power.

TUNDU LISSU
Mwanasheria mkuu
CHADEMA
 
Hata tukiwalipa, ila iwe fundisho, na sie tutakula sahani moja na bodi ya TMAA, watumishi wake na wale wa wizara ya nishati na madini, tutawachunguza utajiri wao, je wafanana na mishahara na posho zao?!
Kama hapana basi tutakwapua zote, na ku freeze hata account zao, ikiwezekena hata kesi ya kuhujumu uchumi pia, liwe na fundisho kwa wasoma mikataba na watumishi wengine walio kwenye sekta nyeti..
 
Vipi za samaki hakupiga mahesabu ya Mbali?
Walipewa watu rushwa then wakaenda kumdanganya Mh JK. Sasa kwa hili hata kama wakila rushwa Dkt Magufuli hadanganyiki, na ndiyo maana timu zote zina ulinzi 24hrs a day, na usalama wa taifa wapo kazini 24hrs kuhakikisha system zetu haziingiliwi.
 
GTs,
Nawashauri tusiwe waoga ktk kulinda rasimali zetu. Tulitishwa hata kipindi kile eti wauza madawa wana nguvu, ila mpaka sasa kila mmoja anajua kinachoendelea. Sasa hata kwa hawa mafia wezi wa ACACIA na kundi lao, hawana nguvu kabisa, maana ni wezi na wao wanajitambua, ingawa wanajikosha bado ni wezi.

Kwa tulioishi ulaya pamoja na wazungu tunajua jinsi walivyo wanafiki na wachoyo. Na kibaya zaidi wamekuwa wakituibia kupitia misaada, rasilimali zetu n.k., sasa ktk hili wataalamu wetu wamesema ukweli, na litasimama hivyo hivyo.

Tusimame tuungane, maana mafia hawa huwa na tabisa ya kuanzisha/kufadhili vikundi vya wapiganaji ili kuleta machafuko, ila najua kwa Tz hawawezi kwa sababu Taifa hili Mungu analipenda na Usalama wa taifa wetu wapo fiti ile mbaya.

Niwasihi tu wale wanafiki wanaopewa hela na mafia wasidhani kuwa wapo salama, utaifa kwanza utanzania kwanza!
Huu ni wizi wa pili hawa ACACIA walishawahi kutudangaya kwa faida wanaopata kwa mwaka kesi ikaenda mahakamani. Huu ndio wakati muafaka kwa Rais Magufuli kutumia ile mahakama ya kifisadi kuwashitaki wote walioiletea hasara nchi hii bila kujali walikuwa wanashika hadhi gani, haiwezekani leo hapa Tanzania masikini muuza nyanya analipa kodi halafu kampuni kubwa ya kimataifa inakwepa kodi.
 
ulitishwa hata kipindi kile eti wauza madawa wana nguvu, ila mpaka sasa kila mmoja anajua kinachoendelea. Sasa hata kwa hawa mafia wezi wa ACACIA na kundi lao, hawana nguvu kabisa, maana ni wezi na wao wanajitambua, ingawa wanajikosha bado ni wezi.

Kikwete ..mkapa na wenzake wametugharimu sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom