Acacia; Mafanikio ya vita ya kiuchumi

MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,826
5,451
MAONI YANGU KUHUSU RIPOTI YA MAJADILIANO YA MAKINIKIA.

Na Sir Taylor.

Habari,Kwanza napenda Kutoa Shukrani na Pongezi za dhati kwa Mh Magufuli kwa kusimamia hili jambo hadi leo limefika hapa,Mimi mwenyewe nikiri wazi ilifika hatua nikawa naona giza katika hili swala,lakini kwa sasa naona nini kulikuwa kinafanyika. ONGERA SANA Mh Rais.Pili niwapongeze WAZALENDO wetu wote waliohusika ktk kamati mbalimbali ukianzia kamati ya prof mruma,Osoro na mwisho hii ya kabudi. Wamefanya kazi nzito sana.ONGERA sana.Tatu ni watanzania wote ambao toka mwanzo wamekuwa wakiunga mkono juhudi zote hizi.Sio kazi rahisi kupambana kwa hoja za watu waliojiweka KUNDI LA KUPINGA NA KUPOTOSHA KILA KITU.Sio rahisi hata kidogo,lkn naamini walisimama kutetea kile wanachoamini KINAWEZEKANA. ONGERA sana.

Kama mtakumbuka hizi harakati tangu zimeanza mwezi March kumekuwa na sintofaham nyingi sana juu ya hili jambo.Walijitokeza waliopinga kwa nguvu zote hatua na njia zinazotumika kushughulikia hili jambo.Wapo waliosema TUTASHITAKIWA kwa sababu tumevunja mkataba na ilitakiwa tujitoe kwa MIGA,Wapo waliosema hatutapata chochote katika hili jambo. Sina haja ya kurudia MANENO yao kwa sababu hakuna mtanzania asiyejua jinsi ambavyo walikua wanatumia UHURU WAO KUPINGA NA KUPOTOSHA hili swala.

Kwa MTAZAMO wangu hili swala Magufuli kafanikiwa kwa kias kikubwa mno na kama mapungufu yapo basi sio ya kuzidi Kazi nzuri iliyofanyika. Hii ni vita tena kubwa sana,hii ni vita tofaut na kwenda kuharibu shamba la mbowe,tofaut na kupiga mnada mali za lugum na ni tofaut na kuvunja billicanas. Ni vita ambayo magufuli anapambana na Wenye kuendesha dunia,Vita hii sio ndogo na upiganaji wake AKILI zinatakiwa ziwe nyingi nguvu KIDOGO.Na katika hili AKILI nyingi naona zinatumika kuliko nguvu. Huwezi pambana na Hawa mabepar kwa kutumia nguvu nyingi ukashinda. Tuna mifano hai, ni jinsi Nyerere alipotumia nguvu nyingi mgodi wa almas huko mwadui.Kuna nchi kama siera leon,Congo DRC na Angola tunaona ni vita hii ambayo haijawaacha salama.Viongoz walioekana kucheza na maslai ya hawa MABEPARI.Ukiangalia hawa wote na nchi zingine zinazoingia kwenye machafuko ya wenyewe kwa wenyewe au matatizo ya kiuchumi pindi wanapopambana na hawa mabepar sio kwamba wanakuwa hawana HAKI ya kupambania MASLAI YAO. Tatizo wanatumia njia gani kupambana na hawa BABA wa ulimwengu.

Watu wanahoji kama ushahidi tunao kwanini tusiende mahakaman,kwanini tunakaa meza moja na wezi. Hawa wanawaza SAHIHI lkn upeo wa KUONA nje ya mawazo yao ni MDOGO SANA.Ni rahisi sana kusema tuwafukuze,tutaifishe na kufanya chochote kile lkn inatakiwa ujue HAWA NDO WANAOENDESHA DUNIA. Na hawa ndo waamuzi wapi amani iwepo au wapi isiwepo. Hawa ndo wanaoendesha IMF,WB na organisations zote ambazo sisi kama waafrika hatuna ubavu wa kuzicontrol kwa manufaa yetu.KUPAMBANA na hawa watu na mkabaki salama ni AKILI NYINGI ZINAHITAJIKA.

Kuna njia nyingi sana za kusolve matatizo hata katika jamii tunayoishi iko hivo. Huwezi kimbilia mahakaman kama bado unaona kuna loophole ya majadiliano na mkafika muafaka. Mahakaman ni njia ya mwisho sana na hii ni KAMA NOMA NAIWE NOMA naweza iita.Kilichofanyika ni AKILI nyingi sana.Tumekamata ushahid ambao ni makontena waliyodeclare nje ya kiwango kuanzia size ya makontena,uzito wa concentrates zilizomo kwenye container.Tuna nyaraka mbalimbali kuthibitisha madai yetu.

Akili kubwa zaidi iliyotumika ni kuandaa haraka sheria mpya ambazo zinaweza kutumika ktk majadiliano. Ingekuwa ni maajabu kuingia ktk meza ya majadiliano wakati hamna sheria zozote ambazo mngependa zitumike wakati wa makubaliano.Katika mazingira ya vita hii ili Tanzania ibaki salama win win situation ilikua haiepukiki na hapa ndo tunaona sheria zetu mpya zimetumika kufikia muafaka. Kwa jinsi hii vita walivyokuwa wanawaza baadhi ya watu hakika hii vita isingetuacha salama na Tanzania lazima ingefuata history ya Zimbabwe,Congo DRC nk.

Mtu anahoji kutoka 400 trillion hadi 600 billion. Kivipi,tumeshapigwa.Ngoja ninukuu CEO kasemaje "Barrick and the government of Tanzania have also agreed to form a working group that will focus on the resolution of outstanding tax claims against acacia.under proposal as the gesture of good faith,acacia would make a payment USD 300million to the government of Tanzania, with the payment terms to be settled by the working group"mwisho wa kunukuu. Sijaona sehem wamesema wamelipa deni. Kinachoendelea ni misconceptions tu kuwa tumelipwa billion 600.

Lakini ebu tuseme tumelipwa hizo pesa.Maswali ya kujiuliza katika makubaliano yote yaliyotajwa jana ambayo ni kupata hisa 16%,faida kugawana 50/50,makao yao na mambo ya kifedha,kujenga smelter hapa Tanzania,SERIKALI kuwa na wawakilishi katika body ya wakurugenzi,madini yote kama yalivyoripotiwa na prof mruma nje ya dhahabu na copper concentrate nayo walikua wanachukua sasa yatakuwa yetu na makubaliano mengine yote je hayana tija kwa mtanzania?Sio mafanikio?Kama acacia wangekuwa sahihi tungekuwa tumeburuzwa mahakaman mda mrefu sana.Wasingekubali kuingia hasara baada ya makontena yao kuendelea kushikiliwa,wasingekubali sheria mpya zifanye kazi. Naamn wao wameona kuna mapungufu na ndo maana hivi vitu vimefikia hapa.

Mafanikio haya ambayo kwa kiasi kikubwa yapo kisheria,maana yake faida yake ni ya vizaz na vizaz. Tayar msingi mzuri umewekwa. Tunaweza kuangalia hela ni ndogo kwa matumain tuliyojiwekea lkn kwa haya tuliyoyafikia ni mazur zaid na yana maslai kwa taifa. Hata hizo 600 billion. Je haziwez punguza tatizo la pembejeo vijijini?Je haziwez punguza tatizo la maji?je haziwez saidia huduma ya afya?Hivi magufuli angepata hasara gani kama angeacha kama lilivyo hili jambo?Magufli kafanikiwa kupambana hii vita na kutoka salama.Kwa nature na ukipitia history ya vita ka hivi,MAGUFULI NI SHUJAA.Wapo wanaopinduliwa,wapo wanaopandikizwa sumu,wapo ambao wanakuwa assassinated na kuna sehem vita inapandikizwa na mwisho mnauana na Wanakuja kumweka mtu mwenye kulinda maslai yao. TUYAANGALIE MAMBO KWA MAPANA ZAIDI.

MNYONGE MNYONGENI,HAKI YAKE MPENI.

Nimalize kwa nukuu mbili hapa chini.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full of confidence.

Charles Bukowski
na
We think too small, like the frog at the bottom of the well. He thinks the sky is only as big as the top of the well. If he surfaced, he would have an entirely different view.

Mao Zedong
 
Nimefuatilia nione wapi kuna malipo ya $190b, nimeishia kuona porojo zilezile za 50/50. Sijui kuweka hela hapa nchini.
 
Back
Top Bottom