Abdallah Bulembo: James Mbatia hana shukrani

Kwa kweli Mh. Mbatia ameonesha uwezo mkubwa katika kuchangia hoja na Rais hakufanya makosa na mwenyekiti wa wazazi uelewa wake mdogo na Ndiyo maana hata jumuia yake ameivuruga akidhani kuongea kwenye magazeti ndiyo kujenga jumuia
 
Jana m/kiti wa Jumuia ya wazazi Abdalla Bullembo alisema kuwa mhe James Mbatia hana shukrani kwasababu alikuwa na maisha magumu Mh. Rais akamteua kuwa mbunge na kupewa gari nzuri,anavaa suti nzuri lakini hana shukrani/heshima
kwa kitendo chake cha kujiunga na UKAWA na kupanda majukwaani kuiponda serikali ya CCM iliyompa ulaji.

Hivi huyu Bulembo ndie alikatazwa kugombea TFF kwa kutokuwa na Elimu? Kama ni kweli bali TFF walimtendea haki. Je hajui kwamba Mbatia aliteuliwa na Rais wala si Mwenyekiti wa CCM? Je Mbatia aliapa kumtumikia aliyemteua au kuilinda katiba ya nchi? Hivi Bulembo anaweza kuthibitisha kwamba Mbatia hakuwa anavaa suti kabla ya kuteuliwa Mbunge? Je, Mbatia hakuwa na gari kabla ya kuwa mbunge? Je kama hakuwa navyo vitu hivyo kama anavyodai Bulembo, Vitu hivyo viondoe utashi na utu wake kwa sababu tu kateuliwa ubunge?

Hivi reaction ya watu aliokuwa anawahutubia ilikuwa nini baada ya kusikia statement hizo za Bulembo? Nitashangaa zaidi kama walimshangilia badala ya kumzomea.
 
Kwa Rais Kikwete amelalamika? Kwa taarifa yako Rais anafurahi kuona kijana aliyempa kazi anaifanya kama inavyotakiwa. Hakumpapa Ubunge ili afanye kazi za CCM, alimpa Ubunge ili awatumikie wananchi. Huyo Bullembo ni msubiri makombo lazima akitetee chama chake ili siku moja kimbebe.
 
Rais ni tasisi,ni nafasi inayoweza kufanya kazi na mtu yeyote bila kujali Itikadi.
Kupewa ubunge kwa Mbatia sio zawadi kama Kihiyo Bulembo anavyofikiri,na kama ni zawadi amwambie Rais amvue.

Ajabu mbona hakupewa yeye Bulembo. Kauli kama hizi sijui kwa nini wanawaambia wananchi.
 
Huyu bulembo nı mbumbumbu tuu, yy alıtaka kwa vıle kateulıwa na raısı ndıo aunge mkono kıla ujınga unaoamulıwa na ccm? Taıfa nı zaıdı ya chama, zaıdı hata ya huyo alıemteua na tunatakıwa kuweka maslah y ataıfa kwanza, muache kupotosha, UKAWA wanaıtetea katıba ya tume ya raısı alıyoıunda na kupokea report yake na kutıa sıgn, wa kumshangaa nı raısı anaepınga matokeo alıyoyakubalı na kuyasıgn. Only ın tz
 
Jana m/kiti wa Jumuia ya wazazi Abdalla Bullembo alisema kuwa mhe James Mbatia hana shukrani kwasababu alikuwa na maisha magumu Mh. Rais akamteua kuwa mbunge na kupewa gari nzuri,anavaa suti nzuri lakini hana shukrani/heshima
kwa kitendo chake cha kujiunga na UKAWA na kupanda majukwaani kuiponda serikali ya CCM iliyompa ulaji.
Bw. Bulembo anahitaji kusaidiwa. Kauli zake nyingi zina utata na hafikitinkabla ya kuzitoa!
 
Jana m/kiti wa Jumuia ya wazazi Abdalla Bullembo alisema kuwa mhe James Mbatia hana shukrani kwasababu alikuwa na maisha magumu Mh. Rais akamteua kuwa mbunge na kupewa gari nzuri,anavaa suti nzuri lakini hana shukrani/heshima
kwa kitendo chake cha kujiunga na UKAWA na kupanda majukwaani kuiponda serikali ya CCM iliyompa ulaji.

Huyu Bulembo anafikiri kila mtu ananunulika kama yeye
 
Jana m/kiti wa Jumuia ya wazazi Abdalla Bullembo alisema kuwa mhe James Mbatia hana shukrani kwasababu alikuwa na maisha magumu Mh. Rais akamteua kuwa mbunge na kupewa gari nzuri,anavaa suti nzuri lakini hana shukrani/heshima
kwa kitendo chake cha kujiunga na UKAWA na kupanda majukwaani kuiponda serikali ya CCM iliyompa ulaji.

Kweli dunia hii imejaa wajinga.Kwa hiyo Bulembo anataka Mbatia auze uhuru wake kwa ajili ya tumbo kama yeye.Ndio sasa ajue kwamba kama yeye ni mchumia tumbo,sio wote.
 
Jana m/kiti wa Jumuia ya wazazi Abdalla Bullembo alisema kuwa mhe James Mbatia hana shukrani kwasababu alikuwa na maisha magumu Mh. Rais akamteua kuwa mbunge na kupewa gari nzuri,anavaa suti nzuri lakini hana shukrani/heshima
kwa kitendo chake cha kujiunga na UKAWA na kupanda majukwaani kuiponda serikali ya CCM iliyompa ulaji.

Tatizo la CCM ni kutumia nafasi walizonazo kujinufaisha binafsi na sio kuwatumikia Watanzania na ndo sababu kauli za ulaji haziwatoki midomoni mwao. Kwao kila fursa ni ulaji. Mbatia kaonyesha namna ambavyo Kiongozi anatakiwa kuwa. Hata kama nafasi fulani inakupa ulaji,bado unawajibika kutimiza wajibu wako kulingana na majukumu uliyopewa. Ni viongozi wachache sana ndani ya CCM kwa sasa wenye uwezo wa kutimiza wajibu wao bila unafiki ndani yake. Kauli ya Bullembo inathibitisha ukweli kwamba tusiwategemee CCM kutuletea maendeleo ya kweli kwa wakati muafaka. Wao wapo kwa ajili ya ulaji tu!!!!
 
mbatia amewatia funzo,

Kwaiy yeye bulembo alipewa cheo na kujiondoa akili?
 
Rais ni tasisi,ni nafasi inayoweza kufanya kazi na mtu yeyote bila kujali Itikadi.

Kupewa ubunge kwa Mbatia sio zawadi kama Kihiyo Bulembo anavyofikiri,na kama ni zawadi amwambie Rais amvue.

maana yeye amezawadiwa ujumbe wa bunge maalum la katiba,sasa anadhan ndo kila atunukiwaye hupewa
 
Huyu Bullembo ni hovyo,.anataka kuiaminisha Jamii kuwa raisi anateuwa watu ubunge ili kuwapunguzia ugumu wa maisha..

Katika hili sikuungi mkono
 
Back
Top Bottom