Abdallah Bulembo ataka rungu la CCM limshukie Luhaga Mpina kwa kwenda kinyume na maadili ya chama

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, amekiomba Chama hicho kumhoji na kumchukulia hatua za kinidhamu Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa kile alichokiita kwenda kinyume na maadili ya chama...
Bulembo ana jisahau tuu. Hivi ndani ya Ccm ni nani wa kumnyooshea kidole mwenzake?

Bulembo kaua shule za jumuia ya wazazi. Anatakiwa awepo Ukonga na sio uraiani.
 
Mpina hakujifunza kwa yaliyomkuta Jobo Mnazaleti na yule katibu mkuu ikulu aliyedumu kwa muda mfupi ever.

Anashika sharubu za Mama...hapo ndipo atajua wanawake wana sharubu ama hawana.
 
Unaweza kumhoji Mbunge kwa mambo aliyowasilisha mbungeni? Bunge ina kinga yake. Ilikuwaje system ilimruhusu kuwasilisha yale bungeni kama haikuwa interest ya Serikali ya Chama tawala? Bulembo Aache kuchanganya mambo...

Kimsingi hilo bunge linapaswa kuwa la wananchi, lakini ilivyo sio bunge la wananchi maana hawana uhalali wa umma, wako huko bungeni kwa maagizo ya aliyekuwa rais kwa kupitia kiburi chake cha madaraka. Hivyo huyo Bulembo anasema hivyo maana anajua Mpina hayuko bungeni kwa ridhaa ya wananchi.
 
As far as I know CCM; huyu tayari yupo kwenye mode ya killing himself softly ..

Kashaisha...ni suala.la.muda tu...wala hakuna haja ya CCM kutoa tamko.kufanya hivyo ni kumpa mileage za bure ambazo hanazo.
 
Kimsingi hilo bunge linapaswa kuwa la wananchi, lakini ilivyo sio bunge la wananchi maana hawana uhalali wa umma, wako huko bungeni kwa maagizo ya aliyekuwa rais kwa kupitia kiburi chake cha madaraka. Hivyo huyo Bulembo anasema hivyo maana anajua Mpina hayuko bungeni kwa ridhaa ya wananchi.
Iligimate house of assembly!
 
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, amekiomba Chama hicho kumhoji na kumchukulia hatua za kinidhamu Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa kile alichokiita kwenda kinyume na maadili ya chama...
Hebu tuondoe huu utamaduni wa kila mtu akitaka kutoa au kupinga kitu basi wanakurupuka mtu huko eti achukuliwe hatua kwani mkimsikiliza hoja zake na mkachukua mazuri yake na mabaya mkaacha kuna shida gani?

Hii nchi ya kila mtu hakuna mwenye haki ya kumzuia mwenzie kuongea anachoonaa kina faa. Muache uchawa wa kijinga jinga
 
Bulembo ana linda fadhila za binti yake yule kulamba ukuuu wa wilaya kutoka kwa mama, so sishangazwi na maneno ya kinafiki ya huyu mzee. All in all who is Makamba in this country mbona mnataka kuifanya tanzania ni nchi ya kikundi fulani na hakika 2025 tusimamisha mtu mwenye kariba ya Magufuli kuvunja hii miiko iliyojijenga miongoni mwa kikundi fulani…
 
Makamba anakosea mambo mengi tu.

Mfano swala la kuipa tenda kampuni ya uingereza kuishauri serikali kuhusiana na maswala ya gesi

Wakati tayari tuna taasisi yenye majukumu hayo PURA.

Huyu mtu anajiamulia tu mambo na kutumia fedha zetu vibaya na hakuna wa kumfanya lolote.

Nchi yao hii na Chama ni mali yao.
 
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, amekiomba Chama hicho kumhoji na kumchukulia hatua za kinidhamu Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa kile alichokiita kwenda kinyume na maadili ya chama.

Bulembo ambaye ni Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama hicho, ametoa ushauri huo katika mkutano wake na waandishi wa habari akijibu shutuma zilizotolewa na Mpina hivi majuzi baada ya Waziri wa Nishati January Makamba kuondoa tozo ya tsh. 100 kwenye lita ya mafuta.

Bw. Bulembo pia amesema hatua hiyo ya Mpina ni sawa na kumdhihaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa alikwishalizungumzia suala hilo kwa kulitolea ufafanuzi.

Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari, Mpina alisema kitendo hicho cha Waziri Makamba ni sawa na uhujumu uchumi, akivitaka vyombo vya uchunguzi vifanye kazi kwa madai kuwa ni kuwaumiza wananchi.
WEWE MBONA ULIUZA SHULE ZINAZOMILIKIWA NA CCM HUKUPIGWA RUNGU?
 
Back
Top Bottom