Abdallah Bulembo ataka rungu la CCM limshukie Luhaga Mpina kwa kwenda kinyume na maadili ya chama

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
426
585
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, amekiomba Chama hicho kumhoji na kumchukulia hatua za kinidhamu Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa kile alichokiita kwenda kinyume na maadili ya chama.

Bulembo ambaye ni Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama hicho, ametoa ushauri huo katika mkutano wake na waandishi wa habari akijibu shutuma zilizotolewa na Mpina hivi majuzi baada ya Waziri wa Nishati January Makamba kuondoa tozo ya tsh. 100 kwenye lita ya mafuta.

Bw. Bulembo pia amesema hatua hiyo ya Mpina ni sawa na kumdhihaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa alikwishalizungumzia suala hilo kwa kulitolea ufafanuzi.

Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari, Mpina alisema kitendo hicho cha Waziri Makamba ni sawa na uhujumu uchumi, akivitaka vyombo vya uchunguzi vifanye kazi kwa madai kuwa ni kuwaumiza wananchi.
 
Hivi rais wetu ana wasemaji wangapi hata Bulembo? Juzi tena nimesikia makamu mwenyekiti mpya akisema huyu Makamba haguswi atakayejaribu.

Sasa huyu makamu wa mwenyekiti anaingilia mpaka utendaji wa serikali hata Bunge hii nchi vipi haina watu? Kila mtu yupo kimyaa yaani wote ninyi mnafagilia kupewa vyeo vya kuteuliwa?
 
Unaweza kumhoji Mbunge kwa mambo aliyowasilisha mbungeni? Bunge ina kinga yake. Ilikuwaje system ilimruhusu kuwasilisha yale bungeni kama haikuwa interest ya Serikali ya Chama tawala? Bulembo Aache kuchanganya mambo. Mpina angeongelea yale masuala mtaani ilikuwa ruksa kuchukua hatua za kinidhamu jwa utaratibu wa chama.

Katema zile cheche bungeni, na lile bunge ni la wananchi wa Jamhuri wa nchi hii. Siyo Bunge la CCM. CCM muwe na subra

johnthebaptist tupe mwongozo juu ya suala kupitia Kwa Mzee Mgaya Hii chama Na Serikali yake inayoiingilia mhimili mwingine inawatumukua watanzania au wanaccm?

Kumbuka watanzania wote si wanaCCM lakini Bunge la Jamhuri ni lao.
 
Bulembo anapigilia msumari kwamba wabunge wa CCM hawana haki ya kuihoji serikali?.

Sasa sijajua wananchi tunawachagua wabunge wa CCM kwaajili ya nini.

Mzee Bulembo kwenye hili hapana, wabunge wawe na haki ya kuihoji na kuisimamia serikali bila woga.

Nikajua Bulembo atakuja na majibu ya hoja za mpina hasa ukiukwaji wa katiba na Sheria amekuja na hoja ya kuwanyamazisha wanaohoji.
 
Kumgusa makamba ni sawa na kugusa sharubu za SAMIA raisi hana mda wa kuwasikiliza hao anaona ndio watakaompigania kurudi madarakani 2025 haangalii kelele za wananchi anaona january anatosha hata wasemeje january hatolewi hapo! Hiyo ni ndoto ya mchana kweupe
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom