Abdallah Bulembo ataka rungu la CCM limshukie Luhaga Mpina kwa kwenda kinyume na maadili ya chama

Bulembo ni mtu anayeheshimika ndani ya ccm
Hujui chochote kuhusu ccm, Kaa kimya
Umeamua kujibu mwenyewe ahahahaaa, sasa ndg Bulembo unasema nikae kimya hebu kabla sijakaa kimya nikuulize.

Wakati ule unashinda pale nje kibarazani musoma mjini kwenye ile nyumba iliyokuwa karibu na majaruba ya mpunga, ulikuwa na idea yoyote ya siasa za ccm?.

Wakati huo kama wewe ni mwanaccm damu usikopi, nani alikuwa mshauri wa ccm kata ya nyasho hapo hapo alikuwa kwenye balaza la ushauri la wazee?.

Niishie hapo kabla sijakaa kimya.
 
Bulembo ana linda fadhila za binti yake yule kulamba ukuuu wa wilaya kutoka kwa mama, so sishangazwi na maneno ya kinafiki ya huyu mzee. All in all who is Makamba in this country mbona mnataka kuifanya tanzania ni nchi ya kikundi fulani na hakika 2025 tusimamisha mtu mwenye kariba ya Magufuli kuvunja hii miiko iliyojijenga miongoni mwa kikundi fulani…
Mpk Sasa cjaona Nani anaweza kuahvyo labda kalemani mbna sioni wa kuwa magu hata 50 % majaliwa nae kadhibitiwa hna namna
 
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, amekiomba Chama hicho kumhoji na kumchukulia hatua za kinidhamu Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa kile alichokiita kwenda kinyume na maadili ya chama.

Bulembo ambaye ni Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama hicho, ametoa ushauri huo katika mkutano wake na waandishi wa habari akijibu shutuma zilizotolewa na Mpina hivi majuzi baada ya Waziri wa Nishati January Makamba kuondoa tozo ya tsh. 100 kwenye lita ya mafuta.

Bw. Bulembo pia amesema hatua hiyo ya Mpina ni sawa na kumdhihaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa alikwishalizungumzia suala hilo kwa kulitolea ufafanuzi.

Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari, Mpina alisema kitendo hicho cha Waziri Makamba ni sawa na uhujumu uchumi, akivitaka vyombo vya uchunguzi vifanye kazi kwa madai kuwa ni kuwaumiza wananchi.
Bulembo atambue sisi wapiga kura ni zaidi ya CCM
 
Rais Samia keshatoa rukhsa kwa wabunge kuisimamia serikali kwa hoja akiwa ndani ya bunge.
 
Hivi rais wetu ana wasemaji wangapi hata Bulembo? Juzi tena nimesikia makamu mwenyekiti mpya akisema huyu Makamba haguswi atakayejaribu.... sasa huyu makamu wa mwenyekiti anaingilia mpaka utendaji wa serikali hata Bunge hii nchi vipi haina watu? Kila mtu yupo kimyaa yaani wote ninyi mnafagilia kupewa vyeo vya kuteuliwa?
Haya mambo yalianzishwa na awamu ya tano mmeona yalipotufikisha
 
mboga mboha hawapendi kuambiwa ukweli kabisa , kuna yule mzee wa aongezewe hata akikataa alazimishwe , yaani nawaangaliaga tu hawajamaa sasahivi wanavyojikausha utadhani kama sio wao, kuna watu hawana haya hata kidogo yani macho makavuuuu wanamsifia mama sasahivi, wakati walikua mijibwa koko kipindi cha shujaa
 
Hivi Burembo bado yupo na anataka kutafutiwa nafasi ahahahaaa.

Nadhani muda wake umekwisha hii ya kutoka shimoni na kujifanya kuwajibu wenzake ni kutafuta kula, kwani msemajinwa chama hayupo ?.
Kasema kipingi cha kampeni walilala mapolini mvua Yao jua lao
 
Unaweza kumhoji Mbunge kwa mambo aliyowasilisha mbungeni? Bunge ina kinga yake. Ilikuwaje system ilimruhusu kuwasilisha yale bungeni kama haikuwa interest ya Serikali ya Chama tawala? Bulembo Aache kuchanganya mambo. Mpina angeongelea yale masuala mtaani ilikuwa ruksa kuchukua hatua za kinidhamu jwa utaratibu wa chama
Katema zile cheche bungeni, na lile bunge ni la wananchi wa Jamhuri wa nchi hii. Siyo Bunge la CCM. CCM muwe na subra

johnthebaptist tupe mwongozo juu ya suala kupitia Kwa Mzee Mgaya Hii chama Na Serikali yake inayoiingilia mhimili mwingine inawatumukua watanzania au wanaccm?

Kumbuka watanzania wote si wanaCCM lakini Bunge la Jamhuri ni lao.
Haya mambo yalizaliwa awamu ya tano na huu ndio mwendelezo wake... Kuna wabunge wa ccm miaka Ile walishughulikiwa kusema mambo nje ya bunge ku attack serikali, mawaziri au raisi... Wakasema ni kuihujum serikali na raisi.... Wa nacho fanya Akina mpina Kuna watu walijatibu wakati ule na wakanyamazishwa.... Siasa bhana
 
As far as I know CCM; huyu tayari yupo kwenye mode ya killing himself softly ..

Kashaisha...ni suala.la.muda tu...wala hakuna haja ya CCM kutoa tamko.kufanya hivyo ni kumpa mileage za bure ambazo hanazo.
Labda akose akili tu, ila akiwa na akili hata kidogo tu basi atawasumbua n hawatakuwa na cha kumfanya zaidi ya kumpa ugali tu.

Kuna watu wengi tu waliwahi kuwa na guts za kuyafanya haya ya Mpina na walidumu miaka mingi tu kwenye siasa.
 
Kasema kipingi cha kampeni walilala mapolini mvua Yao jua lao
Kundi la watoto wa vigogo ambao wazazi wao walikuwa wanachama ila kutokana na uaminifu na uadilifu hawakupata umaarufu na wenzao wengi wanaitwa vijana wa Nyerere.

Wazazi wao walichelewa kwa kujifanya wazalendo leo watoto ndiyo wanashangaa wenzao wakiogelea na bata mtoni.

Huyo Burembo anayaelewa hayo, ashukuru Mungu kupitia siasa ikamtoa ila mpira hata Mara shooting Star walimkataa!.
 
Bulembo ana linda fadhila za binti yake yule kulamba ukuuu wa wilaya kutoka kwa mama, so sishangazwi na maneno ya kinafiki ya huyu mzee. All in all who is Makamba in this country mbona mnataka kuifanya tanzania ni nchi ya kikundi fulani na hakika 2025 tusimamisha mtu mwenye kariba ya Magufuli kuvunja hii miiko iliyojijenga miongoni mwa kikundi fulani…
Ni vile tu hawawezi kurusu usajili wa chama kipya cha siasa ambacho kitakuwa na masalia ya wale walioaminiwa kwenye system ya JPM, na sasa wameenguliwa.

Mambo yangekuwa ni moto sana kuelekea 2025.
 
Ni vile tu hawawezi kurusu usajili wa chama kipya cha siasa ambacho kitakuwa na masalia ya wale walioaminiwa kwenye system ya JPM, na sasa wameenguliwa.

Mambo yangekuwa ni moto sana kuelekea 2025.
Tuombe kheri InshAllah
 
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, amekiomba Chama hicho kumhoji na kumchukulia hatua za kinidhamu Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kwa kile alichokiita kwenda kinyume na maadili ya chama.

Bulembo ambaye ni Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama hicho, ametoa ushauri huo katika mkutano wake na waandishi wa habari akijibu shutuma zilizotolewa na Mpina hivi majuzi baada ya Waziri wa Nishati January Makamba kuondoa tozo ya tsh. 100 kwenye lita ya mafuta.

Bw. Bulembo pia amesema hatua hiyo ya Mpina ni sawa na kumdhihaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa alikwishalizungumzia suala hilo kwa kulitolea ufafanuzi.

Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari, Mpina alisema kitendo hicho cha Waziri Makamba ni sawa na uhujumu uchumi, akivitaka vyombo vya uchunguzi vifanye kazi kwa madai kuwa ni kuwaumiza wananchi.
Wanaccm hawaachiani maji ya kunywa mezani - Kikwete
 
Back
Top Bottom