katelero
JF-Expert Member
- May 31, 2010
- 529
- 84
...mimi maswali yangu manne iwapo mwanaume anastahiki ku 'provide for his wife'
1. kwa kiwango gani?...kwa kila kitu? au kwa yaliyo makuu i.e Nyumba, Chakula, Mavazi, na Matibabu.
2. kwa muda gani? mume akiwa mzima au ugonjwa, mume akiwa kijana au mzee
3. mwanamke abakie (full-time) mama wa nyumbani? ...kwakuwa pesa yake haihitajiki, ruksa alee watoto tu?
4. kipato chake (mke) kitafsiriwe vipi?
...nachelea tafsiri ya maamuzi haya 'compared' na mila, desturi na tamaduni za makabila/utaifa.
Kwetu 'Mwambao' yanawezekana sana haya. Mke anashinda ndani kulea watoto, kujifukiza udi nk...
'Unyamwezini' mume na mke wote wanapiga matuta!...Sijui kule kwa 'Wakurya' kukoje...!
Mbu unaweza kuombwa hela ya kodi ya nyumba au ada ya watoto wakati unaumwa umelazwa hospital, na pengine umekuwa mlemvu kabisa huwezi kufanya kazi tena kisa eti wewe lazima uprovide