johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,915
- 141,877
Ikumbukwe kuwa ni takribani 20% ya wananchi ndio walisema wanapendelea mfumo wa vyama vingi uanzishwe nchini na 80% waliukataa kwa madai kuwa kwa wakati ule taifa halikuhitaji na wala halina wapinzani wa "kweli".
Baba wa taifa akasema wachache wapewe na wengi wasikilizwe, ndipo ukaanzishwa huu Upinzani wa ruzuku.
Yaani wapinzani wanapiga hesabu za kujinufaisha wao na "matumbo tumbo" yao ndio maana hata sasa wamekuwa watu wa kuhamahama kufuata fursa.
Mchungaji Mtikila aliwahi kuhamia CHADEMA ili tu awe Mbunge wa Ludewa lakini wananchi wakamkataa akarudi kwenye DP yake.
Babu Duni Haji alihamia CHADEMA ili tu aweze kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.
Mifano ni mingi na hao ndio aina ya wapinzani tulionao ambao sasa wanaiomba CCM iwaletee Tume huru ya uchaguzi.
Niishie hapo.
Maendeleo hayana vyama!