80% ya Watanzania waliokataa mfumo wa vyama vingi walikuwa sahihi, kizazi cha Upinzani wa kweli bado hakijazaliwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,750
139,544
Ikumbukwe kuwa ni takribani 20% ya wananchi ndio walisema wanapendelea mfumo wa vyama vingi uanzishwe nchini na 80% waliukataa kwa madai kuwa kwa wakati ule taifa halikuhitaji na wala halina wapinzani wa "kweli".

Baba wa taifa akasema wachache wapewe na wengi wasikilizwe, ndipo ukaanzishwa huu Upinzani wa ruzuku.

Yaani wapinzani wanapiga hesabu za kujinufaisha wao na "matumbo tumbo" yao ndio maana hata sasa wamekuwa watu wa kuhamahama kufuata fursa.

Mchungaji Mtikila aliwahi kuhamia CHADEMA ili tu awe Mbunge wa Ludewa lakini wananchi wakamkataa akarudi kwenye DP yake.

Babu Duni Haji alihamia CHADEMA ili tu aweze kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Mifano ni mingi na hao ndio aina ya wapinzani tulionao ambao sasa wanaiomba CCM iwaletee Tume huru ya uchaguzi.

Niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama!
 
Akili huna. Asilimia zaidi ya 60% ya wananchi wote ni vijana chini ya miaka 40.
 
Mtoa hoja huna justification yoyote tangible kutetea hoja yako!!

Ni aibu miaka 5 mtu anazuia wapinzani kufanya siasa wakati Katiba na Sheria inatoa uhuru huo...
 
johnthebaptist,
You are too naive. Yaani concept zima ya vyama vingi hujui au huielewi. Ndiyo maana unatumia neno Wapinzani. Hivi Ukiwa nchi kama UK au US Wapinzani ni akina nani!?

Kilichopigiwa kura then ilikuwa ni mfumo wa chama kimoja au vingi siyo kama unavyofiri wewe kuwa chama tawala na Wapinzani. Usimsingizie Nyerere bure!
 
Sio kwamba wangeliruhusiwa kipindi hiki tungeliyaona yaliyojitokeza huko Libya? Walikuwa sahihi kwa kuwa busara yao ndiyo imeufanya mfumo huu wa vyama vingi kuzoeleka na kusahihisha baadhi ya mambo ambayo pengine yangelileta athari kwa Taifa.
 
Mambo yote yaliyoanzishwa kwa dhulma huishi kwa dhulma milele.

Vyama vingi nchi hii ni miongoni mwa matokeo ya dhulma.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom