666-nyayo za kuzimü

666-nyayo za kuzimü

666-NYAYO ZA KUZIMU--19-

Mama weee!!!..mama Tito kanyongwa jamaaanii!!! Mungu eeee!! Tunakwisha uuuwii!!! Ndivyo alivyosikika mama Kurwa alietoka kwenye nyumba ya mama Tito kwa lengo la kumpa pole kwa kifo cha mumewe,huku akikimbia mikono kichwani mithili ya mtu aliechanganyikiwa machozi na uoga ilionekana kuitawala sura yake!! Hakuna alieamini hizo habari mpaka walipoenda kushuhudia na kukuta jambo lile ni kweli limejiri!! Macho yao yalishudia Mama Tito akiwa kaning'inizwa na kamba nyekundu

kama ile iliyomnyonga mumewe muda si mrefu,ulimi ulikua nje na damu ilionekana kutoka puani na masikioni!!!!

Mchanganyiko wa hasira na uoga ulitawala mioyoni mwa wanakijiji,kifo kwa mara ya pili mfululizo!! Hata masaa hayajapita,tena mume na mke!!!..ni nani anaeyafanya haya?? Jamani hii si bure...ni laana inatuua!!!...ni nani aliewaleta wale watu lakini?? Ni

baba Madhifa!!...haraka wanakijiji wasiopungua idadi ya watu thelathini,wake kwa waume,watu wazima kwa watoto kwa jazba kubwa walianza kuelekea kwa baba Madhifa!!...chuki iliyokuwepo kati ya jamii ya wakulima na wavuvi juu ya wawindaji ilizidi kushamiri kwa kiasi kikubwa,baba Madhifa sasa ndie alieokana kama chanzo,kitendo chake cha kuwaokoa wakina mzee Otongo ilikua ni hukumu tosha!

Mawe na dhana zingine kama mapanga mikononi mwa wanakijiji zilikua ni kipimo tosha cha kuonyesha kinachoenda kujiri,hakukua na amani tena!!

Masikini baba Madhifa,hakua na hili wala lile,kuzaliwa kwake kwenye jamii ndogo ya wawindaji ndio kosa lake kubwa,hakuna wa kuwatetea mbele ya wanakijiji wengine,hakuna wa kuwasikiliza!!

Walipowasili kwenye uwanja wa nyumba yake haraka shughuli za ubomoaji na uharibifu zilianza!! Mawe yalirushwa kama risasi kwenye nyumba ile ya udongo bila hata kuangalia na kuuliza kama mna watu ndani,sauti za kejeli matusi na kebehi zilisindikiza

bara-bara shughuli hiyo na hatimaye waliamua waichome kabisa waridhishe roho zao zilizokua za kinyama baada ya kushuhudia mauaji ya wenzao wawili,je hilo ni suluhisho?? Hawakufikiria hicho!!

Baba Madhifa na wanae hawakuwepo,walirudi msituni kuendelea na shughuli zao na hata Mama Madhifa vilevile alikua kisimani akichota maji,Mungu alikua upande wao kwani kama wangelikuwepo ni dhahiri wangelikua mishikaki!!
Lile zoezi halikuishia pale tu kwa baba Madhifa,liliendelezwa kwenye nyumba zingine zote za jamii ya wavuvi zilizokuwepo karibu na kuwafanya wabakie mithili ya vifaranga waliokimbiwa na mama,hawakuweza kufanya kitu,hawakua na uwezo huo,ila waliumia sana rohoni! Kwanini wao?? Au ni kwasababu wao hawahesabiki ndani ya kile kijiji?? Walikua kama yatima,walishindwa kuyazuia machozi.

Sasa wamebaki wakina mzee Otongo,je kipi kitawakuta?? Wale wanakiji baada ya kuridhika na walichokifanya hawakutaka kupoteza muda,miili ya Baba Tito na mkewe ilizikwa na kuhitimisha zoezi la kumuacha Tito yatima kamili,majonzi na simanzi zilitawala lile eneo bila kusahau na hisia za uoga,

Julina na Mama Halima ni miongoni mwa watu waliokuwepo eneo la tukio japokua hawakuhusika kurusha hata jiwe moja kwenye nyumba ya baba Madhifa,chozi lilitiririka kwenye kila jicho la mmojawao ila hasa mama Halima,moyo wake ulikua umebeba siri

nzito juu ya vile vifo,siri ambayo hakuna hata mmojawao anayoijua isipokua yeye,ni yeye pekee aliekua anafahamu ya kwamba mama Tito hakuuwawa bali alijiua kwani alimshuhudia mama Tito kwa macho yake akiichukua ile kamba iliyomnyonga mumewe kule shambani na ndio hiyo aliyoitumia kujimalizia na yeye pia,aliogopa kusema!! Na chozi lilizidi kumshuka haswa!!!

* * * * *
Mama Madhifa baada ya kuweka ndoo yake ya maji kichwani taratibu alianza kujivuta kuelekea nyumbani kwake,macho yake aliyoyatupia mbele ya safari yalimruhusu aone moshi mzito ukitokea kijijini,alipata mashaka,maswali yalikuja kichwani juu ya nini hasa kinachojiri huko kijijini,masikini hakufahamu ya kwamba nyumba yake na za wenzake ndo zinateketea.

Aliongeza kasi kidogo inayoendana na umri wake wa miaka hamsini na tatu ili aweze kuwahi ila ghafla alikabwa na mtu tokea nyuma!!! Puuh ndoo ilidondoka na maji yakamwagika!!! Aliangaika kutetea uhai wake lakini hakufanikiwa!!..mara haraka akavishwa kitanzi chekundu tayari kwa KUNYONGWA!!! Ni nani huyu mnyongaji?

* * * * * * * *
USIKOSE SEHEMU 20 IJAYO.
 
666-NYAYO ZA KUZIMU--20-

Alikabwa kwa nguvu mno akashindwa kupumua kabisa,macho na ulimi vilitoka nje!! Aliburuzwa kama zigo la maganda ya viazi na ile kamba shingoni mpaka ulipo mti mmoja mkubwa wa mkaratusi,akaning'inizwa mithili ya nyama buchani,maisha yake yakakomea hapo,kikatili mno aliuwawa,hakupata hata fursa ya kujua yaliyotokea kule kijijini,hakupata hata fursa ya kumuona mumewe tokea muda wa asubuhi,hata mwanae wa mwisho ampendae,Madhifa.

Hakuna alieshuhudia chochote,hakuna jicho lililoona lolote hivyo bado ilikua ni siri juu ya nani anaeua na kwanini anaua vilevile,kwanini anatumia kamba nyekundu?? Pia lilikua ni swali ambalo bado wanakijiji walikua hawajalipa nafasi vichwani mwao,hali ilizidi kuwa tete na ya kuogofya...ndani ya masaa yasiozidi matano tayari watu watatu walikua washaenda na maji kwa kifo kinachofanana!!


Baba Madhifa na wanae wawili walikua washawasili kijijini,hali ya kuona moshi mzito toka kijijini iliwafanya waache shughuli zao za uwindaji na kwenda kujua kinachojiri,walipofika kijijini hawakuona watu kama inavyokuwaga ni dhahiri walikua wameenda sehemu fulani ambayo wao hawakuifahamu,haraka walielekea ilipo nyumba yao,hawakuamini macho yao,hawakuamini

walichokiona,nyumba yao ilikua tayari gofu na nyumba zingine za wenzao nazo ndio zilikua zinamalizikia kwa moto,haraka waliwafuata wenzao waliokua wamejikusanya kihuzuni hatua kama kumi toka walipo kwa dhumuni la kuuliza ili kujua hasa kilichotokea,kiunyonge waliwajibu ya kwamba wanakijiji ndio wamefanya hayo,baba Madhifa alipata hofu kubwa moyoni!! Mke

wangu yu kwapi?? Aliuliza haraka kwa taharuki akajibiwa ya kwamba alienda kisimani,bila ya kuchelewa aliwaagiza wanae wawili ambao walikua ni wa kiume;Madhifa na Khadhifa kwenda kumjulia hali mamayo huko kisimani,haraka walikimbia

kuelekea huko! Masikini hawakujua ya kwamba mama yao tayari alishaning'inizwa ni ndege tu wa mizoga ndio wanaofaidi,walikimbia kwa kasi na nguvu zao zote huku mioyoni mwao wakiwa wanasali mama yao awe salama,Madhifa alishindwa kuzuia machozi na hofu kubwa ilishika wake moyo,alimpenda sana mama yake.


Baada ya mwendo wa robo saa walikuta ndoo chini waliyoitambua ya kwamba ni ya kwao lakini hawakumuona mama yao!! Ilibidi waanze kufuatilia alama zilizoashiria ya kwamba mtu aliburuzwa toka eneo lile zilizowapeleka mpaka karibu na eneo ambapo mama yao alinyongwa,ndege wa mizoga walisaidia kuhitimisha zoezi.


"Khadhifa!!!..yule anaening'inia pale mtini ni nani???...sio mama yule!!!"

sauti iliyotepeta uoga ya Madhifa iliuliza,
"He!! Mbona kama ni yeye!!!!"

alijibu Khadhifa,haraka walisogea na kugundua ya kwamba walichobashiri ni kweli,alikua ni mama yao! Damu zilitawala dela lake kwa kiasi kikubwa kutokana na kunyofolewanyofolewa na ndege wa mizoga,macho yake yaliokua nje yalikua yashanyofolewa na hata ulimi pia,sura yake ilikua ngumu kutambulika!!!


Haraka Khadhifa ambae ndie mkubwa alifukuza wale ndege na kupanda juu ya mti kwa ujasiri na kufungua ile kamba kuruhusu mwili wa mamaye kushushwa chini,walimshusha na kumbeba kisha safari ya kuelekea walipotoka ambapo baba yao anawasubiri ilianza,hawakua na mama wala nyumba tena,uchungu usioelezeka ulitawala mioyo yao,moja kwa moja walifahamu

ya kwamba waliochoma nyumba yao ndio wanaohusika na kile kifo,yani wanakijiji!!

Chuki kubwa ilipandikizwa mioyoni,roho ya kisasi ilikamata hasa vichwa vyao,hawakutaka kukubali lile jambo liende vile vile tu,hawakukubali roho ya mama yao iende peke yake yani bure kabisa kwa ule unyama aliofanyiwa,hisia za kuwa wawindaji wa watu badala ya wanyama zilizuka!!


Baada ya muda kidogo waliwasili kwenye uwanja wa nyumbani kwao sura zao zikiakisi vya kutosha mioyo yao ilivyo na uchungu,walihisi kama wamekabwa rohoni tena hisia hizo zilizidi hasa baada ya kumuona baba yao,walishindwa kupata jibu juu ya nini watamueleza kwani walimuonea huruma,lakini ghafla walianza kulia kama watoto,kilio ambacho walijitahidi kukizuia tokea muda mrefu,kilio ambacho kilimfanya baba yao ashtuke,kilio kilichofanya baba yao aanguke kwa presha kama kiroba!!

* * * * * * *
upande wa pili wanakijiji waliokua kwenye mazishi ya baba na mama Tito walimaliza shughuli zao,walijiondoa toka kwenye lile eneo la makaburi huku bado habari za uoga juu ya ile hali zikitapakaa,bado hofu iliwashika na walishasahau kabisa dhambi waliyotoka kuitenda ya kuchoma nyumba za watu wanaowahisi wao ni chanzo,walikua kimakundi makundi lakini ghafla mama Halima alimvuta pembeni Julina na kumwambia kwa kumnong'oneza kiumbea..

"mama Tito hakuuwawa!!"

"unasema??"
"ndio hivyo kama ulivyonisikia..!"
"we umejuaje??"
"nilimshuhudia kwa macho yangu akiichukua ile kamba iliyomnyonga mumewe,na ndio hiyo kajinyongea!"
"weeeh!!"
"we si ulizimia,ungeyaonea wapi?? Ila!!..uufunge huo mdomo wako,tena uufunge hasa!"
"ntaweza kweli??"
alidakia Julina.
* * * * *

USIKOSE SEHEMU 21 IJAYO.
 
666-NYAYO ZA KUZIMU--21-

"kwanini usiweze??...ushaanza!!"
kwa ukali kidogo mama Halima alitamka,
"sawa mama nitajitahidi kadri ya uwezo wangu"

Julina alimtia moyo,waliendelea na safari yao ya kuelekea majumbani taratibu huku wakiwa washaachwa nyuma na wenzao,stori ndogo ndogo zilitawala maongezi yao hasa juu ya tendo lile la uchomaji moto wa nyumba zakina Madhifa kitu walichoonekana kupinga kupinga kabisa japokua walikua hawana uwezo wa kuongea mbele ya umati wa wanakijiji,wangeonekana wasaliti.taratibu walitembea bila hofu walishasahau

kidogo mambo ya vifo kutokana na kupumbazwa na vijistori vidogo vidogo vya hapa na pale,ila ghafla Julina alisimama kisha akasema..
"mama Halima,nina hofu"
"nini tena Julina mwanangu? Mwanao si yupo kwa mzee Patili.."
alisema mama Halima huku akirudi nyuma kumfuata,
"sio juu ya mtoto wangu Mama,ni juu ya mume wangu Kitanzi!...ni muda sasa hajarudi,sijui nae atakua ashanyongwa??"

"mh-mh,usiseme hivyo bwana kwanza embu twende nyumbani ukapumzike mana tokea usiku ulipojifungua upo kwenye heka heka tu hata mtoto wako atakua anakuhitaji mno kwa sasa,tafadhali twende!"
kidiplomasia mama Halima alipooza jambo lililotaka kuzuka,alimshika mkono Julina na kumvuta waende.

Nyuma ya mama Halima na Julina alionekana mtu anakuja kwa kasi! Pande la mtu,pande la mbaba! Mweusi tii kwa rangi na kichwani alikua hana nywele kabisa,yani upara!!

Mikono yake miwili mikubwa iliyoshiba ilikua imeshikilia kamba nyekundu,macho yake makubwa mekundu yalisadifu hamu kubwa iliyo moyoni mwake,masikio yake yalizoea makelele ya kuomba msamaha ya watu mbalimbali na hata pia mikono yake ilizoea kunyofoa roho za watu,alikua ni mnyongaji!!!

Ghafla mama Halima alihisi kitu akageuka nyuma haraka,hakuona kitu!! Wasiwasi ulimteka moyo,akamwambia Julina
"nahisi kuna kitu!"
huku akigeuka geuka nyuma,
"nini tena hiko??"
Julina mama uoga haraka aliuliza,
"bado sijafahamu! Ila tuongeze mwendo Julina,twende!!"

haraka mbio zikaanza,maumivu bado yalikua na Julina kwani si muda mrefu toka atoke kujifungua lakini uoga wake ulimsaidia mno kumkimbiza,tayari moyo wake ulishawasha jenereta,ulikua mbio mno kuliko hata wa yule aliehisi kitu,yani mama Halima!! Joto lilipanda mwilini mwake,kajasho kauoga kalimteremka! Mungu wangu nisaidie!! Alijiambia moyoni.

Baada ya muda kidogo waliwafikia wenzao wakaungana nao,walishusha pumzi ndefu ya kutoamini kama wamefanikiwa huku mioyo yao ikianza kutulia taratibu,walijuta kwanini walibaki.
Lile jitu lilitokomea,halikuonekana tena,halikujulikana lilielekea wapi!! Lilichokipanga hakikufanikiwa,wakina

mama Halima waliponea chupuchupu watiwe kitanzini kama isingelikua hisia zao zilizowastua,hivyo nani anafuata?? Hiko kilikua ni kitendawili.
Upande wa pili wa shilingi nyumbani kwa mzee Patili maongezi madogo madogo yalichukua nafasi,fahamu

zilishamrudia mama Kadogo japokua majeraha bado mwilini yalimsumbua na pia vilevile kichwa kilikua kinamuuma,dawa alizopewa na yule mzee sio siri zilimsaidia vilevile mzee Otongo.

Maongezi yao yaliokua yanaendelea yalishindwa kufikia hitimisho kwani kila walipojadili kuhusu vilivyotokea huko nyuma bado hawakupata jibu kwamba vimeishia wapi,ni ngumu kuamini kama lile jeshi limewaacha tu

vilevile,walipata kidogo mashaka,walikua hawafahamu ya kuwa kuna mauaji yanaendelea kijijini,walikua hawajui kabisa juu ya hilo,walikua hawafahamu ya kwamba sasa jeshi la 666 limekuja kivingine!!
Muda ulianza kuruhusu jua lizame,taratibu giza likaanza kuingia,wanakijiji kutokea kwenye mazishi walianza

kuitia miguu yao ndani ya kijiji,mila zao na desturi haziruhusu kulaza maiti,hivyo mtu akifariki mapema tu anazikwa akapumzike kwa amani,kila mwanakijiji alielekea kwenye nyumba yake,tito aliekua yatima yeye alichukuliwa na mama Kurwa,mmama mmoja muongeaji sana mwembamba ambaye ni jirani yao,mama

Halima na Julina moja kwa moja walielekea kwenye nyumba ya mzee Patili,kumpasha habari na kumchukua mtoto waliemuacha hapo kwa muda.Habari zile ziliwashtua sana! Mauaji ya watu wawili ndani ya kijiji kwa kunyongwa kilionekana kuamsha hisia ya kwamba ujio wa jeshi la 666 umewadia!
Mama Kadogo na mzee Otongo pia walihisi vivyo hivyo!

Upande wa pili mzee patili na wakina mama Kadogo walijisikia vibaya juu ya taarifa ya kuchomwa kwa nyumba za wakina baba Madhifa na walijiona wakosefu mbele zao.

Ngo! Ngo! Ngo! Hodi iliita,mzee patili aliinuka na kwenda kufungua,alikua ni Khadhifa! Alikuja kumuita mzee patili akawasaidie kwani baba yao yupo kwenye hali mbaya!! Mzee Patili alishangazwa na zile habari na hasa alishangazwa zaidi baada ya kuambiwa hicho kitu kilijiri baada ya kuleta mwili wa mama yao waliokuta umenyongwa maeneo ya kisimani,haraka mzee Patili alichukua madawa fulani kisha mbio zikaanza kuelekea eneo la tukio!

Kutokana na kaumbali kalichopo walichelewa,walipokaribia walisikia sauti ya kilio waliyoitambua ni ya Madhifa! Hofu zikajazwa mioyoni mwao! Nini tena hiki jamani?? Walijiuliza huku wakiongeza kasi!!


USIKOSE SEHEMU 22 IJAYO!
 
666-NYAYO ZA KUZIMU-22-


kutokana na kaumbali kalichopo walichelewa,walipokaribia walisikia sauti ya kilio waliyoitambua ni ya Madhifa! Hofu zikajazwa mioyoni mwao! Nini tena hiki jamani? Walijiuliza huku wakiongeza kasi! Haraka waliingia ndani,mzee Patili bila kuchelewa alichukua madawa yake aliyoyabeba na kuanza shughuli ya kumpakaa dawa baba Madhifa alielazwa chini na kidogo alimmezesha kwa kumfungua kinywa,ilikua ni dawa ya kumrudisha kwenye fahamu,aliwaambia hivyo wakina Madhifa waliokua na hofu kubwa ya kumpoteza baba yao kama walivyompoteza mama yao,uzoefu wa mzee Patili kwenye yale matukio ulifanya jambo lisiwe gumu kihivyo,baada ya kupaka ile dawa aliwahitaji watulie ifanye kazi na baada ya muda kidogo itaonyesha matunda,aliutumia huo muda kwena kuangalia maiti ya mama Madhifa iliyokua imefunikwa gubigubi,ilimtetemesha mno na kumuogopesha,maiti ilikua haitamaniki na yenye kutisha kutokana na majeraha makubwa iliyonayo,shingoni kulikua na alama ya kamba iliyoashiria ya kwamba ilimkaba vilivyo,aliifunika kisha akayarushia macho yake kwa wakina Madhifa,hawakua na amani hata kidogo,roho ya chuki na kisasi ilichipukia mioyoni mwao,hofu ya kumpoteza baba yao na uchungu wa kumpoteza mama yao uliwafanya machozi yatiririke yakisindikizwa na kwikwi za kilio,aliwaonea huruma sana na kichwani akajiuliza leo hawa watoto watalala wapi?? Akatikisa kichwa kwa masikitiko kisha akaangalia anga lililokua kiza kuashiria giza lishaingia.
Baada ya muda usiopungua robo saa baba Madhifa alianza kupiga chafya! Alirudi duniani!! Wakina Madhifa hawakuamini lile tukio,ilikua ni kama miujiza mbele ya macho yao!! Haraka walimkimbilia baba yao kwa kutaka kumjulia hali,tabasamu zilizoambatana na machozi zilionekana kwenye nyuso zao,walimkumbatia baba yao kwa nguvu huku wakilia! Walitia huzuni,mzee Patili nae chozi lilimshuka taratibu,lile jambo lilimgusa wake moyo.
Hakukua na muda tena wa kupoteza,walifahamu hakuna msaada wowote wangeupata toka kwa wanakijiji na ukizingatia hawakuhuitaji hata kidogo,waliungana na wanakijiji wenzao na mzee Patili wakauzika mwili wa mama yao,hisia za kwamba alinyöngwa na wanakijiji zilifutwa baada ya mzee Patili kuwapa tahariri ya kua yale mauaji hayahusiki na mwanakijiji yoyote bali ni kwamba yanafanywa na jeshi la 666 lililowadhuru wale watu waliowaokoa japokua kwa kiasi kimoja yameleta mkanganyiko,hisia za uoga ziliwatetemesha na ukizingatia kwa ule usiku iliwabidi walale nje baada ya nyumba zao kuchomwa.
* * * *
pembeni ya nyumba ya mama Kurwa upande wa kushoto kulikua kuna mti mkubwa wa muembe ambao ukitoka huo nyumba ya mzee Yosso ndio ilikua inafuata,hali ya giza iliyokuwepo ilifanya mti ule kutoonekana vizuri na kutisha kidogo,pembeni yake alikua ameegemea mwanaume mmoja alieshikilia kamba mkononi akipiga mahesabu kichwani,ni lile jibaba pande la mtu lililowakosakosa wakina mama Halima,ni yule mnyongaji!!! Mungu wangu! Sasa lilikua ndani ya kijiji tena karibu na nyumba ya mama Kurwa na mzee Yosso au baba Matata,lilikua linafanya nini pale?? Hilo halikufahamika ila taratibu lilianza kujongea na kuusogelea mlango wa mzee Yosso au baba Matata,lilipokaribia liligonga mlango....ngo! Ngo! Ngo! Hodiiii! Kwa sauti ambayo haikuendana hata kidogo na mwili wake! Ilikua ni sauti ya kike tena ya mama Kurwa ambaye ni jirani!!... Karibuu! Alijibiwa tokea ndani,kwa kua halikua na lengo la kuingia ndani lilibakia pale nje likisubiri mlango ufunguliwe,mama Matata aliekua na mumewe ilihali na mwanae wakila ilimbidi ainuke taratibu na kuelekea mlangoni kumfungulia aliegonga,ni kosa kubwa alilitenda hakujua kama alipeleka nafsi yake kifoni!! Alipokwa kama pochi! Lile jibaba leusi kama giza lililokuwepo lilimbeba mama Matata na kuanza kupotelea nae maporini!! Makelele ya mama matata ya kuomba msaada yalisikika vizuri kutokana na utulivu wa mawimbi usiku hivyo kupelekea wanakijiji kushtushwa kwa kiasi kikubwa bila kusahau mumewe ambaye ndie aliekuwa wa kwanza kutoka nje kwa hamaki! Hakumuona mkewe! Alianza kukimbia kufuatilia sauti aisikiayo huku akiita jina la mkewe kwa nguvu! Ile sauti haikuskika tena! Ilitokomea na lile jibaba,ilitokomea porini!! Baba Matata hakuona kitu,mkewe akawa tayari ashakwenda!!
Alieka mikono kichwani huku akilia kama mtoto,hakua na la kufanya aligeuza na kuanza kurudi kijijini kichwani mawazo yakimsonga na moyoni hofu ikimtinga!! Akili yake yote ikawa sasa ni kwa mama Kurwa kwani sauti ya yule aliekua anagonga ilikua ni yake,alikimbia,alipofika kijijini alikuta watu wameshajazana,sauti ya mama Matata iliwatoa majumbani mwao hasa ukizingatia hofu zao zilishawashwa tokea mapema siku ile,minong'ono ilitawala,baada ya kumuona baba Matata,walimfuata na kumuuliza kilichojiri,hakujibu kitu,alimfuata mama Kurwa huku akitoa macho,akauliza kwa ukali!
"mke wangu yuko wapi???"
huku akimnyooshea kidole! Mama kurwa alibanwa na kigugumizi,hakua na la kujibu! Ghafla mmama mmoja akaropoka..
"jamani kuna mtu pale kwenye mti ananing'iniaa!!!"
je ni nani huyo?


USIKOSE SEHEMU YA 23 IJAYOO....

 
666-NYAYO ZA KUZIMU-23-

alimnyookea moja kwa moja mama kurwa huku akitoa macho,kwa ukali akauliza!
"mke wangu yuko wapi??"
mama Kurwa alikosa cha kujibu,kigugumizi kilimbana,ghafla mmama mmoja aliropoka!
"jamani kuna mtu ananing'inia pale mti!!!"
Baba Matata aliachana na mama Kurwa na kukimbilia kwenye huo mti kushuhudia alichosikia,hakuamini macho yake kwa alichokiona! Alikua ni mke
we!! Alivishwa joho jekundu kitanzi kikimning'iniza! Damu zikiwa zinamtoka puani na masikioni! Aliishiwa nguvu za miguu akakaa chini na kuanza kulia!! Matata nae aliposhuhudia mwili wa mamaye unaning'inia katika ile hali kilio kilizidi kuchukua nafasi!! Baba na mwana wakawa wanalia kilio kilichoshindwa kutofautisha mkubwa na mdogo.Mwili wa mama Matata ulishushwa na kitanzi kikafunguliwa,wanakijiji walitawaliwa na hofu mara mbili ya ile iliyokuwepo mwanzoni,kushuhudia watu kunyongwa kwa siku mara tatu kama dozi haikua kitu cha kawaida,haikua kitu cha mzaha kabisa,ni kitu cha kuogopesha mno!! Kila mwanakijiji aliruhusu chozi la hofu na uchungu litoke huku wakiwa wanajiuliza mioyoni kwamba ni nani anaefuata sasa baada ya wale,miili ilikua inatetemeka na msamiati 'hamu ya kulala' haikua kabisa kwenye kitabu chao cha ile siku,nani alale kwa ile hali?? Hata mtu kukaa peke yake ilikua ni mtihani!!!
Wakati baba Matata na mwanae wakiendeleza kilio baadhi ya wanaume waliokuwepo pale walijivuta pembeni na kuanza kuteta jambo,
"sasa jamani ndio hivyo kama tunavyoona,tunazidi kutokomea! Sasa tunafanyaje sisi kama wanaume??"
alieleza mzee Rama,baba wa watoto saba akaae nyuma ya nyumba ya mama Kurwa,alikua ni kiongozi mkubwa wa kuwashawishi wanakijiji wakachome nyumba za wakina Madhifa,
"mh kusema ukweli hata mie naogopa hapa nilipo,ujue hiki kinatisha!"
"ah-ah! Kila mtu anafahamu kuhusiana na hilo,sisi kama wanaume tumejivuta pembeni ili tuangalie ni jinsi gani tutakavyolikabili,hatuwezi tukakaa tu hivi,tutakwisha!"
Mzee Rama alimdadavulia Tambwe alieonekana kutia mushkeli,
"kusema ukweli hili jambo si la mchezo hata nukta,mimi nadhani ya kwamba si binadamu wa kawaida anaefanya haya!...Nilisikia kwa masikio yangu sauti ya mama Matata ikielekea msituni lakini cha kushangaza tumemkuta kaning'inizwa kwenye ule mti!!"
mwalimu Baraka alichangia huku akiunyooshea kidole ule muembe,
"hata mie nahisi hivyo,hiki kitu kitatuwia vigumu sana,kumdhibiti mtu asiye wa kawaida yataka moyo ukizingatia hatujui hata yupoje!"
mzee Rama alisema,Lutiko aliekua kimya nae akachangia baada ya mzee Rama
"mi nadhani mtu mkubwa ataetusaidia ni mzee Patili,yeye ana ujuzi na haya mambo!"
"ni kweli! Hilo wazo zuri,nadhani mnaelewa ya kwamba nyumba ya mzee Patili ipo mbali na za kwetu na hata yaliyojiri hapa bado hayafahamu,sasa inabidi tumjuze!"
wazo hilo lilionekana kuungwa mkono na wale waume,kazi ikawa ni nani atakaejitolea kwenda kumpa taarifa mzee Patili,kila mtu alikua anahofia kwenda kule kwa kale kaumbali mwenyewe ilikua ni kama kujitoa sadaka,hakuna alietaka,kila aliechaguliwa aliuliza kwanini mimi?? Hivyo ikawa ngumu kufikia hitimisho.
Wakati hayo yanachukua nafasi Matata aliufata mwili wa mama yake na kuanza kuuangalia kwa kutoamini huku machozi yakimtoka,alijiuliza juu ya ile nguo aliyovishwa mama yake hakupata jibu,kuna kitu aligundua kwenye ile nguo haraka akaita Babaaa!! Sauti iliyowastua na kuwateka hisia wanakijiji wengine,baba Matata bila kuchelewa alifika eneo aliloitwa na mwanae akauliza
"nini mwanangu??"
huku macho yakiwa mekundu kama nyanya kwa kulia,
"kuna kitu kimeandikwa kwenye hii nguo aliyovalishwa mama!!"
"nini tena hiko??"
aliuliza Baba Matata,kutokana na kutojua kusoma aliamuru mwanae amsomee,matata akasoma kisha akasema..
"imeandikwa BADO KIDOGO!!!"
* * * * *
Baada ya shughuli ya mazishi kuchukua nafasi ilimbidi mzee Patili afunge safari ya kurudi kwake,aliwaaga wakina Madhifa waliokua wanatayarisha tayarisha kwa ajili ya usiku ule,walimshukuru kwa msaada na pia vilevile aliwahaidi atakuja kesho kuwasaidia shughuli za ujenzi,walifurahi kusikia hilo ila bado nyuso zao zilishindwa kujifungua kwa furaha,mioyo yao bado ilikua na huzuni.
Ilikua ni tendo la ajabu kwa mzee Patili kuondoka na kuelekea nyumbani mwenyewe kwa ule muda ukizingatia vitu vya kutisha vilivyochukua nafasi kijijini,alikua na hofu lakini hakutaka iwe sababu ya yeye kubaki,aliamini kama siku imewadia hawezi likwepa hilo,mikono aliweka nyuma na kwa kasi kidogo alikua anatembea akipita miti na vichaka huku sauti za wadudu wa usiku zikigota masikioni mwake na kumfanya ageuke geuke mara kwa mara,baada ya muda kidogo alikaribia na kwake,macho yake aliyoyarusha mbele yalimruhusu aione nyumba yake ya udongo vizuri,ghafla alisimama!! Macho yake yalimshuhudia pande la mtu likiwa linasogelea mlango wake na mkononi akiwa na kamba,hofu ikagota moyoni,mtu yule alikua mgeni machoni mwake na alihisi vibaya juu yake,akasogea karibu huku akinyatanyata aweze kumuona vizuri,mara lile jitu likagonga hodi Na mtindo ule ule alioutumia kwa mama Matata!!
Nini hiki?
USIKOSE SEHEMU YA 24 IJAYO.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom