Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,051
- 34,788
666-NYAYO ZA KUZIMU..
SEHEMU YA 1
Upepo ulivuma mno,miti na majani ilionekana kuinama kutokana na kushndwa kupambana na pepo ile kali,giza lilikua kali sana kwa kuwa mwezi ulikua umefunikwa gubigubi na wingu zito jeusi lisiloonyesha hata
kama mvua itanyesha.utulivu wa hali ya juu ulitawala,hakuna kilichosikika zaidi ya milio ya kiuoga ya mbwa na vijidudu vidogo vidogo vya usiku,kila kibatari kilichowashwa ilhali na moto ilizimika kutokana na kutokua
stahimilivu na hali iliyokuwepo,hakukuwa na mtu yeyote alieonekana yu nje akifanya jambo lolote,na ni kutokana na hali ya ajabu ya ghafla iliyotawala katika lile eneo.Kwa mbaali angani ilionekana nyota ndogo
ikichomoza,ghafla sauti ya kuamuru ilisikika kutoka kwenye kijumba cha msonge ikisema..
"sukuma,jitahidi Vero sukuma!...enhee..tena...tena!!..ewaaah!...umepata mtoto wa kiume Vero!"
sauti ya mama Marinda mkunga wa jadi Maarufu kijijini iliskika..iliyoambatana na tendo na kumsaidia bibie
Veronica kupata mtoto wake wa kwanza kabisa,upepo ulitulia ghafla,hali iliyomfanya Mama Utopi kupumzika na zoezi la kukikinga kibatari kisizimwe na upepo ili shughuli ile ya Ukunga iliyokua inafanyika ipate kuisha
salmini,alikiweka kile kibatari chini na kusogea karibu zaidi ili apate kumshuhudia mtoto aliyeingzwa
ulimwenguni..
"mbona hata halii?"
akauliza mama Utopi kwa shauku kubwa ya kufahamu,
"mie mwenyewe sijui,kwani miaka yangu yote ishirini ya ukunga sijawah kukutana na hili jambo la mtoto kutolia ingali anaonyesha yu mzima kwa kuchezesha mikono na miguu yake.....
Na isitoshe...ni wa baridi mno! Zaidi hata ya maji ya asubuhi ya mtoni!"
alisema kwa msisitizo mama Marinda huku akimtolea macho mama Utopi aliesimama,Vero hakuchangia chochote kwani hakuwah kukumbana na lile swala kokote pale,hivyo aliishia kuwatazama mama Utopi na
Mama marinda wakiwa wanajibizana.Mama marinda aliemshkilia mtoto alianza kuingiwa na hofu,alimtazama yule mtoto kwa macho yakinifu hakupata jibu,alionekana ni mtulivu mno,hakuonyesha dalili ya kucheka wala
kulia,Mama Marinda akaanza kuhisi mapigo yake ya moyo yanaenda mbio,jasho lililojaa uoga taratiibu lilishuka...
* * * * * *
USIKOSE SEHEMU YA PILI!