666-nyayo za kuzimü

666-nyayo za kuzimü

kaka mzizimkavu umetisha,hadi nimeacha kufanya project kisa nafuatilia story napendekeza story kama hzi uwe unasimulia wakati wa likizo tymeeee
 
666-NYAYO ZA KUZIMU--13-

Mungu wangu wale walikua wakina mama Kadogo!!
Jeshi la 666 liliongeza kasi huku macho yao yakieka msisitizo kwa wale watu kwa mbali waliowaona,mzee Otongo alihisi watu wanakuja kwani alisikia vishindo vikubwa na sauti za watu ambao hazikuleta maana masikioni mwake,aligeuka na kumshika

mkono mama Kadogo na kuanza kukimbia nae kwa kasi!!.

"mama Kadogo kimbia wanakuja!!!"
kwa tahamaki alitamka huku akimvuta mama Kadogo alietia kidogo uvivu,mzee Otongo alijitahidi kumburuta mama Kadogo alieonekana kama mzigo kwa nguvu zake zote na hakutaka kabisa kumuachia,mama Kadogo hakutamka neno lolote kitu

kilichoonyesha ya kwamba alishakata tamaa hata ya kuishi!!..hata kasi yake ya kukimbia ilikua ni ile ya kukosa matumaini kabisa!

Jeshi! Jeshi! Jeshi la 666 lilizidi kuwakaribia wakina mama Kadogo na huku mbele yao akionekana mama Utopi ndie aongozae msafara!

Kanzu yake aliyovalishwa yenye rangi nyeupe nusu na nyekundu haikutosha kumzuia kukimbia kwa kasi mithili ya simba alieona swala,aliruka viunzi na visiki,aliruka mashimo na vizingiti lengo kichwani likiwa moja tu,la kumuangamiza mtoto aliezaliwa na kuua wote wale waonekanao vikwazo kwao,

kimbia! Kimbia! Kimbia!

Alizidi kusema mzee Otongo kwa sauti iliyokaribia na kulia huku bado aliekua anamvuta akiwa kimya na mzito kama furushi la dhambi!


Hayawi hayawi yakawa! Mama Kadogo alipigwa na gongo mgongoni na kudondoka kama mzigo chini!!

Alilia kilio cha maumivu kilichokwangua hadi sakafu ya moyo wa mzee Otongo aliegeuka na kushuhudia jeshi! Jeshi! Jeshi la 666 likiwa tayari karibu nae lishawadia,
alipigwa kofi moja kali lililomrusha mbali mithili ya mtu aliepigwa na shoti ya umeme!

Hata kabla ya kufungua macho yake alisikia mgongo wake ukiita kwa mlio wa nguvu uliosababishwa na kupigwa na gongo!

Aaaaaaahhh!! Alilia mzee Otongo kwa uchungu wa maumivu ambao haukusaidia hata kidogo kumuokoa na kipigo alichokua anakipokea toka kwa jeshi! Jeshi! Jeshi la 666,alipigwa kipigo cha mbwa mwizi!

Alipigwa kila eneo na alichanwa chanwa mgongoni na makucha ya wale watu walio na mioyo ya wanyama!

Hakuwahi kuhisi maumivu kama yale toka azaliwe na mama yake Lenaka miaka arobaini na mbili iliyopita ndani ya kijiji cha Igesambo! Macho yake yalianza kupoteza muelekeo na yakaanza kuelekea juu kisha yakafumba kabisa!

Upande wa nyuma hatua kama tano mama Kadogo alikua bado anashushiwa kipigo na wanawake wenzake wakina mama Marinda,Vero na mama Utopi waliokua wanyama tayari chini ya CHERNOBOG!!

Hawakua na fikra za huruma hata kidogo! Hawakua na mioyo ya kibinadamu! Hawakumjua tena mama Kadogo na akili yao haikua tena ya binadamu hivyo walitumia kila zana ikiwemo mikono yao iliyo na kucha mithili ya simba kumjaza alama za kutosha mmama yule alieonekana yu kimya!!

Kabla ya wao kuridhika na lile zoezi ghafla jua lilianza kuchomoza,anga likaanza kuwa la kahawia na giza likaanza kupotea!!

Walipigwa na butwaa na kuwehuka huku wakitoa sauti za ajabu na wakikimbia huku na huko bila mpangilio kurudi kule walipotokea,walichanganyikiwa baada ya kuona ile hali na zile chapa zao zilizo juu ya mapaji yao ya uso zilianza kufuka moshi uliodhihirisha ya kwamba wanaungua!!!
Hae hae lile eneo lilikua! Lakini bado mama Kadogo na mzee Otongo walikua kimya huku miili yao ikivuja damu!!
Je watapona? Na itakuaje baada ya jua kuchomoza?


USIKOSE SEHEMU 14 IJAYO!
 
Mie najua mzee otongo atafanikiwa kumsuru huyo mkombozi wao!vry interestn,cnt wait to read it more n more!
 
666-NYAYO ZA KUZIMU--14-

Kabla ya wao kuridhika na lile zoezi ghafla jua lilianza kuchomoza,anga likaanza kua la kahawia na giza likaanza kupotea!!
Walipigwa na butwaa na kuwehuka huku wakitoa sauti za kupayuka na wakikimbia huku na huko bila mpangilio kurudi kule walipotokea,walichanganyikiwa baada ya kuona ile hali na zile chapa zao zilizo juu ya mapaji yao ya uso zilianza kufuka moshi uliodhihirisha ya kwamba wanaungua!
Hae hae lile eneo lilikua!
Lakini bado mzee Otongo na mama Kadogo walikua kimya huku miili yao ikivuja damu!
Kuchomoza kwa jua kulithibitisha kushindwa kwa CHERNOBOG (Mungu mweusi),lengo la kumuangamiza mtoto aliezaliwa ilibidi lifanyike haraka na kwa ufanisi mkubwa kabla ya jua kuchomoza kwani nguvu zake zina mipaka,zina mipaka? Ndio zina mipaka,wakati wa usiku huwa ni kali na za kutisha zaidi na ndio mana walitaka watekeleze ule mpango kabla ya jua kuchomoza ili kuhakikisha ya kwamba jua halitokutana tena na uso wa dunia,hivyo utawala utakua wao daima na milele!
Masaa yalizidi kusonga huku miili ya mzee Otongo na mama Kadogo ikianza kuzongwa zongwa na Inzi waliofuata majeraha makubwa waliosababishiwa na jeshi! Jeshi! Jeshi la 666,saa nne asubuhi isiyotambulika madakika yake watu watatu waliokua katika shughuli za uwindaji toka kijiji cha jirani Utowele waliiona miili ile miwili iliyolala kama mizoga,walishtushwa na lile jambo! Na moja kwa moja walidhani ya kwamba watakua wamedhuriwa na wanyama wakali wa msituni kwani safu ya milima Iramba ina wanyama wakali kama chui na simba ambao ni mara chache kuonekana mida ya asubuhi na mchana,mapigo ya moyo ya mzee Otongo yalisikika kwa mbali sana! Vile vile na ya mama Kadogo kitu kilichoashiria ya kwamba hawana muda mrefu maisha yao yatarudi yalipotokea,yani mavumbini.
Wale watu watatu,mmoja akiwa ni mzee wa makamo na wengine wawili wakiwa vijana,waliibeba ile miili na kuelekea kijijini kwao,ilibidi wasitishe lile zoezi la uwindaji kwa sababu za kibinadamu,je watapona? Hilo lilikua ni swali lililokita kichwani mwa wale watu walioonyesha roho za utu.
Baada ya mwendo wa robo saa waliingia kijiji cha Utowele,kijiji walichokua wanakitafuta wakina mama Kadogo kabla ya kukumbwa na la kuwakumba,kijiji chenye wakulima na wafugaji kwa kiasi kikubwa,kila mtu alishangazwa na ile hali! Na pia walibumbazwa na lile tendo! Hawa mbona wametuletea mizoga? Hilo ndilo swali lililokuja kichwani kwa kila alieshuhudia lile tukio,haraka taarifa zilienea! Kila mtu alieona alimtaarifu na mwenzie,mwisho wa siku kijiji kizima!
We baba Madhifa mbona umetuletea mizoga kijijini kwetu??? Maswali yalirushiwa kwao,kila walipotaka kujibu walikumbana na lingine! Na hali ilikua mbaya zaidi baada ya kusema kuwa wameiokota msituni,wanakijiji walicharuka! Waliwataka wakina baba Madhifa na wanae wawili wairudishe ile miili kwani wanaweza wakaleta laana kwenye kijiji chao,hakuna alietaka kuwasikiliza kwa maelezo zaidi na ukizingatia wakina baba Madhifa ni jamii ndogo ya wawindaji kwenye kijiji cha Utowele kilichojazwa kwa kiasi kikubwa na wafugaji na wavuvi.
Tokaaa!!! Peleka mizoga yako huko!!!!!
Hatutaki maiti tusizozijua kijijini kwetuuu!!..we una okota okota tu!!
Maneno ya kebehi na kashfa yalirushwa kwao yaliyochanganyikana na dharau kutokana na hadhi yao ndogo ndani ya kijiji cha Utowele,waligeuka na kuanza kurudi msituni walipotokea baada ya kuona zoezi lao lilioambatana na utu limepingwa vikali na wanakijiji wenzao,ghafla kabla ya kutokomea,sauti ilisikika toka kwa mmoja wa wanakijiji aliyeonekana ni mkubwa kiumri akitokezea toka kwenye mlango wa nyumba ndogo ya udongo iliyojaa moshi ndani kutokana na shughuli ya upikaji dawa aliyokua anaifanya,
"suubiiiiiirrrriiiinii!!"
huku akiambatanisha na zoezi la kupunga mkono!
"waleteni hao watu!!"
"sio watu,ni miili ile! Wamekufa!"
sauti ya mmoja wa wanakijiji iliskika ikipinga,
"nyamaza!! Nani kakuambia wamekufa??"
aliuliza yule mzee na kufanya kidogo ukimya utawale huku macho ya wanakijiji yakionesha kujawa na hofu,
baada ya muda mfupi baba Madhifa alikua ashafika kwenye eneo la tukio na wanae wawili waliowabeba wakina mzee Otongo na mama Kadogo,waliiweka ile miili chini kama walivyoelekezwa,yule mzee akaanza kuikagua!
* * *
JE ITAKUAJE?
Usikose sehemu ijayo!!!!

USIKOSE SEHEMU 15 IJAYO
 
666-NYAYO ZA KUZIMU-15-

Ilichukua kama dakika kumi yule mzee akiitizama na kuipekua ile miili huku wanakijiji wakiwa wamemzingira,aliinua macho yake na kutoa amri ya ile miili kuingizwa ndani,wale vijana wa baba Madhifa walitekeleza hilo jambo haraka,waliingiza ile miili ya

mzee Otongo na mama Kadogo ndani ya kale kajumba kadogo cha udongo cha yule mzee alieonekana kuheshimiwa na kusikilizwa na wanakijiji,bila ya kujivunga yule mzee nae aliingia ndani na kuwaacha nje wanakijiji waliokua na shauku kubwa ya kutaka jua kinachoendelea,baadhi yao walianza onekana wakijiondoa kwenye lile eneo taratibu na kwenda kuendelea na

shughuli zao zingine huku bado midomo yao ikiteta lile tukio lililoonekana kuchota hisia zao kwa kiasi kikubwa,wakati hayo yote yanachukua nafasi kuna baadhi ya wanakijiji walikua hawana habari kabisa kuhusu lile tukio!!...labda kutokana na kubanwa na

hali husika,umbali wa nyumba kumi na tano toka pale pa yule mzee kulikua na nyumba moja tulivu ya udongo iliyopakwa chokaa iliyofanya ionekane ni ya kipekee kidogo tofauti na nyumba zingine,madirisha yake makubwa yapitishayo hewa na sauti bado

hayakutosha kuwajuza watu walio ndani juu ya kinachoendelea kwa nje,nyuso zao zilijawa na tabasamu na huku wakionekana

kutowaza kabisa yanayojiri ulimwengu mwingine,

"enhe..sasa nimpe jina gani?"
lilikua swali alilouliza mdada mmoja aliemshika mtoto akijulikana kama Julina huku akitabasamu
"mmh mie mwenyewe sijui,we si ndo mama bwana! Mie kazi yangu ya ukunga nshaimaliza"
alijibu mama Halima,mmama mwenye rangi ya maji ya kunde,mkunga maarufu kijijini aliebakia baada ya kifo cha mama Ramla miaka miwili iliyopita,
"au tumsubirie baba yake?"
"utakavyoona wewe ni sahihi..."

"ujue nini mama,mimi ni kama mwanao,sina utofauti na mwanao Halima,sijui hata nikushukuru vipi kwa kweli,namsubiria tu mume wangu arudi ndipo tutakapojua cha kufanya"

"wala usihofu mwanangu,ujue hii kazi ya ukunga ni kama karama kwangu,si ajira!! Kwahiyo naifanya kwa ajili tu ya kuwasaidia

wanizungukao kwani baada ya mwanangu Halima kufariki,kila mtoto nizalishae ni kama mtoto wangu"


"pole sana mama,kifo cha Halima kiliniachia pia pengo kubwa,kama unavyojua,alikua ni rafiki yangu mkubwa! Yeye ndo kwa kiasi kikubwa alinishawishi niole na Kitanzi"

"tuachane na hayo mwanangu nisije nikatonesha donda lililoanza kupona,ila mumeo Kitanzi yupo wapi saa hizi?"
"mmmh...hata sifahamu kwa kweli,aliahidi kuwa atakuwepo hapa usiku wa jana,lakini mpaka saa hizi sijamtia kwenye zangu mboni"

nyuso zao zilificha matabasamu yalionawiri hapo kabla,mawazo yakaonekana kuwashika hatamu,Julina alianza kupata hofu,mama Halima akaligundua hilo..

"sikiliza mwanangu,ujue sisi binadamu tunapanga na mungu pia anapanga,hivyo huwezi jua,tuombe tu uzima!"
"mmh kweli mama.."

kidogo maongezi yaliingiliwa na kilio cha mtoto,mtoto alieonekana hana muda mrefu ulimwenguni,haraka Julina alitoa titi lake la kushoto na kumyamazisha nalo,uso wa Mama Halima ulionekana unaficha jambo,na hata macho yake yalikua yanasadifu ya kwamba ana kitu ndani ya mtima chamsumbua..


"mama vipi??..mbona hivyo tena!"

"mmh,kuna kitu kinanitatiza kusema kweli,jana usiku wakati tupo katija zile shughuli za kufungulishana nilisikia kelele!!"
"kelele??...si kelele zangu hizo ama?"
"hapana!...mara ya kwanza ilikua ni kelele ya kike,na mara ya pili ilikua ya kiume!!!"
"wee!..mie mbona sikuzisikia??"
"usingeweza kuzisikia,uchungu uliokua nao usingekuruhusu ufanye hilo.."
"mama una uhakika na hilo jambo??"

aliuliza Julina kwa umakini huku akimtikisatikisa mwanae kitaratibu,

"asilimia zote!...na ubaya ni kwamba kila ninapotulizana,zile sauti hunirudia masikioni!!!!!"
kwa msisitizo alinena Mama Halima huku akiyatoa macho,hofu ikaanza kumrudi Julina tena!!...huyo atakua sio mume wangu kweli?? Alijiuliza moyoni,kabla hajapata majibu,hodi ikaskika!

"ngo!-ngo!-ngo!"

"nani??"
aliuliza mama Halima,
"wageni!!"
sauti ilijibu toka nje,
"wakina nani?"
"wageni!!"
ilirudia tena!

Ilimbidi mama Halima ainuke na kwenda kuchungulia dirishani kabla ya kufungua,he!! Alishuhudi mabibi wawili wageni machoni wakiwa mlangoni!!..aligeuza shingo yake na kumtizama Julina kwa tahadhari,

"unawajua hawa watu?"
aliuliza,
"wakina nani?"
"njoo uwaone!"

alielekeza kwa sauti ya chini iliyokamatwa na kauoga,

Julina aliwatazama wale mabibi kupitia pale dirishani kisha akamjibu mama Halima kwa kunong'oneza,
"mmh mh,siwajui!!!"
* * * *

je hao watu ni wa kina nan? Wana uhusiano wowote na jeshi! Jeshi la 666?

Vipi kuhusu mume wa Julina,kitanzi?
Mzee Otongo na Mama Kadogo wanaendeleaje? Na lengo la kumuokoa mtoto litafanikiwa?
Jeshi la 666 lipo wapi?


USIKOSE SIMULIZI HII YA KUSISIMUA SEHEMU 16 IJAYOO.........
 
Bado tunaendelea kuisoma


||"Tomorrow will say its a memory and we have enjoyed our lives for a couple of days."||
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom