666-nyayo za kuzimü

666-nyayo za kuzimü

666-NYAYO ZA KUZIMU--16-

Cha kushangaza walivyorudisha tena nyuso zao dirishani kutizama nje...hawakuona kitu!!!!..Pah!!!..tik-tak!!! Tik-tak!!! Tik-tak!!! Tik-tak!!..mioyo yao ilianza kwenda kasi ya ajabu!!! Bumbuwazi lilikamata midomo yao bara-bara! Macho yaliwatoka mithili ya kwamba wamemshuhudia shetani akionja pepo!!!..walitupiana macho ya uogo wakiulizana wameenda wapi??? Swali lililopasua hisia zao mithili ya shoka kali lililotoka kiwandani kwenye gogo bua lililochoka!
Mungu wangu..watafanyaje sasa?? Hilo lilikua ni swali la pili rejea lililokita vichwani mwao kama hitimisho!!!
Hapakukalika tena!!..nyumba ilizidi kuwa ndogo kwao!
* + * + *
koh-koh! Sauti ya kikohozi cha maumivu kiligona sikioni mwa mzee Patili,aligeuka haraka na kuangalia kilipotokea akagundua ya kwamba chatoka kwa mzee Otongo aliekua amelala chini chali,alitabasamu kwa mbali,jitihada za dawa yake aliyompaka zilionekana kuvuta kheri,hakutaka kupumbazwa na hilo jambo,aligeuka na kuendelea na shughuli yake ya kumpaka dawa mama Kadogo taratibu akimalizia miguuni baada ya mikononi na usoni akijitahidi kuyaziba majeraha na dawa ile ya unga yenye rangi ya kahawia,mchanganyiko wa miti mbalimbali iliyosagwa.
Chumba kilitawaliwa na moshi kwa kiasi kikubwa,lakini hilo halikuonekana kumkwaza mzee Patili,kwani tangu na tangu,enzi na enzi amekua katika yale mazingira ambayo hasa huchangiwa na shughuli zake za upikaji dawa,mvi ziligoma kabisa kuja kichwani japokua umri uliruhusu hilo,uso wake ulio na makunyanzi ndio uliothibitisha ya kwamba kala chumvi,mzee Patili alikua ni zahanati tosha pale kijijini,akiheshimika na kusikilizwa kama marehemu baba yake aliemrithisha hizo kazi.Baada ya kumaliza ile shughuli ya upakaji dawa,alishusha pumzi ndefu kisha akajituliza kwenye kigoda chake chenye ufa kwa mbali uliodhihirisha ya kwamba ni cha muda mrefu,haraka akili yake ilimtumbukiza kwenye lindi la mawazo,lindi la mawazo mazito juu ya ndoto aliyoota usiku wa kuamkia hiyo alfajiri,ndoto ile ilionekana kumkosesha amani na hata raha vilevile na kila alipotaka kuitafutia ufumbuzi hakupata kitu!!!
Alitizama juu ya dari kimawazo huku kichwa kikiegemea mkono akijaribu kuitumikisha akili yake iliyojaa uzoefu wa maisha kumpa majibu,
ghafla!!!!
"mzee patili funguaaa!!!"
sauti za kile zilisikika toka nje,
"niniii???..nyie wakina nani!!!"
kwa tahamaki aliuliza,
"Julina na mama Halima!!!..tafadhali tufungulie haraka!!"
alijibiwa,alijinyanyua toka kwenye kile kigoda haraka na kuelekea mlangoni,akaufungua mlango na haraka kwa papara waliingizana wakina mama Halima!!
"nyie vipi???"
aliuliza mzee Patili,hakujibiwa,akauliza kwa mara ya pili kwa sauti ya msisitizo!
"nyie kuna nini?? We mama Halima vipi na huyu Mzazi tena!!!"
huku wakihema kwa pupa wakajibu,
"kuna wabibi wawili!!"
"wamefanya nini?"
"wa..wa..walikua wanagonga..mm..mlang..mlango.."
"halafu haraka wakapotea!!!"
Julina akamalizia sentensi huku akiwa kamkumbatia mwanae na mikono itetemekayo!,
"wakapotea!!! Wakaelekea wapi??"
"hatujuuii!!!!"
julina alidakia,
"he! Mzee Patili hawa waliolala hapa chini wakina nani???"
aliuliza mama Halima baada ya kuiona ile miili ya mama Kadogo na mzee Otongo pale chini,Julina pia mwenye damu iliyotawaliwa na uoga nae alistuka baada ya kuona hilo,akatahamaki
"mungu wangu!!!! Mzee Patili hawa wakina tena???"
"msijali kuhusu hao watu,waliletwa hapa na baba Madhifa,waliokotwa toka porini,embu punguzeni uoga na presha enh...tulieni embu,tulieni kisha mnielezee kilichojiri"
aliwatuliza mzee Patili.
Mzunguko wa damu wa Julina uliongeza kasi kutokana na uoga! Alikua anahema kwa kasi,mama Halima vilevile!
Mzee Patili ilimbidi anyamaze huku akiwashuhudia wale wakina mama kwa jicho la kutafakuri hali ile iliyowatokea,moshi uliokuwemo mule ndani ulianza kumuathiri mtoto,akaanza kupaliwa na kikohozi hali iliyomfanya mzee Patili kumshauri atoke nje,kiuoga alijibu
"nani?? Mie!! Ah-ah sitoki nje! Wale wabibi watanifata!!!"
mzee Patili aliamua kumaliza zogo,alimnyakua mtoto toka kwenye mikono ya mama yake Julina kisha akatoka nae nje,hali ya kushangaza Julina nae kwa uoga akatoka nje!!!!
* * * * *

JE ITAKUAJE? Usikose! SEHEMU 17 IJAYOO....
 
mh huyu mzee Patili nae.....dah sijui itakuaje. Mziz makavu endelea kutupa burudani zinazottufundisha na kututoa katika dimbwi la mawazo. umetisha kaka
 
666-NYAYO ZA KUZIMU-17-

"vipi tena si ulisema hutoki nje??"
aliuliza mzee Patili,

"eh! Yani mie nibaki peke yangu ndani??..wale mabibi si watanifuata!!"

akajibu Julina huku macho ya uoga yakipendezesha uso wake mwembamba mweusi.Punde si punde mama Halima nae alitoka nje na kujumuika na Julina na mzee Patili aliembebelea mtoto,walianza kuteta kuhusu wale mabibi na pia bila kusahau ndoto ya

mzee Patili iliyowashangaza na kuwaogopesha wakina Julina kwa kiasi kikubwa!

"mito ilikua miekundu,haikuskika tena sauti za ndege,milio ya shida na malalamiko ndio iliyotawala,harufu ya kifo na umauti ndio iliyoshika hatamu,miti ilipendezeshwa na miili iliyoning'inia kwa kunyongwa,na mioyo ya binadamu ilikua ni ya wanyama,tena wanyama haswa!!!"

alizidi kudadavua mzee Patili ile ndoto huku macho ya wakina Julina yakiwa yanakaribia kutoka kwa mshangao!!

Akaendelea,
"kila mmoja niliemuona alikua na chapa ya namba mwilini mwake!"
"chapa!!..ipi tena??"
Julina aliuliza kwa mjazo wa kutaka kujua,kwa masikitiko alijibu mzee Patili
"chapa yenye namba tatu,sita zilizorudiwa mara tatu,yani 666!!!..cha kutofautisha tu kilikua ni wapi hiyo chapa

ilipokuwepo,wengine kwenye mapaji ya uso,wengine mikononi,wengine mapajani na kadhalika! Maisha hayakua kama yalivyo,maisha hayakua kama tunavyoyajua,kila mtu muoga na maisha yake alikubali kubandikwa chapa itakayomuwezesha kuendelea kuishi,na wale wenye misimamo yao,walinyongwa kama kuku!!!"


maneno hayo yalizidi kuteketeza amani ndani ya mioyo ya wakina Julina na pia kuzidi kupalilia roho ya uoga iliyochipukia kwa kasi!!....taswira ya kile kilichokua kinaelezewa na mzee Patili ilikua imejengeka ndani ya vichwa vyao hivyo kuipa mwanya hisia za uoga kukumbatia mioyo yao iliyokua inaenda mbio!!

Udadavuaji wa ndoto ulizidi kutolewa na mzee Patili,lakini kabla ya kumalizika alikuja mama Tito kwa kasi huku akiwa kashikilia

kichwa na anapiga ukunga,ilikua haiitaji vipimo kujua ya kwamba alikua kwenye matatizo!!

"uuuuwwwiiiiiiii!!!!....Maamaaa weee!!! Mungu wangu eeeenhh!!!...jamaniiiiii!!!!"
"mama Tito vipi tenaa???"
aliuliza mzee Patili kwa hamaki huku wakina Julina wakiwa wameishiwa pozi kwa mshangao!!
"mume wangu jamaniii!!!!...mume wangu..mungu wee!! Mume wangu Jamanii!!!!!"
"sasa mume wako kafanya nini???"
"nimemkuta mume wangu kanyongwa kule shambani,jamani baba Tito wanguuuuuwwii!! Mume wangu mie ntaishijeee!!!"
sauti kali ya kilio ya mama Tito iligonga kwenye masikio ya wanakijiji,haraka lile eneo lilifurika watu,habari za kunyongwa Baba Tito zilihamsha taharuki,msururu wa watu ulianza safari na kuelekea eneo la tukio wakiwemo mzee Patili na wakina Julina ambao hawakutaka kabisa kubaki pale kijijini.

Sauti za vilio vya wanawake ilipata kusikika vizuri,tahamaki ilimshika kila mtu,kuona mwili wa baba Tito ukiwa unaning'inia kwenye mti ule wa muembe halikua tendo la kawaida kabisa machoni mwao! Hisia za uoga zilitawala na baadhi yao wenye roho ndogo walizirai akiwemo Julina!!


Nani amefanya haya?? Na amefanya kwa madhumuni gani?? Kila alieshuhudia lile jambo alijiuliza na kuwauliza wenzake pia,sauti ya kilio cha mama Tito iliyokua inazidi kupotelea kutokana na kukaukiwa sauti ilizidi kuchimbua na kumwagilia huzuni iliyodamiri lile eneo,na pia tukio la kumpepea Julina aliezimia liliendeleza hofu mioyoni.


Mwili wa Baba Tito ulishushwa na kufunguliwa toka kwenye kile kitanzi,na taratibu ulibebwa kupelekwa kijijini kwa ajili ya shughuli za mazishi huku bado maswali mengi yakizaliwa ndani ya vichwa vya watu waliokua pale juu ya kipi hasa kinachoendelea.

Wakati safari ya kurudi kijijini ikiwa inaendelea ghafla mjadala mzito ulianzishwa,mjadala uliokua unaongelea juu ya ujio wa Mzee Otongo na mama Kadogo kama sababu kubwa iliyopelekea ile hali,yani ujio wao ndio umeleta laana pale kijijini na ndio mana mambo ya ajabu yameanza kuchukua nafasi!!

Asilimia kubwa ya watu walionekana kuafiki hilo jambo isipokua Mzee Patili aliesimama kidete kukanusha hilo kwa nguvu zote na kutetea tendo lake la kuwapokea wale watu kwamba lilikua sahihi.

Mama Halima hakua na la kuchangia kwani hakushuhudia hayo mambo na pia Julina hakupata hiyo fursa kwani alikua bado hajazinduka,mtoto wake alikua amebebwa na mzee Patili na mwili wake ulikua mgongoni mwa Mama Halima!
Je itakuaje? Na ni nani anahusika na hayo mauaji? Wakina mze Otongo watakua salama mbele ya wanakijiji?

USIKOSE SEHEMU YA 18 IJAYO.....
 
Mzizi bwana usiwe una post usiku pz.utafanya wengne tuachike ujue manake usku ni full kuweweseka cz ya hofu ya hii hadithi inavyotisha hubby anashangaa ,asije zania Nina mapepo anitwange talaka plz save my marriage bwana mie bado penda mjew Wangu lol..Fanya kupost mchana
 
666-NYAYO ZA KUZIMU--18-

Kwa mbali sauti za vilio zilifika kwenye masikio ya mzee Otongo,mwili wake bado ulikua unavuta kwa maumivu japokua fursa ya kuishi bado ilikuwepo mikononi mwake,tumbo lilikua linamuuma kwa sana ilihali na kichwa kutokana na dhoruba kali aliyokumbana nayo ya Jeshi! Jeshi! Jeshi la 666! Alitaka kujiinua,mungu wangu!! Alisikia mpasuko wa maumivu umepita mgongoni pahh!!...ka sauti ka kulalamika kakaitika..aaaahh!!! Kilichoashiria ya kwamba maumivu yamegota penyewe,aliurudisha mwili wake chini na kugeuza shingo kutizama pembeni alipomuona mama Kadogo ambaye bado fahamu hazikurudi kwenye makao yake,alipandisha na kushusha macho yake juu ya mwili wa mama Kadogo na kushuhudia jinsi gani majeraha yalivyoshika utawala,kila pande ya mwili wake ilikua na jeraha na hata alivyojiangalia mwilini mwake aligundua hilo,macho yake yakaanza kubarizi lile eneo alilokua,kuanzia juu chini na pembezoni,umbali wa hatua tano toka alipokua kulikua na jiko litumialo kuni,na sufuria ilikua juu ya mafiga.kilichomo ndani ya sufuria kilionekana kuchemka kwani sauti ya kutokota kupita kiasi na mvuke mkubwa kutoka kwenye sufuria zilithibitisha hilo,mzee Otongo alitambua hicho kitu lakini mwili wake usingeweza kumruhusu kusogea kutokana na mzigo wa maumivu aliokua nao,sauti za watu zilizidi kufika masikioni mwake na mwishowe alisikia mlango unafunguliwa,alikua ni mzee Patili,macho yao yaligongana na kidogo kamshangao kiliwapitia,taswira ya mzee Patili haikua ngeni machoni mwa mzee Otongo ila haikua hivyo kwa mwenzie ambae ilikua vigumu kumtambua kutokana na kile kipigo kumchakaza sura yake kwa kiasi kikubwa,hawakuongea kitu,mzee Patili alifunga mlango na mkono wake mmoja uliokua haujamshikilia mtoto na kufanya sauti za wanakijiji zilizokua bado zinaruruma kwa nje juu ya ujio wa wageni pale kijijini zififie kidogo,
"vipi unaendeleaje??"
mzee Patili aliuliza,
"...mmm..kichwa kinanigonga mno,mgongo nao,vilevile tumbo!!!...issshh!!"
alilalamika mzee Otongo,
"usihofu,mpaka jioni utakua ushapata unafuu kwani hiyo dawa niliyokupaka ni nzuri sana kwa majeraha na kutuliza maumivu.."
"ahsante sana!..eti,kwani hapa ni wapi??"
aliuliza mzee Otongo ili kupata uhakika wa pale alipo baada ya nafsi yake kumtonya kwamba ni utowele,
"upo kijiji cha Utowele kwa sasa,kwani nyie mlikua mnatokea wapi na mnaelekea wapi??"
"tulikua tunatokea Igesambo,na safari yetu ilikua ni kuja hapa Utowele.."
"mmmh...kufanya nini??"
aliongezea swali lingine,mzee Otongo alijivutavuta huku akipambana na maumivu na mwishowe akakaa,kisha akajibu kwa tabu..
"lengo letu lilikua ni kumuwahi mtoto aliezaliwa.."
kauli hiyo ilimshtua mzee Patili! Hakuna mtoto aliezaliwa kijijini zaidi ya yule aliembeba,mtoto wa Julina!!!"
kwa hamu ya kujua akaongeza swali lingine..
"mtoto aliezaliwa?? Wa nini hasa??"
"huyo mtoto ndie uhai wetu,ndie tumani letu na utawala wa giza ulilijua hilo na ndio mana walitujeruhi,kutudhoofisha na kufanikisha lengo lao la kumuwahi,na hata huku kuchomoza kwa jua ni ishara ya uzao wake....ila yu hatarini na inabidi alindwe kwa nguvu zote kwani jeshi! Jeshi! Jeshi la 666! Wanamsaka kwa hali na mali wamtokomeze!!"
maneno yale yalipenya mpaka kwenye mishipa ya damu ya mzee Patili na hapo ndipo alipoanza kupata mwanga juu ya ndoto aliyoiota,lakini kuna kitu aligundua! Haraka akauliza
"wewe ni Otongo??"
"naam...ndie mimi!..bila shaka wewe ni Patili!"
"haswaa mie ndie!"
kile kitu kilimshangaza sana mzee Patili,ni muda mrefu umepita toka walipokua pamoja kutokana na uhusiano wao wa kikazi wa kiganga na hakutegemea kama wangekutana katika ile hali!!
Ila bado mawazo yalizidi kumsonga kichwani!!!
* * * *
nje ya kijumba cha mzee Patili bado wanakijiji walionekana kuteta hasa juu ya kifo cha baba Tito ambaye mwili wake ulikua ushahifadhiwa ndani kwake,kutokana na ugumu wa kujua kinachoendelea kila mwanakijiji alitupia hisia zake juu ya wale wageni waliofika ya kwamba kwa njia moja au nyingine wanahusika,nani unadhani?? Ni hawa hawa tu!! Mbona hayajawahi kutokea tangu na tangu?? Hii ni laana!!! Hawa watu wametuletea laana!! Tutakwisha jamani!!! Wanakijiji walipayuka,ngebe za wanakijiji zilizopamba moto juu ya kukemea na kulaani tendo la ujio wa wale wageni bado hazikubadilisha kitu!!!
ALINYONGWA MWINGINE MTU MWINGINE!!! NA TENA ALIKUA NI MAMA TITO!!!...PEMBENI YA MAITI YA MUMEWE!!! nani anafanya haya mauaji? Kwanini anaua?? Amedhamiria nini?? Nini hatma ya wakina Mama Kadogo mbele ya kiza cha jamii??
* * * * * *

USIKOSE SEHEMU 19 IJAYO,USIDHULUMU NAFSIYO!
 
Oh just in time


||"Tomorrow will say its a memory and we have enjoyed our lives for a couple of days."||
 
Duh! Asante MziziMkuu ingawa inatisha sana,lakin inatukumbusha sana tumrudie Mungu.
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu roho yanipwita....natamani utupie vipande vilivyobaki. Nina mawazo mengi mpaka kichwa kinauma. Maswali mengi majibu sina🙁🙁🙁:what::what::what:😕😕😕😕
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom