666-NYAYO ZA KUZIMU--29
Wale waliokua wanawashwa wakaanza kukauka na kua magofu meupe kama chumvi!!!
Kilio kilichobeba uchungu na uoga kilipata kutoka vizuri toka kwenye midomo ya wakina mama na watoto,vilevile mioyo ya wakinababa ilikita kwa nguvu na macho yao yalitoka kwa kutoamini,ulikua ni kama mchezo wa kuigiza,sehemu ile yote ilitawaliwa na magofu ishirini na mawili yote yakitokana na ile dawa ya awamu ya pili! Wanakijiji walipungua kwa kiasi kikubwa,watoto wengi walipoteza wazazi,wanawake wengi walipoteza waume zao,na hata vile watu wengi walipoteza watu wao wa karibu,simanzi iliyoje!!!
Mzee Patili alichanganyikiwa kabisa,hakujua cha kufanya japokua mzee Otongo alikua anajitahidi mno kumtuliza,alijiona yeye ndie muuaji na hata baadhi ya wanakijiji walianza kufikiria hivyo,walifikiria ya kwamba vile vifo ni dhahiri vimesababishwa na mzee Patili ilihali wengi wao bado walikua kwenye tahamaki ya njia panda hasa baada ya wale walioleta dawa kupotea kiajabu machoni mwao!!
Mama Kadogo aliutumia ule mwanya kuita rai na kuteka hamsha za wanakijiji,kwa kujiamini alisimama mbele yao na kusema
"Jamani..jamani!! Naomba tusikilizane! (ukimya ukatawala lakini bado vikwikwi na vimafua vya vilio vilikua vinachukua nafasi)....katika vita hii tunayopambana nayo kufa kwa mtu au watu isiwe kitu cha kutushangaza,mtu yeyote kwa muda wowote anaweza akafa kwenye mapambano haya hilo inabidi liwe kichwani,naomba tusiruhusu roho za simanzi ziweke kiza kwenye njia yetu bali roho ya ushupavu na ya kusonga mbele,ni hakika tumezidiwa akili na hili jeshi la 666 katika huu mchezo,waliutumia ipasavyo ule mwanya tuliowapa wa kuwatuma wale vijana,nadhani hilo halina maswali...tumeona kwa macho yetu walivyopotea kiajabu na kuudhihirishia uma ya kwamba wao sio wale tuliowategemea!"
haraka Mwalimu Baraka alidakia
"hakika mama,hakika!! Wale hawakua wakina Mrisho kama tulivyodhani,mie mwenyewe naweza nikasema hivyo kwa ushahidi wangu mdogo nilioushuhudia,walikua ni watu wa baridi mno! Na hata baadhi ya maswali niliyowauliza walishindwa kabisa kujibu,kusema ukweli nilipata hofu lakini sikuwa na uhakika asilimia mia hivyo nikaamua nijitoe lile eneo kimyakimya!"
maneno hayo ya mwalimu Baraka yaliamsha minong'ono miongoni mwa watu,mama Kadogo aliwatuliza na kisha akaendelea kunena..
"ni matumaini yangu dawa tulizopaka zina msaada kwetu,bado ninaamini hivyo japokua hili tukio la wakina Mrisho linaweza kuwatia mashaka mioyoni,hapo ndipo tunapoweza kurudia kauli yangu ya mwanzoni ya kwamba walituzidi akili,nahisi kuna kitu walichokifanya hawa jeshi ambacho bado hatujakifumbua...."
(kabla hajamalizia mzee Rama kwa jazba alidakia)
"sasa tufanye nini?? Hamuoni ya kwamba tunaendelea tu kufa!! Au nyie bado hamjatosheka???"
kauli ya mzee Rama ilizua tena minong'ono na malumbano,baadhi ya wanakijiji walionekana kumuunga mkono na baadhi yao walionekana kumpinga,makundi mawili yakazaliwa miongoni mwao!! Ni dhahiri imani zao haba zilianza kuwachonyota,mzee Patili taratibu alisimama na kuelekea pale alipo mama Kadogo kisha akawaomba utulivu kwa muda ili apate kunena,wale waliokua bado na imani nae walifunga midomo yao na kumpa masikio lakini wale ambao imani zao zilitiwa doa hawakujali hilo,waliendelea kururuma tu,mzee Patili akatoa tamko..
"kama imani yako haiko nami tena,sitofanya jitihada zozote kuiinua maana umeamua hivyo,kama nilikua nanyi tokea ujana nikiwahudumia na bado imani zenu zina madoa kuhusu mimi,hakuna chochote ninachoweza fanya kwenu kwa sasa.Ninaelekea upande wa kulia nilipotokea,kama bado una imani nami waweza nifuata,kama huna imani nami waweza kubaki.."
sura ya mzee Patili ilionekana si yenye furaha,alikua anawaza jambo na dhahiri alionekana ameumia,alishika njia ya kuelekea nyumbani kwake na kundi la watu huku nyuma lilimfuata akiwemo Julina mwenye mtoto aliebeba matumaini yao,bila hata kuonyesha aibu usoni mzee Rama nae na wenzake walioonyesha kutia shaka juu ya mzee Patili nao walikuwemo ndani ya msafara wakiivuta miguu yao kumfuata,hawakufanya hivyo kwa kupenda bali iliwabidi kwani mtoto ambaye ndie ngao ya matumaini alikua upande ule hivyo hawakua na jinsi,mzee Rama bado alikua na gubu jeusi lililokua linamkereketa,hakupendezewa kabisa na ile hali ya uongozi wa mzee patili,wivu ulimkua unamsumbua kwa kiasi kikubwa,alitaka yeye ndie awe anasikilizwa na yeye ndie awe anatoa amri,wivu ulimshika mishipa yake ya damu,akili yake ilimtuma amuibe yule mtoto wa Julina,alifahamu fika ya kua akimmiliki yule mtoto jamii nzima itamsikiliza yeye kwani ndie atakaekua ameshikilia matumaini yote ya wanakijiji,atafanyaje sasa?? Alijiuliza kichwani mwake,baada ya kupata jibu haraka alimvuta mwenzie pembeni na kumwambia..
"unataka kufa na wewe,ama??"
swali hilo lilimshangaza alieulizwa,kiuoga nae akajibu..
"hapana!!"
"sasa nisikilize nitakayokuambia..."
JE ANATAKA KUMUAMBIA NINI?
UADUI WA MZEE RAMA MWISHO WAKE NI NINI??
USIKOSE SEHEMU 30 IJAYO