Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,741
- Thread starter
- #41
666-NYAYO ZA KUZIMU--10.
Kadogo alikua anahema juu juu na kwa nguvu hali iliyomfanya mzee Otongo amzibe mdomo,ubavu wa mzee yule uliegemeana na wa mama Kadogo aliyekua anatetemeka hivyo mtetemo wote ule uliokua unampitia mama Kadogo alikua anausikia,walitoa macho na kufumba kabisa midomo yao ili wasiskike,huku wakishuhudia watu wale walio idadi ya watu watano wakiwa wanapepesa macho yao kutafuta watu kwa ajili ya sadaka zaidi,mzee Otongo alinong'oneza..
"mama Kadogo tuondoke hapa si salama"
"mh tukiondoka si watatuskia?"
"hapo walipo wananusa harufu yetu na ndo mana unaona wamekazania hili eneo"
"kwahiyo?"
"tuondoke taratibu kabla hawajatugumia"
alizidi kutia msisitizo mzee Otongo,
baada ya muda si mrefu walinyanyuka taratibu toka kwenye kibanda kilichokongoroka walipokua wamejificha,walianza kunyata kama watu wanaohesabiwa hatua,pole pole huku macho ya tahadhari yakiwa yanawatizama wale watu mara kwa mara,mioyo yao ilikua inadunda kwa kasi hasa Kadogo ambaye ana matatizo,alitoka jasho mno ikiwa ni moja ya viashiria ya kuanza kuzidiwa,damu ilikua inazunguka kwa kasi mwilini na mama yake aliligundua hilo,alianza kuhisi mkono wa mwanae alioushika unapoteza nguvu na hakua na jinsi zaidi ya kumnyanyua na kumweka mgongoni,waliendeleza zoezi la kunyata kunyata na kunyata mpaka pale mzee Otongo alipotoa ishara,
"tukimbie mama Kadogo!"
na mbio zikaanza kama za farasi,mzee Otongo alitangulia sana mbele na kumuacha mama Kadogo nyuma hali iliyomfanya aamue kumsaidia mama Kadogo mtoto anaeonekana kumchosha ili wakimbie zaidi,mkono wa mama Kadogo ulishikwa na mzee Otongo kinguvu hasa ili usiponyoke,walijitahidi sana kukimbia huku wakipambana na hali ile ya baridi la usiku na visiki na mawe mbalimbali yaliyoonekana kuwaumiza miguu yao,hawakujali hilo ila walilenga tu kusogea mbele na kuokoa roho zao.Mgongo wa mzee Otongo ulionekana kuhimili mzigo wa mtoto Kadogo ila mama Kadogo ambaye alitoka kukimbia kabla ya kukutana na mzee Otongo alionekana hana nguvu tena ya kuendelea na zoezi lile,alisimama huku akishika kiuno,akasema..
"mzee....uuh!...uuh..siwezi tena!...nimechoka!"
"mama Kadogo jitahidi,hatujawaacha mbali sana wanaweza wakatufikia!"
"mzee Otongo....uuuh..uuh!..nimechoka sana aisee..!"
huku akiinama,
"mama Kadogo!!"
"abee...mzee Otongo"
kiuchovu aliitika
"embu angalia ile!!"
"nini tena??"
mama Kadogo aliuliza,
"ile angani! Ni nyota nyingine ama macho yangu!!?"
haraka mama Kadogo aliyarusha macho yake angani kutizama alichoelekezwa,
"ndio!! ...eh!..ndiooo jamani! Ni nyota nyingine mzee Otongo...ni nyota nyingine!!!"
"ha! Mama Kadogo kuna mmama ana uchungu wa kujifungua sasa hivi tunavyoongea!! Na ndie atazaa mtoto atakaetuokoa,mama Kadogo tumaini li hai!..huree!!"
"sasa huyo mmama yupo wapi??"
"kijiji cha pili toka ilipo Igesambo,na inabidi tumuwah kabla huyo mama hajadhuriwa na Jeshi la 666 kwani wakiiona tu ile nyota watamtafuta kwa udi na uvumba ili wamtokomeze!!...haraka inuka mama Kadogo,haraka tumuwahi mtoto anekuja!"
haraka mama Kadogo alieanza kupata nyuso yenye mwanga wa matumaini aliinuka na wakaanza kutembea harakaharaka kwa dhumuni la kukusanya nguvu ya kukimbia hapo mbele,kushoto kulia kushoto kulia miguu yao ilipiga maksai wakitafuta kijiji cha pili toka kilipo Igesambo,kijiji cha Utowele,kijiji cha wavuvi na wakulima kama imaanishavyo jina lake,kukifikia kijiji cha Utowele inabidi wavuke mto mkubwa Inguvai,wapite safu ya milima Iramba kisha ndipo watakapokanyaga ardhi ile ya mwanga,ardhi ya tabasamu,ardhi ya mapinduzi na ardhi ya ukombozi,baada ya safari yao kutimiza nusu saa walianza kusikia maporomoko ya maji yaliyowajulisha ya kwamba wapo karibu na mto,mto Inguvai usiopungukiwa na maji misimu yote ya mwaka kutokana na kutokea kwenye safu ya milima Iramba ipokeayo mvua za kutosha zipendeshazo msitu kwa umbijani,
ilihitaji uangalifu mkubwa sana kuvuka mto ule hasa muda ule wa usiku,maji yake yana nguvu mno na yanatosha kabisa kumpeleka mtu mzima hata mnyama yeyote endapo akitumbukizwa.
Walivyowasili kwenye kingo za ule mto mzee Otongo alimshusha chini kadogo,kisha aligeuza sura yake na kumtazama mama Kadogo akisema
"inatubidi tusali mama Kadogo,mungu awe nasi na atushike mkono,atuongoze kuuvuka mto huu,na pia atuongoze tuivuke milima ile...na hata kama mmoja asipofanikiwa isiwe mwisho wa mapambano.umenisikia mama kadogo?"
* * * * *
JE WATAFANIKIWA??
JESHI LA 666 NALO LIMEGUNDUA KUHUSU ILE NYOTA?
USIKOSE! SEHEMU 11 IJAYO...