Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,741
- Thread starter
- #21
666-NYAYO ZA KUZIMU-5-
"mnasema nini??"
"sisi ni mamajusi wa kishetani!..na tumekuja kumlaki mfalme wetu!!.."
"m..m..mfa..mfalme...yu..yu..yupi!"
aliuliza Vero huku akitetemeka,
"mfalme Chernobog,Mungu mweusi!"
Vero macho yalizidi kumtoka,hofu ilichochea ndani yake,alimuangalia yule mtoto aliembeba akamuona anatabasamu!...aliporudisha macho juu,aliona wale wazee watatu tayari washaingia,alisk
ia moyo umepasuka ghafla....hakuvuta tena pumzi,mwishowe akapoteza fahamu.Neno CHERNOBOG lina asili ya urusi,ni
mchanganyiko wa majina mawili,cherno ikimaanisha 'nyeusi' na bog imaanishayo 'mungu',kwahiyo kwa pamoja huza neno 'mungu mweusi' kama anavyoitwa mtoto yule na wale wazee.
Mtoto alichukuliwa kutoka kwenye mikono ya Vero aliepoteza fahamu,kila mzee alimbusu kwenye paji la uso na kuongea maneno fulani yaliyozid kulitunza tabasamu la yule mtoto.
Ghafla alifungua macho yake,hayakua ya binadamu wa kawaida na hata alipopanua mdomo wake,hakua na ulimi wa binadamu
wa kawaida,vyote vilikua ni viungo vya nyoka,tabasamu lenye afya lilichomoza kwenye kila sura ya wale wazee,kwa pamoja wakasema..
"baruch haba chernobog..
Ooh baruch haba"
lugha ya kiebrania(Hebrew) ikimaanisha 'karibu mungu mweusi,ooh karibu!'
..Vero bado fahamu hazikumrudia,hivyo hakupata kushuhudia kilichokua kinajiri,alijiona yu ndani ya giza nene akipepesa macho huku na kule kuutafuta mwanga,akiwa katika harakati hizo mara ghafla alihisi mkono umemgusa begani,haraka aligeuza yake shingo kwa hofu kuangalia ni nani,hakuona kitu,jasho likawa linamtiririka,mwili nao ukawa unatetemeka ilihali na nywele kichwani zikawa zinasisimka,
"wewe nanii???"
sauti iliyoshiba uoga ya Vero iliskika,hakuna sauti yoyote ya kimajibu iliyorudi masikioni mwake zaidi tu ya mwangwi uliomjuza ya kwamba yu ndani ya jengo.
Aliunyanyua mguu wake na kuanza kusogea mbele akiutafuta mlango huku akipata taarifa finyu kuhusu anapokanyaga kutokana na macho yake kushindwa kupambana na giza lile kali,kila alipozidi kusogea mbele alizidi kusisimka na kuhisi hatari zaidi,mguu wake wa kulia ulio mbele ulikanyaga kitu chenye ncha kali,alipiga yowe ya maumivu uliojibiwa na mwangwi mkali uliorudi masikion mwake,nafsi yake ilizidi kushiba hofu kwani alipoangalia kilichomchoma ni nini,hakupata kukiona!..bali tu alishuhudia mguu wake ukimimina damu,hapo ndipo alipoisikia sauti,nzito ya msisitizo na yenye kuogopesha!..
"tazama nao huo ndio utawala unaokuja!..
Utawala wa kiza!...kiza!..kiza na giza!!
Utawala wa nyama na damu!!
UTAWALA WA CHERNOBOG!!!...
Ha! Ha! Ha! Ha! Ha!........."
Vero alipiga makelele ya kiuoga na ghafla alijikuta ameamka toka kwenye usingizi ule mzito!....alipotazama pembeni hakuona kitu zaidi ya kusikia sauti za nyimbo zikitokea nje,alijinyanyua kwa tabu kutokana maumivu aliyokua bado anayo,alijisogeza mpaka mlangoni na kuanza kuchungulia,macho yake yalishuhudia wazee karibia ishirini wakiwa wamevaa mavazi meupe na mekundu wakicheza na kuimba huku wakimrusha rusha yule mtoto juu juu!!..
Baada ya dakika tano lile zoezi lilikoma,sauti ya mzee mmoja aliyekua ameshikilia fimbo yenye alama ya msalaba ikasema..
"wana wa utawala wa kiza huu ni wakati wetu!!"
"amen!"
wakaitikia wale wengine huku wakiinamisha vichwa vyao,
"na tupo hapa kumlaki mfalme atakaetuöngoza mpaka pale tutakapoikamata dunia!!"
"ameen!"
"na kuanzia leo jua halitochomoza,na ni ishara ya kutokua na mipaka kwenye maamuzi!"
"Ameen!"
"ila sadaka ya mtu mmoja haitoshi kabisa kumpokea mfalme wetu,hivyo basi inahtajika nyingine ya ziada!!.."
"ameen!"
"na nendeni mashariki na magharibi,kaskazini na kusini..MKAITWAE!!!!...."
Wale watu walitawanyika huku na huko kwenda kutafuta sadaka kwa ajili ya mapokezi ya mungu wao CHERNOBOG yani 'mungu mweusi',macho yao mekundu,miili yao ya kijivu iliyofunikwa na mavazi meupe na mekundu ilizidi kuchanja mbuga pande zote nane za dunia kwa ajili ya kuifanisha tafrija yao.
Baba Kadogo alizidi kutembea kuelekea mbele,alibakisha umbali usio mrefu sana kukamili
sha safari yake aliyodhamiria,ghafla panga lilimponyoka,akainama akaliokota akaendelea na safari,baada ya hatua mbili tatu panga likamponyoka tena!
Moyo ukaguma,akapata wasiwasi kuhusu ile hali,ila hakujali sana,aliinamisha tena mgongo wake akaliokota,mara ghafla akahisi upepo umempita kwa haraka!
Mwili wake wote ukasisimka!
Ujasiri wake ukaanza kupata mashaka,moyo wake nao taratibu ukaanza kuchanganyia mbio,alihisi joto limepanda,kijasho chembamba kilimshuka,alimeza mate kisha akaendelea kutembea,haukupita tena muda mrefu panga likamponyoka kwa mara ya tatu!
Milio ya hatari ikaanza kuita kichwani mwake,nafsi yake ikamtonya ya kwamba hayuko salama,bila kuuliza mara mbilimbili wala kupoteza muda wa ziada aliinama na kuliokota ganga kisha akaanza kukimbia!!
Hakuruhusu miguu yake isimame wala kupunguza kasi,alikimbia kadiri ya uwezo wake huku akihema juu juu kwa pupa kuitafuta oksjeni,tahamaki alisikia vishindo kwa nyuma vinakuja kwa kasi!
...Baba Kadogo alieanza kuloa uoga na kujuta kwanini hakusikia ile kauli ya mkewe alizidi kuongeza mwendo!
Alikimbia kupita uwezo wa miguu yake,mwishowe kama kiroba cha viazi alidondoka puh!!...panga kule!
Kabla ya kujikusanya na kuinuka,tayari alishazungukwa na watu watatu waliopendezeshwa na mavazi meupe na mekundu!!
Sauti kali ya maumivu ya baba Kadogo iliskika kwa nguvu kutoka msituni
"aaaaaahhh!!!!!!"
kisha tena kukawa kimya,
idadi ikawa ni watu wawili waliokwenda kwa ajili ya sadaka tayari!
* * * * * * * *
mama kadogo alihisi moyo wake umelipuka ghafla!
Alikosa amani,moja kwa moja alihisi kuna jambo baya limechukua nafasi,alitoka kwenye dirisha alipokua anachungulia na kumsubiria mumewe,kiuchovu na kimawazo akaelekea kwenye kiti alipo mama Utopi ambaye bado fahamu hazikumrudia,alikaa kihuzuni huku akishika tama,
"jamani mume wangu,sijui yupo salama huko?..mbona mapigo yangu ya moyo yanaenda mbio hivi?....eh mungu saidia!"
"koh!-koh!"
ghafla kikohozi cha mama Utopi kikaskika!
Haraka mama Kadogo aligeuza yake shingo na kumtazama,
"mama Utopi!"
"ab..bee!"
"vipi mama unajiskiaje?"
"......mmm,mikono inaniuma na miguu pia..inavuta sana!"
alisema mama Utopi huku sura yake ikiakisi maumivu aliyokua nayo,
"usihofu mama,itapoa tu kwani dawa iliyoekwa kwenye hizo bandeji ni kiboko.."
"ahsanteni jamani...ahsanteni sana"
alisema mama Utopi huku akikunja kunja sura kutokana na miale ya maumivu kumpitia,
"haina shida mama,ila samahani sana kwa wale mbwa wetu waliokujeruhi.."
"wala usihofu mwanangu.."
"hivi mama ilikuaje kwani?"
"mh...mama Kadogo,tumekwisha!!"
"tumekwisha? Kivipi yani...sijaelewa!"
"kile kizazi cha nyoka alichotuambia mzee Otongo yule mganga..kimewadia!!"
"eh? Umekionea wapi??"
"mtoto va Vero!..mtoto wa Vero ndie yule....
(kabla hajamalizia alikatishwa na hodi toka mlangoni)
"ngo! Ngo! Ngo!"
"nanii?"
aliuliza mama Kadogo huku macho yakiwatoka kwa uoga,
"mimi Baba Kadogo!"
sauti toka nje iliskika,
mama kadogo alifikiria kidogo,kisha akataka kuinuka ila mama Utopi alimzuia haraka!
Kisha akamuuliza,
"una uhakika huyo ni Baba Kadogo??"
swali lililomstua mama kadogo na kumfanya aanze kutia shaka,
* * * * * * *
je huyo mlangöni ni nani?
USIKOSE SEHEMU 6 IJAYO!