jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Nakubali.Jamaa ni more than JK Govt combine.Siyo siri.Kama ni yeye peke yake anaitumia hiyo id,basi sidanganyi.Mwanakijiji is a movement by himself!
Nakubali.Jamaa ni more than JK Govt combine.Siyo siri.Kama ni yeye peke yake anaitumia hiyo id,basi sidanganyi.Mwanakijiji is a movement by himself!
Fafanua ueleweke hicho kipaji cha wanyama..Marehem Mtemi Senge wa Singida.
Mzee aliyekuwa na kipaji kuhusu wanyama pori mpaka ikasemekana anajuwa lugha za wanyama, he is a legend, ni wangapi humu wanamuelewa?
jamaa wapo weng sannaa,kwa wasaanii,
1. honorable mr 2 aka sugu....
2. mzee jongo
3.bishanga bashaija.
Waandishi ni wengi mno lakini wachahce ni
1. karugendo padri
2.mwanakijiji
3.ulimwengu
4.said kubenea
na weng mnoo
madractrari kwauchache,
1. dr Maro mtaharam wa moyo na former dr wa mkapa
2.Dr Rwakatare na wengine weng..
Stephen Akhwari- Mtanzania aliyekwenda Olympic Mexico 1968. Aliumia baada ya kuanguka na aliendelea na mbio kwa taabu na maumivu makubwa akiingia uwanjani baada ya saa 2 mshindi wa kwanza kupatikana. Amepewa heshima kubwa sana Duniani hadi leo kwa akuli yake 'sikutumwa na nchi yangu kuja kuanza mashindano bali kumaliza'.
Filbert Bayi- Alivunja record ya dunia ya mita 1500 christ church Newzealand na akawika sana dunia kama 'symbol 'ya Tanzani katika vyombo vya habari duniani. Kwa msisimko wake ndio tukawapata akina Gidamas Shahanga, J.Ikangaa n.k.
Jela Mtagwa- Aliongoza kikosi cha Tanzania mashindano ya soka Lagos mwaka 1980. Hatujarudi tena hadi kesho. Alikua na akina Peter Tino, Tenga, Kajole(RIP), Mohamed Salum n.k
Fadhili William (Mtanzania? Mkenya?)- Kutoa kibao kisichochuja hadi leo Malaika.
Prof Shivji- Gwiji la kitaaluma nchini na ughaibuni, mwanaharakati na mtu anayeijali jamii sana.
Ananilea Nkya- Mama mwenye nguvu ya ushawishi wa hoja na inspiration kwa akina Dada.
Hemed bin Jumaa- Kiongozi wa dini aliyekuwa na busara na ushawishi mkubwa sana wa hoja. Aliheshimika sana nje ya nchi kwa uzamifu wake katika mambo ya dini( ulamaa). Aliheshimiwa sana hata na wapinzani wa hoja zake
Rugambwa- Mtanzania wa kwanza kuwa na shahada ya PhD katika mambo ya dini. Alikuwa na mtulivu mwenye busara,asiyependa kuonekana wala makuu. Ameacha mengi katika sekta hasa ya elimu
Mama Kam- Mwalimu aliyethibitishia umma kuwa wasichana hawana tofauti na wavulana kitaaluma kama kutakuwa na uwanja sawa wa kushindana.
Rwegarulila- Mwanataaluma aliyebuni miradi mingi ikiwa ni pamoja na chuo cha maji kilichopewa jina kwa heshima yake.
Prof Thom MMari- Alifungua uwanja wa mawazo huru chuo kikuu, kutoa fursa ya majadiliano bila kujali yanakinzana na maslahi yake au la.
Ndiye makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar aliyeweza kuingia Mkrumah katikati ya zogo la mgomo. Aliheshimiwa sana na wanafunzi. Aliweza kutoka nyumbani kwake kwenda kwenye vikao vya Kunji alipotakiwa bila ulinzi.
itaendelea
Kwa upande wa sanaa kuna mtu aliyejulikana kama George Lilanga.
Huyu alikua na kipaji cha hali ya juu cha uchongaji vinyago, uchoraji na upakaji rangi.
Amekua akipeperusha vyema bendera ya Tanzania kila pembe ya dunia. Na amewahi kupata several
international accolades.
Kwa taarifa zaidi unaweza kucheki GeorgeLilanga.com
marehemu askofu sebastian kolowa, wengine hamkawii kusema naingiza udini, lakini alikuwa ni mtu anaheshimika kwa kada zote na kwa dini zote, viongozi wa serikali pia walimtambua kwa busara zake za kutatua migogoro hasa ule mgogoro wa dayosisi ya meru, ameifanyia makubwa ya kukumbukwa taasisi ya warutheli tanzania.
2.Reginald Mengi
3.Jenerali Ulimwengu
4.Somebody Nyirenda
5.Riz1 JK
6
Ruge wa clouds fm.