50 Greatest Tanzanians (minus politicians)

Candid Scope - Mtunzi wa Honesty to My Country
Kainerugaba Msemakweli - Mlipuaji wa Mafisadi wa Elimu
 
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa..... kweli bange balaa, HAPO ONGEZEA AMOS NYANG'UYE NA RAMA J SAUNIGA

sijawahi kuvuta hata siku moja.
Ila ungesema Mirungi ungeona ningenyamaza kimyaaa na ungenikuta kwenye jukwaa la michezo
 
Dereck bryson, Mbunge wa zamani sana wa wilaya kinondoni. Huyu alikuwa anajua sana kujenga miji na mipya na kuweka huduma muhimu za jamii. Utaona wilaya ya kinondoni karibia miji yake mipya yote ina mitaa, shule za msingi na vituo vya polisi. Kijito Nyama, Mikocheni, mwenge na sinza.

halafu mwingine ni Brown Ngwilulupi: Huyu alikuwa meneja mkuu wa kampuni ya Sigara wakati wa ulanguzi wa siasa. alikomesha magendo ya sigara. alipandishs sana uzalishaji wa sigara na akaanza kusambaza sigala nyingi vijijini vijijini badala ya mijini. Walanguzi wengi walikuja nunua sigara Dar na walipoenda kuziuza vijijini walikuwa tayari sigara nyingi zimejaa na zinauzwa kw abei ya serikali!!!!!

Mwingine: mtu yeyote aliyepinga ujamaa mwaka 1967, Kasanga Tumbo. Ujamaa policy, Umetuletea fedhea barani africa na hatima yake huyo ujamaa ukafa kifo cha haibu!
 
Michael Ngaleku Shirima -mfanyakazi wa zamani wa Shrika la Ndege la Afrika Mashariki, mmoja wa waanzlishi wa Shirika la ndege la Tanzania na mwanzilishi na mmiliki wa Precision Air Services Ltd. Anazo sifa nyingi lakini kubwa ni mnyenyekevu, msikivu, mvumilivu, msomi na msomaji, mwenye upeo na zaidi na mchapakazi. Alinza na ndege ndogo kwa ajili ya kupulizia mimea akawa anenda na wakati akiongeza ndege nyingine na kutafuta teknolojia ya kisasa kwa ajili ya kuendeleza biashara yake. Kampuni imekua na sasa ina thamani ya dola za kimarekani milloni 55. Kampuni imetoa ajira na inaendelea kutoa ajira za moja kwa moja na zisizokuwa za moja kwa moja kupitia makampuni madogomadogo yanayofanya biashara na Precision Air.

Imekuwa ni kati makampuni machache yanayomilikiwa na mzalendo kwa asilimia kubwa ya umiliki kuandikishwa katika soko la mitaji la Dar es Salaam na sasa kampuni inauza shares zake ili Watanzania walio wengi wapate umiliki katika kampuni hii.

Faida ya biashara yake anasaidia watoto walioko ktk mazingira magumu kupitia shirika liitwalo Coronel Ngaleku Children's Centre lililoko Rombo Mkoa wa Kilimanjaro
 
Jina ambalo ningeweza kuliweka kama maarufu ni la bwana David Mwaibula, jamaa alisimamia suala la usafiri dsm na lilifanikiwa na sasa design yake inatumika nchi nzima (katika miji mikubwa) leo tunaona magari ya abiria (daladala, express, vifodi nk) vina alama za kutambulisha vinaenda wapi na makonda na madereva wanavaa suti
 
Chief Mkwawa. Alipigana vita na wajerumani kwa silaha asilia na aliwauwa wanajeshi wajerumani waliokuwa na silaha bora. Alikimaliza kikosi chote cha wajerumani. Walimshinda waliporudi mara ya pili na alijiua mwenyewe. hawakumpata.

Muadhama Kardinari Lugambwa. Cardinari wa kwanza Muafrika.

Julius Mwasanyage. Mwafrika wa kwanza kupata degree ya uchumi.

Padre Alanus OSB. Alihamasisha wananchi kujenga barabara km 28 kwa kutumia majembe, sululu na moto kwa kupasulia mawe. 70,s
 
Filbert Bayi, alituweka katika record duniani kwa miaka mingi tu kabla record yake haijavunjwa, enzi zake kweli alitutoa kimaso maso, tusimuache !
 
Mtemi Majebele, kosa alilo fanya ni kuwambia wakoloni wasimpe nyerere nchi. Mchonga alivyoshika nchi akamwacha mzee wa watu afe njaa.
 
tupo wengi japokuwa sio vizuri kujitaja lakini nimo naitwa Lofe Lameck. Nimefanya mengi sana nashangaa si enziwi
 
Hamis Gaga (gagarino) - uchezaji wake wa mpira uliibua watoto wengi mtaa kupenda mpira

Shaban Mazinge - comperative religions studies champion in Tanzania

Said Bakhresa - Azam product serves the poorest people in Tanzania...mlipa kodi mkubwa nchini (mapinduzi katika viwanda)

Mohamed Said - Mtetezi wa wanyonge na mwandishi mashuhuri wa vitabu Tanzania
 
nadhani mleta thread angeleta criteria... coz tulishawahi kusikia wanawake nao walikua na achievement awards zao ambazo weledi engi hawakuzipenda

without criteria mie hata sara simbaulanga na maumba ntawaweka humo
 
Hamis Gaga (gagarino) - uchezaji wake wa mpira uliibua watoto wengi mtaa kupenda mpira

Shaban Mazinge - comperative religions studies champion in Tanzania

Said Bakhresa - Azam product serves the poorest people in Tanzania...mlipa kodi mkubwa nchini (mapinduzi katika viwanda)

Mohamed Said - Mtetezi wa wanyonge na mwandishi mashuhuri wa vitabu Tanzania
We si mdini kweli wewe?Ama ni just a coincidence?Hapo kwa Gagarino nimekubali tho.
 
Jina ambalo ningeweza kuliweka kama maarufu ni la bwana David Mwaibula, jamaa alisimamia suala la usafiri dsm na lilifanikiwa na sasa design yake inatumika nchi nzima (katika miji mikubwa) leo tunaona magari ya abiria (daladala, express, vifodi nk) vina alama za kutambulisha vinaenda wapi na makonda na madereva wanavaa suti
Kweli tuna safari ndefu sana wabongo.Yani hayo ni majukumu yao waliyotakiwa wayafanye toka zamani sana.Lakini kutokana na ubovu wetu,basi hivi ndo viwango vyetu,hakuna muujiza wowote he was just doing his work the way he was supposed to. Sasa hata hili nalo tumpe ugreatest?Naona kwasababu labda umeguswa sana na hayo aliyoyafanya kutokana na adha ya usafiri.Hivyo sikulaumu coz ni tatizo sugu ambalo umeona/pata relief.Otherwise hakuna cha ajabu alichofanya.Na pia "umaarufu
' siyo "ugreat" so maybe siyo kosa lako.
 
Dereck bryson, Mbunge wa zamani sana wa wilaya kinondoni. Huyu alikuwa anajua sana kujenga miji na mipya na kuweka huduma muhimu za jamii. Utaona wilaya ya kinondoni karibia miji yake mipya yote ina mitaa, shule za msingi na vituo vya polisi. Kijito Nyama, Mikocheni, mwenge na sinza.

halafu mwingine ni Brown Ngwilulupi: Huyu alikuwa meneja mkuu wa kampuni ya Sigara wakati wa ulanguzi wa siasa. alikomesha magendo ya sigara. alipandishs sana uzalishaji wa sigara na akaanza kusambaza sigala nyingi vijijini vijijini badala ya mijini. Walanguzi wengi walikuja nunua sigara Dar na walipoenda kuziuza vijijini walikuwa tayari sigara nyingi zimejaa na zinauzwa kw abei ya serikali!!!!!

Mwingine: mtu yeyote aliyepinga ujamaa mwaka 1967, Kasanga Tumbo. Ujamaa policy, Umetuletea fedhea barani africa na hatima yake huyo ujamaa ukafa kifo cha haibu!

i will go for the true prof maji marefu!jamaa anachomoa majini balaa!
 
i will go for the true prof maji marefu!jamaa anachomoa majini balaa!
Humu ni home of great thinkers lakini makapi yamo.Hakuna kigezo cha kuchuja wakati wa kujiunga,hivyo kama unataka kuwa great thinker basi jiunge na JF tu and you become one?Teh teh teh!Nadhani ili kuwe na great thinkers,ni lazima kuwe na watu kama nyie,otherwise tungepima vipi?Te teh teh!Sina mbavu miye.Kuondoa majini ni msaada mkubwa sana kwa taifa.
 
Kuna yule Stephen Akwari, sijui kama nimelipatia jina lake. Aliyeumia wakati akikimbia marathon, akamaliza muda mrefu sana baada ya mtu wa mwisho kumaliza. Alipoulizwa kwa nini aliendelea kushindana baada ya kuumia, akasema nchi yake imemtuma kumaliza mashindano

John Stephen Akhwari....cheki hapa upate undani wake zaidi.
John Stephen Akwani - Olimpiadas Mexico 68 - YouTube
Finish the Race ~ personal story of courage - YouTube
John Stephen Akhwari - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom