Marehem Mtemi Senge wa Singida.
Mzee aliyekuwa na kipaji kuhusu wanyama pori mpaka ikasemekana anajuwa lugha za wanyama, he is a legend, ni wangapi humu wanamuelewa?
Kwanza kabisa ni vyema kuanza na waasisi wa ukombozi ambao ni watemi na machifu kama wafuatao ambao tumebeba maana nyingi sana toka kwao kwa mfano ngome au ofisi ya Mtemi mirambo wa Tabora ilijulikana kama IKULU yaani KUBWA ama KUU.Ndio mpaka sasa tunatumia jina hilo kutamka ofisi kuu ya Nchi yetu hivyo hatuwezi kusita kuwatambua kwanza waasisi wa movement ya ukombozi wetu pasipo kuwataja watemi na majemadali wao walioasisi movement hizo
1: Mtemi Mirambo- Wanyamwezi-Tabora
2: Mtemi Mwinyugumba Wahehe- Iringa
3: Mtemi Merere Usangu
4: Mtemi Machemba Wayao
5: Mtemi Isike Wanyamwezi Tabora
6: Mtemi Mkwawa Munyigumba Mufwimi -Wahehe Iringa
7: Mtemi Kinjekitile - Wamatumbi Kilwa
8:Chifu Kidaha Makwaia - Wasukuma Shinyanga
9: Chifu Abdiel shangali Uchagani-Hai Kilimanjaro
10:Chifu Admu sapi Uhehe -Iringa
11:Erasto Mange'enya
12: Ivo Mhaiki
13: Mwami Thereza
14: Thomas Marealle
Viongozi kama
1: Ali Ponsa
2: Ally Sykes
3: Abdul Sykes
4: Paul Boman
5: Yoseph Saadan
6: A.Kandoro
7: Said A.Maswanya
8: Agnes G.Sahani
9: P.Kunnambi
10: i.M.Bhoke-Munanka
11: Elias Amos Kisenge
Viongozi wa Mkutano Mkuu wa TAA uliofanyika chini ya Mwalimu JK Nyerere Julai 7th hadi 9th 1954
Walianza wakiwa zaidi ya kumi na saba lakini waliomaliza mkutano huo na kuanzisha TANU ni kumi na saba [17] tu.
1: Jk Nyerere - Rais
2: Geramano Pacha- Jimbo la Magaharibi
3: Yoseph Kimalando- Jimbo la Kaskazini
4: Yafati Kirilo- Jimbo la Kaskazini
5: C.O.Milinga- Jimbo la Kaskazini
6: Abubakari Ilanga- Jimbo la Ziwa
7: L.B Makaranga - Jimbo la Ziwa
8: Saadani A Kandoro Jimbo la Ziwa
9: S.M Kitwana Jimbo la ziwa
10: Kisunguta Gabara Jimbo la Ziwa
11: Tewa Said Tewa Jimbo la Ziwa
12: Dosa A Aziz Jimbo la Mashariki
13: Abdul Sykes Jimbo la Mashariki
14: Chief Patrick Kunambi Jimbo la Mashariki
15: Yoseph K.Bantu Jimbo la Mashariki
16: Ally Sykes Jimbo la Mashariki
17: Yohana Rupia Jimbo la Mashariki
Kuna Wadau kama Mwinyimvua Kingaru na Mohamedi Magota wallingia matatizoni na Serikali ya Wakoloni huko Morogoro baada ya kukamatwa Ruvu kwenye garimoshi wakiwa na kadi 2500 za TANU mwaka 1954.Walikamatwa wakapelekwa kituo kidogo cha polisi na kuchojolewa nguo zote, wakaludishwa Dar es salaam kwa escort ya magali mawili chini ya ulinzi mkali wa Serikali ya Wakoloni.Wamefika dar wakakuta na kaka yake Mwinyimvua, Ali Kingalu naye alikuwa ametiwa nguvuni kuungwa kwenye tukiola kisiasa la wapiganaji hao wa wakati huo.
Walipelekwa Mahakaman saa 4 usiku wakasomewa mashitaka na hakimu mzungu el maalufu kama Kikono zama hizo.Kwa kuwa Mkono wa Mzungu huyo ulikuwa umekatika.Makosa ya wapiganaji hao yalikuwa kama ifuatavyo.
1: Mnataka Kuua Wazungu [Wayuronodi]
2: Mnawatisha watu na kuwafanya waingie TANU hata kama hawapendi
3:Mnawalazimisha watu kuingia TANU
4: Mmewachochea watu wakatae kilimo cha ngazi -hata kusababisha polisi kuingia na kumua mtu mmoja kwa risasi huko Matombo
Wakapelekwa rumande Dodoma siku hiyo hiyo wakiwa watu watano
1: Mwinyimvua Kingaru
2: Ali Kingaru
3: Mohamed Hussein Magota
4: Mohamed Senei
5: Mohamed Minchumu
Walifungwa miaka miwili,lakini baada ya rufaa kwa kutumia mwanasheria mwenye asili ya asia Baria mkazi wa morogoro Mohamed Minchumu alitoka baada ya kuonekana hana hatia na ghalama za kesi hiyo zilikuwa ni shilingi elfu tatu [3000] amabzo zilitokana na michango ya wanachama wa TAUNU. Waliosalia wanne walibanwa zaidi na kuongezewa kifungo cha kuhamishwa toka kwao morogor0o na kupelekwa gereza la Biharamulo baada ya kifungo chao waliamlishwa kubakia Kizuizini ambako walipelekewa wake zao na kuamliwa kiuishi huko toka mwak 1956 mpaka mwaka 1958 siku moja baada ya mkutano mkku wa TANU hapo Juu.
Mikoa ya Kanda ya ziwa nayo ilikuwa na wapiganaji kuanzia miaka ya 1950 watu kama
1: Mtemi Abdalah Musa Nzera wa Msalala
2:Wiliam Ichwekeleze wa Geita [Mpinga Siasa ya Mseto Ulioanzishwa na wakoloni 1958]
3: Ali Chifunda Lukuba [Alitoa sharti kuwa ili akubali mseto basi aozwe binti wa mhindi maalufu wakti huo Selani Manji Mzee huyo alikuwa na umri wa Miaka 70]
4: Hezron Makaranga Mpandachalo-Buchosa [Mpigania uhuru Mashuhuri wa Kanda ya Ziwa]
5: Robert Bupima- Bukokwa
6: Mtemi Abdalah Nzera
7:Yacob Mikomangwa
8: Zebron Mikomangwa
9: Mashauri Kabadi
10: Yoseph Wangaruke
11:Rafael Mataruma
12: Nyambagali Luhunje
13: Kaimu Mtemi Malindi
14: Kulwa athumani
15: Katemi Ngalabushi
16: Dotto Athumani
15: Wapindoshi Fele
16: Ngereja Ndindilo
17:Abeli Masasi
18: Andrew
19: Ng'wahale Athumani
20: Nyanda Nkanda
21: Ngereja Chamanja
22: Msabila Shilinde
23: William Masota Bunuma [Alikaimu nafasi ya Mpandachalo wakati yuko kifungoni]
24: Augustin Madaha
25: Agness Gigwa Sahani [Mweneza TANU kwa Kanda ya Ziwa mwaka 1955]
26: Elias Amos Kisenge [Ktaibu Mkuu wa Chama cha TANU mwaka 1958]
MATOKEO YA UCHAGUZI MWAKA 1958 kuanzia tarehe 9:02:-17:02:1959
Jina Jimbo Chama Utaifa
1: J.B.M Mwakangale Nyanda za Juu Tanu Mwafrika
2: J.Senkei Nyandaz za Juu Tanu Mwafrika [Binafsi]
3: W.K Mwanjinsi Nyanda za Juu Tanu Mwfrika
4: A.S.Bajaj Nyanda za Juu Tanu Mwasia
5: R.K Manji Nyanda za Juu Tanu Mwasia
6: Bi M Cheshamu Nyanda za Juu Tanu Mzungu
7: A.S. Fundikira Magharibi Tanu Mwafrika
8: M.M.Rantasi Magharibi Tanu Mwafrika
9: G.P. Kunambi Masharikii Tanu Mwafrika
10: A.H Jamali Mashariki Tanu Mwasia
11: J.Keto Tanga Tanu Mwafrika
12: B..Krishiina Tanga Tanu Mwasia
13: S.K. Eliufoo Kaskazini Tanu Mwafrika
14: S.Mustafa Kaskazini Tanu Mwasia
15: D.M.N Braison Kaskazini Tanu Mzungu
16: R.M.Kawawa Dar es Salaam Tanu Mwafrika
17: K.K.Javeri Dar es Salaam Tanu Mwasia
18: L.N.Sijaona Kusini Tanu Mwafrika
19: Dk DL Stelling Kusini Tanu Mzungu
20: Paul Boman Ziwa Mashariki Tanu Mwafrika
21: C.G. Kahama Ziwa Magharibi Tanu Mwafrika
22: N.K.Laksiman Ziwa Magharibi Tanu Mwasia
23: B.C.Jonson Ziwa Magharibi Tanu Mwafrika
24: M.M Kihere Kati Tanu Mwafrika
25: A.Kasumu kati Tanu Mwasia
26: Dk H.W.Hana Kati Tanu Mwasia
Kutokana na uchaguzi huu Tanganyika ilipata mawaziri katika Serikali ya wakoloni waafrika wafuatao
1: S.N. Eliufoo kuwa waziri wa Afya
2: Abdalaah Fundikira waziri wa Ardhi na Upimaji
3: C.G.Kahama waziri wa Ushirika
4: Derek Braison [Mzungu kwa tiketi ya TANU] waziri wa Madini na Biashara
5: Amiri Jamal [Mwasia] waziri wa Miji,Mitaa na Kazi