30 - 36 years old: An Official Thread

Nipo katika umri huo, yapo ambayo nimetimiza na lipo ambalo sijatimiza,
Bado sijakata tamaa naendelea kumuomba Mola anijalie nitimize
 
I'm in that age. Ni umri wa pressure hasa Kama uoiokuwa nao au kusoma nao wengi wamefanikiwa. Pressure ya ndugu inaongezeka...Kama hujaoa wanataka uoe kwa haraka...hawajali struggle yako bali wanataka mafanikio yako..Kama una partiner naye anataka uharakishe mpande madhabahuni awe safe....kama upo nyumbani ni hatari zaidi.....

Wanaosema life begins at 40 huwaamini tena...wakati mwingine unaona hata ibada haziendi...it's mid life crisis ya hatari...Ila mapambano yaendeleee
 
Huo umri ni sawa umeshakosa magoli mengi sana, sasa imefika dk 95 umepewa penalt halafu ukimwangalia keeper ni kama kaenea kwenye goal galafu kama anarukaruka hivi kuziba hata vipengo vidogo.
Haha hatari
 
Tangu nifikishe miaka 30 naona mabadiliko ya mwili na roho

-nilikuwa siwezi kulala mchana saivi nalala mda wowote

-nilikuwa siwezi kukaa sehem moja kwa mda mrefu, saivi nakaa.

Na mengine mengi
Sure man, kabisaa on point, huu umri ni wa aina yake
 
Hatari boss tupambane tu
 
Usiji stress bro, kuwa na mtoto pale utakapokuwa tayari, usiwe pressured na umri ila uwe triggered,
 
Hapo naweza kukuelewa Sasa Mkuu, pambana,usichoke, mzee wangu katoboa Ana Miaka 40,kabla ya hapo ilikua ile vijana wanaita Apache alolo Yani hakuna kitu
Mshahara wake wakati Ana Miaka 30 ilikuwa ni laki 7 take home!!! We utatoboa tu Mkuu
Alitoboa at 40, coz alipambana from 20s to 30s, big up to your pops
 
Shemeji pole Sana,Cha muhimu ni kimoja tu,uzeeni tusiishi kwa tabu,Kuna member Fulani humu aliwahi kusema ni heri ataabike sahivi ila uzeeni aishi vizuri
Cha msingi tukifikisha 50 tusiwaze pesa ya kula Wala kulipia Kodi
Sure tupambane na tusave b4 40s, ili ikifika hizo 40s na 50s, tusiishi kwa pressure saaana
 
Sure boss. Pressure iko juu, ila hakuna kukata tamaa

Wanaosema Life begins at 40, hawakosei lakini wana mis interpret

Life begins at 40, after what you prepared at 20s n 30s.

Sasa chezea life in your 20s 30s alafu upambane kuishi at 40, yani hio kati ya watu 10 ni moja tu atatusua.
 
Noma sana!
 
Wewe unavyo?
 
Samehe tu maana huenda dharau zake zilikuongezea nguvu kupambana lazima uliwaza usiku na mchana.
Ukifanikiwa washukuru waliokusupport ila washukuru zaidi haters maana ndo wanakuongezea kujituma.
 
Ni mwongozo tu na maoni, ukisoma hivi unaangalia ni wapi ulipo kuyokana na maoni yake, nini ufanye kama hujafanya ili walau ufike stage fulani katika maisha.

Ni kweli maisha hayana kanuni, lakini kuna namna ukienda tofauti utajishangaa mwenyewe badae.

Ni vizuri kukumbushana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…