2012 sijawahi kucheka zaidi ya hivi

2012 sijawahi kucheka zaidi ya hivi

Njemba ivaa midabwada inakatisha barabara mara inakuja vx anaendesha mwanamke anamgonga(utaona mchiriz wa mchuzi wa nyanya mdomoni),baada ya hapo anapelekwa zahanati akitoka hapo dem anampenda Njemba anakuwa tajiri...
Title yake Love Doesn't Ask Why..!!
 
Majambazi kwenye movie uwa ni walewale mfano kuna jamaa anaitwa 'Ben' na dogo mwingine black kajazia mwili.
 
Uanza na matangazo mengi ya biashara karibia robo saa nzima wanatangaza filamu zilizotengenezwa na studio husika.

Jamaa anasema yupo nyumbani kwake lakini kiunoni amefunga taulo imeandikwa "Bondeni Guest House"

Mwanamke yupo kitandani amelala usiku wa manane na mumewe lakini amevaa kitop na jeans, mdomoni lip stick,machoni wanja vimeshaini! Mume ana pensi na Tshit mkononi ana saa kali!

Wachezaji hawatumii taswira zao halisi ikiwemo sauti za kubana pua, mavazi ya kukodisha au kuazima nk.

Msanii anapiga picha akiwa amesimama kwenye mkoko (usafiri) mkali ambao kwenye tamthilia au filamu nzima humuoni akiendesha..

Jamaa ana act yeye ni mkuu wa kituo cha polisi lakini anamwita "afande" askari aliye chini yake ("yupo wapi afande Jack aje nimtume eneo la tukio)

Binti ana act "u secretary" lakini haonekani akitumia hata mara moja kompyuta iliyo mbele yake.

Mtu ana act yupo ofisini ni Boss lakini pembeni yake unaona Kabati la Nguo
 
part one na two zinatoka at the same time.

wataspend alot.of time baharini afu waende dinner huku hawaongei.

hawawez kuongea maneno kumi.bila hata matatu ya kingereza na mara nyngi cha kuunga.

Nakubali, tena kiingereza cha chonya kina nafuu....!
 
hahahahhah mkuu umeua!!!!
Uanza na matangazo mengi ya biashara karibia robo saa nzima wanatangaza filamu zilizotengenezwa na studio husika.

Jamaa anasema yupo nyumbani kwake lakini kiunoni amefunga taulo imeandikwa "Bondeni Guest House"

Mwanamke yupo kitandani amelala usiku wa manane na mumewe lakini amevaa kitop na jeans, mdomoni lip stick,machoni wanja vimeshaini! Mume ana pensi na Tshit mkononi ana saa kali!

Wachezaji hawatumii taswira zao halisi ikiwemo sauti za kubana pua, mavazi ya kukodisha au kuazima nk.

Msanii anapiga picha akiwa amesimama kwenye mkoko (usafiri) mkali ambao kwenye tamthilia au filamu nzima humuoni akiendesha..

Jamaa ana act yeye ni mkuu wa kituo cha polisi lakini anamwita "afande" askari aliye chini yake ("yupo wapi afande Jack aje nimtume eneo la tukio)

Binti ana act "u secretary" lakini haonekani akitumia hata mara moja kompyuta iliyo mbele yake.

Mtu ana act yupo ofisini ni Boss lakini pembeni yake unaona Kabati la Nguo
 
no comment nisije kukosa tenda za ku act sebuleni kwangu ,ila wakiondoka wanaacha uchafu hao utadhani chekechea
 
mwanaume anampgia simu mpenzi wake aliyeko disco, disco panaonekana usiku lakini nyumbani aliko mwanaume panaonekana mchana jua kaliiii!!!!! BONGO MOVIE
 
Kuna movie ya "Valentine Day"ilitangazwa sana nikashawishika kuitazama kuna sehem dada kaagiza juice ya passion kaletewa fanta hotelini na wala hakushtuka wala kulalamika kuwa pia ukiona movie sitting room kuna flame za picha ambazo sio za wahusika wa hiyo movie (mara nyingi huwa ni za wenye nyumba halisi) basi ujue ni hiyo ni bongo movie .
 
utaona mwigizaji anaangalia kamera ili ahakikishe anachukuliwa picha!
bongo movies, bongo lala, bongo music, taaluma isiyo vigezo na elimu haitumiki!
 
Mara nyingi majina ya movies hayana uhusiano na stories zenyewe, isipokuwa wanakurupuka kutumia jina maarufu kwa kipindi husika.
Fikiria majina ya movie zilizotoka kama facebook, vuvuzela, majanga,Gongolamboto (baada ya yale mabomu).
Subiri majina ya movies mpya kama vile king'amuzi, digital, analogy, katiba mpya etc.
Pia kuna title za movies ambazo nilicheka nilipozione (nimewahi ona title moja ya filamu inaitwa Killings of the camps-wakaitafsiri mauaji kambini...duh)
 
Kuanzia mwanzo wa filamu hadi mwisho sterling au muhusika mkuu ,kavaa mashati mawili na suruali moja tu

Kubadilisha nguo kunategemeana na hadithi, hubadilishi kwa kujifurahisha tu,
hebu kama huelewi ni bora ukakaa kimya kuliko kujidharirisha. Nani alikwambia
kwenye movie ni sehemu ya fashion show?...
 
kuna moja inaitwa basilisa, clouds kaigiza kama jini. amevaa jinsi , kavaa jezi kama ya wacheza basketi, saa kali na makeup za kutosha.
 
utamuona mtu akipigwa risasi ya tumbo ye anashika bega,dah sijuwi mahusiano yakwapi hapo,basi ujuwe ni bongoland filamu
 
Back
Top Bottom