"2011" – What a year it has been!!! KARIBU 2012....


AD nyumba ndogo naiogopa kama ukoma. Sina mpango wa kuiongeza nyumba ndogo zaidi ya kupigania mafanikio ya nyumba kubwa na watoto wangu. Hiyo itakupa raha ya kuitwa baba na sio dingi au baba mlevi.
Vile vile ukipigania maendeleo ya familia yako unapata ile raha ya kuona watoto wanakuwa wakiwa na raha ya kuwa na baba anayewajali

Pia nina mpango wa kuongeza zaidi upendo kwao wajione nao walistahili kuwepo duniani kwa wakati muafaka.

Kushikamana na Mungu zaidi na zaidi ni malengo yangu ya mwaka huu unaokuja pia.

RR naona alikuwa anahisi bado asubuhi haijafika wakati ilikuwa kabisa ndege washaanza kuwaamsha watu
 
ahahaaa sis bwana kwanza thax kwa maombi yako kuhusu kummaintain huyu switheart kwa elimu yenu ya hapa jf kiukweli imenisaidia sana mahusiano yetu kuwa mazuri
kuhusu kufunga ndoa na mimba kwa sasa siwezi kuzungumzia ilo nitakupm
 


Tulizo hili lilikua DARASA tosha!! lol (Kweli tena)


Thanks for the acknoweledgement Tulizo... Appreciated. I am sorry i keep rubbing this in.... BUT with your logical outlook katika maisha naamini kabisa your wife is one lucky lady na kwamba maisha na ndoa na familia yasonga na yataendelea kusonga hadi kufikia pale ambapo Lizzy karusha Uzi... (ujanani hadi uzeeni...lol). Mafanikio yako ni mazuri, nimeyapenda na nakuombea kwa Maanani na 2012 iwe hivo hivo.....


Matarajio yako yamesimama..... Naona am the only one hafikirii kujiiunua kwa mtindo wa Kilimo. Umemsoma SMU, naona you guys have the sama plans for 2012 it is beta mchange ideas kidogo, hamuwezi jua mtabenefit vipi from one another....

Genuinely sijawahi kufikiria kua hata wewe na mpenzi wa Ulanzi....lol... Nikaribishe siku moja bana. ila mengine am not surprised nor it seems I was not wrong. A family man, a soccer person and a Man of responsibilities. My hope ni kua hua wayatimiza hasa the way I think....

Thank you for sharing.... Na looking forward kua woote JF next year....
 
Shem langu la ukweli hongera kwa mafanikio.... na hiyo ya kutaka kupata ujauzito, sijamsikia hommie akilizungumza.....unataka kumchakachua?

Kwangu mie natamani huu mwaka uishe haraka iwezekanavyo. Mazuri ni machachekuliko mabaya khaa!

Mazuri:
Sijapata misukosuko yoyote katika maisha yangu.... nyumbani, JF, kazini, kwa ndugu, jamaa, jirani na marafiki
Nimeongeza idadi ya marafiki (ukiwemo wewe ADI wa ukweli)
Sijachangia posti hata moja kwenye jukwaa la mastress
Sijapigwa BAN wala kupewa onyo
Nimeshuhudia binti yangu Matesha akipata sakramenti ya komunyo ya kwanza
Nimekaa na wazazi wangu kwa wiki tatu mfululizo nikiwa na binti yangu Mamshanga(sijawahi kufanya hivyo tangu nianze maisha ya kujitegemea)
Nimekutana LIVE na JF members - niliokuwa nawajua through keyboard (wazee waA-Town).... Mzee wa Rula, Lily Flower, Sweetlady, Blaki Womani, Filipo,Saharavoice, Liverpool, Preta, Pakajimmy, Wiselady na kama kawaida wazee wa Dar na vitongoji vyake, na nimeendelea kuwa na uhusiano nao wa karibu kiasi chakukutana almost kila weekend pareeeparee pa ukweee... - GY, Teamo, MTM,MwanajamiiOne,The Finest, Askofu, Maty, Kaizer, Bigirita, Memo, bombu, RR, LD,Maty, Maskini Jeuri, Fidel80, Manda, Carmel na wengineo.

Mabaya….Dah!
Misiba kibao yaani ya kutisha…. Binamu yangu, jirani yanguna rafiki yangu mwana JF mwenzetu Chetuntu kuwataja wachache (Mungu aendelekuwarehemu)
Kibanda changu nachoishi kuwaka moto (hii sitokaa niisahau)ahsante Mungu, majirani, mchanga na maji…. Sijui ningekuwa wapi leo.
Baba yangu kupata ugonjwa ghafla uliompelekea mpaka sasakutorudi katika hali ya kawaida
Kaimu kangu ka mchina kuharibika

Hivi…. Ngoja niishie hapa kwanza, babu wa watu nsije mwagamichozi mbele ya screen… watanicheka wajukuu!
 
Any man can be a Father ,ILA WEWE NI BABA BORA MKUU

 
mkuu mbona hapo kwa colour hujatushirikisha ila pole sana na ashukuriwe mwenyezi mungu kwa kukunusuru mkuu

 
mkuu mbona hapo kwa colour hujatushirikisha ila pole sana na ashukuriwe mwenyezi mungu kwa kukunusuru mkuu

Ahsante mpendwa..........

Ningewashirikisha kuja kuuzima moto au? Lilikuwa ni tukio ambalo sitokaa nilisahau.... Nakumbuka kumpitisha Matesha wangu katikati ya Moto! Damn!
 
ahsante mpendwa..........

Ningewashirikisha kuja kuuzima moto au? Lilikuwa ni tukio ambalo sitokaa nilisahau.... Nakumbuka kumpitisha matesha wangu katikati ya moto! Damn!
aha kukupa moyo na kukutia moyo kwa maswaibu hayo bwana aunt wangu matesha jamani loh mungu mkubwa
 


Snowball ni furaha kwangu kwamba nimekufukunyua uko ulipo kua.... Siku nying bana hivo happy to see you hapa.

Nafurahi zaidi kua 2011 has been awesome for you and best yet have been fully fulfilled plans..... HONGERA. Ni wachache kwa kweli wanaweza sema hivo....

Nikija upande wako wa Relationships za long Distance.... We are in the same boat. Sina mengi yakusema.... ila tu yataka moyo (na yataka uwe really good at E-sex lol). But nakutakia kia la kheri katika the relationship in question... And am not surprised about the re-thinking part.... Enways BEST of Luck...

Mzima lakini?
 


R' misimamo yako kwa kweli hunikosha.... And on behalf of your wife and Family I declare kwamba I am PROUD of you. Kikubwa I really hope hua wafanikisha as I understand hapa Jamvini.... Hua wanifurahisha saaana. NAOMBA umpe hilo darasa ODM na wengine woote (nina bahati kweli Sweetie Kaizer hayupo hivo...lol).

You are a Great Dad and hubby it seems.... Jamii yetu hilo kundi lapungua kila siku! Sad.... just hoping for the better....
 
ahahaaa sis bwana kwanza thax kwa maombi yako kuhusu kummaintain huyu switheart kwa elimu yenu ya hapa jf kiukweli imenisaidia sana mahusiano yetu kuwa mazuri
kuhusu kufunga ndoa na mimba kwa sasa siwezi kuzungumzia ilo nitakupm



hahahaha.... Me like the sound of that sisy.....:gossip:
 

Thank you so much dear
Babu ujumbe utamfikia tuu ipo siku yake.
Asante sana sana.
Na lengo jingine kubwa ni kwa PA kufunga ndoa maana duh hii biashara yake ya kuzunguka kwa sasa inatosha.
BTW nampa pole sana Babu Kwa yaliyomkuta. Mradi uzima ukiwepo Mungu ana mipango yake. Pole sana Babu
 
tel him bwana
 
thank you dear.
Nakuombea sana upate mafanikio mema katika mwaka ujao.
Asante sana sana.
asante kwa maombi yako mkuu
naamini mungu ataendelea kunisaidia maana ni mwema always
i wish huyu honey wangu awe kama wewe
 
2011:mwaka wa huzuni sana kwangu, nimepoteza marafiki wengi wa karibu kuliko miaka yote iliyopita( Mungu awarehemu wote)


Namshukuru mungu bado nahema! Mafanikio ni mengi, malengo mengi nilojiwekea yametimia kwa uwezo wa mungu...machache sana yamesalia.
 
hahahaha.... Me like the sound of that sisy.....:gossip:
niliwish kufanya mambo mengi before that big day ila my fellow honey ana haraka it seems like haniamini ila i wish ningepewa sometime
ila kama ujuavo mimi mwanamke shosti ukikataa sana yanaweza kukukuta makubwa ila namini all in all mungu atanisaidia
 
asante kwa maombi yako mkuu
naamini mungu ataendelea kunisaidia maana ni mwema always
i wish huyu honey wangu awe kama wewe
Nakuombea sana sana na naamini utafanikiwa sana
Usiwe na shaka maana Mungu ni mwema siku zote hawezi kukutupa.
Asante sana dear
 
….nakuombea kwa Maanani na 2012 iwe hivo hivo...........
Thanks AshaDii.. Pia Tuko pamoja katika maombi kwa Mola atuongoze vijana wake hasa wote wa hapa jamvini..

...Genuinely sijawahi kufikiria kua hata wewe ni mpenzi wa Ulanzi... ....
Ha ha ha ..huwa nakunywa ulanzi kama kinywaji na sio kama sumu au dawa ya Stress ambayo haikawii kumbadili Bint muuza ulanzi toka kuwa “ugly betty” hadi kuwa “miss world”..

… a soccer person …....
Yes, ila timu yenyewe ina wachezaji wachache (watoto wangu tu) na wengine bado wako kindergarten…Ila tuko kwenye mazungumzo ya kumsajili mama watoto..ili ajiunge nasi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…