shem langu la ukweli hongera kwa mafanikio.... Na hiyo ya kutaka kupata ujauzito, sijamsikia hommie akilizungumza.....unataka kumchakachua?
Kwangu mie natamani huu mwaka uishe haraka iwezekanavyo. Mazuri ni machachekuliko mabaya khaa!
Mazuri:
Sijapata misukosuko yoyote katika maisha yangu.... Nyumbani, jf, kazini, kwa ndugu, jamaa, jirani na marafiki
nimeongeza idadi ya marafiki (ukiwemo wewe adi wa ukweli)
sijachangia posti hata moja kwenye jukwaa la mastress
sijapigwa ban wala kupewa onyo
nimeshuhudia binti yangu matesha akipata sakramenti ya komunyo ya kwanza
nimekaa na wazazi wangu kwa wiki tatu mfululizo nikiwa na binti yangu mamshanga(sijawahi kufanya hivyo tangu nianze maisha ya kujitegemea)
nimekutana live na jf members - niliokuwa nawajua through keyboard (wazee waa-town).... Mzee wa rula, lily flower, sweetlady, blaki womani, filipo,saharavoice, liverpool, preta, pakajimmy, wiselady na kama kawaida wazee wa dar na vitongoji vyake, na nimeendelea kuwa na uhusiano nao wa karibu kiasi chakukutana almost kila weekend pareeeparee pa ukweee... - gy, teamo, mtm,mwanajamiione,the finest, askofu, maty, kaizer, bigirita, memo, bombu, rr, ld,maty, maskini jeuri, fidel80, manda, carmel na wengineo.
Mabaya
.dah!
Misiba kibao yaani ya kutisha
. Binamu yangu, jirani yanguna rafiki yangu mwana jf mwenzetu chetuntu kuwataja wachache (mungu aendelekuwarehemu)
kibanda changu nachoishi kuwaka moto (hii sitokaa niisahau)ahsante mungu, majirani, mchanga na maji
. Sijui ningekuwa wapi leo.
baba yangu kupata ugonjwa ghafla uliompelekea mpaka sasakutorudi katika hali ya kawaida
kaimu kangu ka mchina kuharibika
hivi
. Ngoja niishie hapa kwanza, babu wa watu nsije mwagamichozi mbele ya screen
watanicheka wajukuu!