2011 UDSM nilinusurika kukamatwa

2011 UDSM nilinusurika kukamatwa

Huu mwaka sitausahau pale mlimani.

Washikaji zetu ,Christopher mbusule, Lusako ,Ndunguru na wengine wengi tu walipoteza chuo.

Mlimani city ilikuwa jumba la maficho . Tulikimbia tukajificha kwenye maduka. Wale jamaa walikuja na hasira kama za simba wakitutafuta.

Poleni sana washikaji wote mliopoteza chuo kipindi Hicho. Harakati zenu zilifanyika neema kwa wengine.

Mungu bado anatupigania . Siku zimepita na maisha yanaendelea.
Graduate anaandika nilinusulika dah
 
Nilichojifunza kwenye wengi poana mengi. Wewe unaweza ukawa unafikiri kua lengo lenu ni moja ila kumbe miongoni mwenu kuna watu wana maelngo tofauti kabisa na maovu. Kusema kweli mgomo wa 2011 ulikua wa mwisho na sidhani kama itakaa kutokea mgomo mwingine tena kwenye vyuo vikuu.
Vijana walifanikiwa kwa asilimia mia moja kwenye mgomo ule japo furaha iligeuka msiba baada ya kusherehekea ushindi kwa kutaka kwenda kutoa kipigo kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi (DARUSO) ambapo ilikuja kutafsiriwa kama jaribio la kutaka kupindua serikali ya wanafunzi.

Wakati mwingine najiuliza kama wale wanaosomea uandishi wa habari (Mass communication) matukio kama yale hawawezi hata kuyaandalia habari kwa kina na kuja na kitabu au makala zinazoelezea kwa kina kiini cha tatizo na masimulizi mpaka ilivyoisha na hasara au faida zilizopatikana.

Ila yote kumi tisa yule jamaa aliyejiita alshabab alikua mtu wa tofauti sana (Charismatic leader) kwa waliokuwepo mitaa ya chuo na kufatilia kiundani jamaa alijaliwa uwezo wa kushawishi watu.

jina lake lilikua halifahamiki kwa hiyo hata utawala walipata shida sana kumdhibiti mana hawajui ni nani wala anasoma kozi gani, alisumbua sana.
Yule jamaa alikuwa ni hatari sana.
 
Huyo huyo Ndunguru akafika revolution square pale, akaanza kutema hoja baada ya muda watu wakajaa, jamaa yuko peku peku anaongea balaa. Kilichokua kinasisimua zaidi ni hoja zilivyokua zinatolewa. Baada ya Ndunguru na wengine kukamatwa sasa ndio chuma Alshabab kilipoamka sasa,, akaanza peke yake ku mobilize watu na kuhubiri. The guy will make a very good politician sijui yuko wapi siku hizi.
Dah nmetokaa mpk machozi kipindi hikii hali ilikuwa tete mno, tumefka tu chuo 2010, tukamkuta Ally Hapi (chuoni alijulkana kama Salum) mwanaharakati akatuaminisha kuwa yeye ni Mpinzani anampinga rais (Kipara) ambaye alitajwa kama mwana CCM kumbe mchumia tumbo Salum Sijui Hapi nilikuwa namuona ndumilakuwilii mnoo, mwisho wa siku kwa usaliti alioufanya alikimbia Chuoo manake raia walkuwa na Hasira nae Vibayaa ila tanzania wasaliti ni wengi mno, nakumbuka baada ya wanaharakati wengi kufukuzwa ndo wale viongozi wa Daruso namkumbuka mbusule ambae alikuwa Speaker walivosimama kututetea wakatemwa pia ila mule mule Daruso walikuwemo machizi, basii wanafunzi wakajiweka pembeni, akaibuka Ndunguru jamaa alkuwa na mwilii mkubwa, Hoja nzito nae akakamatwaa ndo akatokea Alshabaab...Huyu jamaa alkuwa Kichwa, Organiser mzurii Mno, aaaah nmemkumbka Alshabiib haaa Kizazi cha Kuhojii kilishiaa hapaa UDSM....
 
Kweli kabisa.. nakumbuka mwaka 2008 njaa ilisababisha tukagawiwa chai na maharage Kama dinner kisa shule haikuwa na unga wa kupika ugali...
Ilikuwa shida sana..
Daah aisee maharage yenyewe yalikuwa mazuri au yaleyale ya kwetu?
 
sasa watoto ni waki nani wewe umesha pata mafao yako kikokotoo NSSF.kuona jua sio kuona mengi inawezekana hata mtwara upajui.basi waache waleta uzi watuburudishe
hivi kupajua mtwara ndio ujanja?
 
Ninyi mliyafanya haya 2011 Mimi niliyafanya haya 2004 nikiwa mwaka wa tatu.
 
Una bahati kwamba haudaiwi na Bodi ya Mikopo. Sasa ndio wakati wako wa kuwa na misimamo - katika level nyingine km ya akina TL.
Kusema kweli ule ujinga siwezi fanya tena kipindi kile nilikua na misimamo ya kipuuzi sana,mwisho wa siku nimekuja kusoma chuo kingine bila mkopo na mzigo wote nikawabebesha wazazi wangu

Ila rev square ni jukwaa ambalo ulitakiwa liendelezwe hadi kesho
 
Back
Top Bottom