2011 UDSM nilinusurika kukamatwa

2011 UDSM nilinusurika kukamatwa

Hivi baada ya ule mgomo boom ndyo liliongezeka vile kutoka 5,000 had 8,000 nadhan
Huu mwaka sitausahau pale mlimani.

Washikaji zetu ,Christopher mbusule, Lusako ,Ndunguru na wengine wengi tu walipoteza chuo.

Mlimani city ilikuwa jumba la maficho . Tulikimbia tukajificha kwenye maduka. Wale jamaa walikuja na hasira kama za simba wakitutafuta.

Poleni sana washikaji wote mliopoteza chuo kipindi Hicho. Harakati zenu zilifanyika neema kwa wengine.

Mungu bado anatupigania . Siku zimepita na maisha yanaendelea.
 
Ila kuna watu ni hatari nakumbuka alshabab kipindi cha mgomo tulikuwa pale utawala mwanadada akaanza kutiririsha maneno maprof walitoka kwny ofisi zao wakasimama kule juu gorofani wakimsikiliza walibaki wanatikisa tu vichwa vipaji vyao vingeendelezwa tungekuwa na wapembuzi na wanasiasa makini sn,
Hiyo siku naikumbuka sana
 
Duuu.Ni shidaaa.Hakika kwa sasa hatuna tena vyuo.Unakumbuka mabomu ya Mlimani City kwenye harakati ya kwenda ikulu?.Kwa kifupi,CASS ilipoteza wawili.Hao wote tulikuwa nao kwenye literature.
Pale shati langu lilichanika mgongo mzima baada ya kupenya sehemu kwenye fensi ya waya, huku nikiacha raba yangu pale
 
Mbona ID yako na avatar yako haviendani, kwema?

Kwema tu, habari yako!!?

Mwenzako kaandika kwa hisia ila ww umeangalia tu spelling,,content hujaijali.

Am sorry, ila nimechukia kwa kitendo hicho.

Hii ID na avatar haviendan kwa lengo flan,,..na havina uhusiano na uhalisia wwote wa maisha yangu.
 
pole sana.ulitusaidia pole kwa kweli
vipi lakini
Kusema kweli ule ujinga siwezi fanya tena kipindi kile nilikua na misimamo ya kipuuzi sana,mwisho wa siku nimekuja kusoma chuo kingine bila mkopo na mzigo wote nikawabebesha wazazi wangu

Ila rev square ni jukwaa ambalo ulitakiwa liendelezwe hadi kesho
 
Hahaha halafu kama sijakosea huo mgomo watu wa COET kama vile walijitenga navyokumbuka ni kama vile walifunga geti lao ngwini wasiingie mule hahaha
Yeah walijitenga,kama kumbukumbu zangu zipo sahihi kuna Prof wao alipigwa,Jamaa wa Coet walikuwa hawataki kuungana nasisi kwenye mgomo
 
Back
Top Bottom