Nyaru-sare
JF-Expert Member
- Aug 2, 2019
- 5,263
- 3,628
Kuuuuumbe unaona sasa?? yaani mie niliosoma nao huko woote? hakuna hata mmoja aliwahi shinda kwenda seco. ni mimi tuu! na nilipo kanyaga sec. tu maisha yalikuwa murua sana!! wkt wanafunzi wanagomea msosi niliwalaumu kimoyomoyo sana!Naluelewa mkuu. Nilisoma shule nzuri sana kwa kweli, nadhani inaendana na IST . Darasani tukiwa 30 tunaonekana wengi sana. Aina ya shule nnayotamani wanangu wasome pia. Wanafunzi wanachochewa kuwa wabunifu. Walimu wanafundisha kwa nia na kujadiliana na wanafunzi, siyo kufoka foka na fimbo. Ubunifu unapewa kipaumbele na kila somo linaumuhimu sawa na lingine siyo yale mambo ya 'sciences ni bora kuliko arts' na kila mwanafunzi anaaminishwa atatoboa katika sekta yoyote apendayo. Library ina vitabu kama vyote so nilikuwa nashinda huko nasoma kila topic niipendayo kuanzia wanyama na samaki, hollywood film industry hadi shakespeare (hii yote ni kujisomea mwenyewe siyo kusukumwa usome).
Pia ulikuwa na kipindi kinaitwa 'library' kama nakumbuka vizuri. Darasa zima linaenda library na kazi ya mwanafunzi hapo ni kuchagua kitabu chochote na kujisosomea kwa dk. 30 - 60. Ukikutwa huna kitabu unakula adhabu. Wa kusoma 'sungura na fisi', haya. Wa kusoma 'quantum physics' haya...mwisho wa siku mwanafunzi anajikuta anajua mengi na naamini inaboresha maisha yake ndani na nje ya nafsi yake. Inamsaidia mwanafunzi kutambua ni nini anapenda na inamsaidia kuamua mapema anataka kufuata taaluma gani baadae. Na wanajifunza kufikiria 'nje ya box'.
Suala la shule za vijijini na hali zake linanisikitisha mpaka leo na katika michango yangu midogo ya kijamii, nachangia kwenye elimu.
Ok! nikamaliza sec. bana nikaenda chuo cha sirikali maweeee!! yaani nilitamani hata kubaki hapo chuoni maisha yote! yaani maisha swafiiiii!! ever seen before kabisa! tena wanakupa na cha juu!! Loool! nkasema hapa hapa! unakuwa afisa halafu dent!
tatizo lao kubwa bana hapo shuleni!! sana uki fail!! bana wee unarudishwa tuuuu!! tena faster! utake usitake! .... inauma sana unaweza ukanywa sumu!
kila nilipopiga hatua mbele palikuwa ni bora ya zaidi ninakotoka!! kusema kweli nilirudi kijijini lkn siyo kiviiile!..... jamani shule za mbele tamu sana! ni kwa vile watu hawajui tu!