Taratibu za kufuata ili kupunguza thamani za hisa za kampuni

Cobrahypnosis

JF-Expert Member
Jul 28, 2021
354
642
habarini wanajukwaa natuamini wote ni wazima wa afya na mlio na changamoto mungu awe nanyi katika kila hatua AMEN.
Naomba muongozo wa taratibu gani za kufuata ili kuweza kupunguza thamani ya hisa za kampuni. mfano katika memats ya kampuni tuliandika thamani ya hisa moja ni 2 million lakini tunataka kupunguza thamani ya hisa mpaka elfu 20 kwa hisa moja ili kuendana na hali halisi ya mtaji wa kampuni. wajuzi naombeni mchango wenu. ahsante.
 
NiPM
 
Mkuu utakapo jibu kwa ufasaha na usahihi kwene post hii utafaidisha maelfu ya wadau hapa. Jukwaa lingekuwa halina maana kama kila mtu angekuwa anajibu inbox kwa mwenzie. Share maarifa yako nasi ili kila msomaji afaidike.
 
habarini wanajukwaa natuamini wote ni wazima wa afya na mlio na changamoto mungu awe nanyi katika kila hatua AMEN.
Naomba muongozo wa taratibu gani za kufuata ili kuweza kupunguza thamani ya hisa za kampuni. mfano katika memats ya kampuni tuliandika thamani ya hisa moja ni 2 million lakini tunataka kupunguza thamani ya hisa mpaka elfu 20 kwa hisa moja ili kuendana na hali halisi ya mtaji wa kampuni. wajuzi naombeni mchango wenu. ahsante.
Kwanza kabisa inabidi katika MEMART iwe imetoa mamlaka yakuweza kupunguza hisa zake(reduction of shares),ili uweze kufanya hivyo lazima yafuatayo yaweze kufuatwa;

1: Kabla ya kufanya kikao hicho cha kupunguza hisa lazima Mkurugenzi au majority shareholders wahakikishe kwamba,kampuni itakuwa na uwezo wa kulipa madeni yake yote kwa wadeni wake ndani ya kipindi cha miezi 12

2:Lazima kutolewe taarifa ya kikao Special Resolution ya kupunguza hisa za kampuni ikiambatana na cheti au certificate of insolvency ya Director pamoja na ripoti ya wakaguzi (auditors reports)

3:Maazimio maalumu ya kupunguza hisa za kampuni(special resolution for reduction of share capital)baada ya kukamilika inapaswa kufungua maombi(Petition)kwenda mahakamani ya kuridhia (confirm) azimio la kupunguza hisa ya Kampuni ,lengo la kufungua maombi(petition) mahakamani ni kuhakikisha kwamba madeni yote ambayo kampuni iko nayo ynaweza kulipwa kwa wakati au haitaweza kuthiriwa na azimio la kupunguza hisa(resolution for reduction of shares),baada ya hapo sasa kwa muongozo wa mahakama Kampuni itapewa maelekezo ya kutoa tangazo kwa umma la azimio lake la kupunguza hisa za Kampuni kupitia gazeti la serikali,ndani ya siku 5 toka tarehe na siku ambayo azimio hilo lilipitiswa,ikiambatana na sababu za kupunguza hisa or share capital.

4: Kupeleka au kusajili azimio la kupunguza hisa ya Kampuni kwa msajili wa makampuni,ikiambatana nakala ya mahakama ya kuridhia kupunguzwa kwa hisa za kampuni.

Naimani utakuwa umepata mwangaza
 
Back
Top Bottom