14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

14-Oktoba-1999: Ulikuwa wapi?

Me ndio nilikuwa na miezi miwili tu, kuwepo pale ppf. Nakumbuka at that time, ndio nimetoka toka tu chuo, then nikabahatika kuingia pale....ila kiti kikawa kichungu gafla, maana kila mtu anakitamani..!!

Sasa siku hiyo nipo nimekaa tu, nikiwa na mawazo yangu ya hapa na pale.....ndio paap naletewa taarifa na Ps wangu.

Ps: Mkuu, Mkuu Baba amefariki...
Me: Ooh!! pole sana binti, alikuwa anaumwa?.
Ps: Me sijui lolote mkuu.
Me: (Kichwani) nikaona huyu binti, kashaanza kupagawa..."inawezekana vipi, baba yake anafariki then ajui lolote..."

Ila suddenly ndio nikapokea simu ya mkubwa wangu, Mr Erio. "Ebwana Mr prisoner of hope, mzee wetu wa taifa ndio katutoka hivi.....so naomba ufanye 1,2,3.

Aiseeh iliniuma sana!
 
hehehe..chaka siopoa yani,daah niliondokaga nikaenda Moro nikakaa kama miaka 7 ile kurudi nilipotea aisee

Yan hapo abiola kwa chini kulikua na ndugu yangu ana genge, siku hizi hata ramani zimepotea, mambo yamebadilika kweli
 
Nilikuwa darasa la nne, ila nazani mheshimiwa hakufariki tarehe hiyo mi nazani hiyo tarehe ndo uma wa ki tz ndo ulifahamisha baada ya mambo yote kusetiwa kuwa hakuna buguza ya kutokea mana kuna people ziliamin bila mheshemiwa tz haisongi, watu wakaa standby siraha mkononi majeshi yote. Pili kuhusu nyimbo zilikuwa zishatungwa kitambo na zilikuwa zinasubiria tukio tu mana mheshimiwa hali yake ilianza kuwa tete kitambo na wajuzi wa mambo wakawa wanajua soon kuna kitu kita happen
 
Amini usiamini. Nyerere alikufa kabla ya 14 October 1999. Alikufa mapema ila serikali haikutangaza ili kujitayarisha kwanza zikiwemo nyimbo zile za Komba. Nilikuwa university wakati huo. Nililia machozi. Kusomeshwa bure nikipewa madaftari, kalamu na waranty za serikali za kusafikiri kwa meli, treni na mabasi bure wakati niko sekondari lilikuwa jambo la kumshukuru Nyerere. Bila yeye, ningekuwa mkulima huko kijijini.
Nilikuwa Mafinga sec! Siku hiyo tulikuwa ziara ya kimasomo Kalenga kuona fuvu la Mkwawa! Nakumbuka nyimbo za Kapten Komba, sijui alizitunga muda gani?
 
Naikumbuka sana maana graduation ya four niliishia kutokuwa kumbukumbu. Mwaka 1999 graduation zote ziliahirishwa ili tukamlilie mwanzilishi wa chama kibovu kuliko vyote Africa kwa wakati huu.
 
**** primary school Mtwara,tumeshapiga paper ya standard seven tunafanya mazoezi ya mahafali,mara paap kengele ya dharula inagonga muda huo mi nipo juu ya mnazi wa shule naangusha madafu,wahuni wenzangu wapo chini wanayafua hahahaa basi tukakusanyika fasta assembly shule nzima,mwalimu mkuu Mama Mwangata anatangaza kwamba nyerere kafariki,wanafunzi wa madarasa ya chini wanalia kwa sauti,walimu wanawatuliza kwamba hakutakua na vita tulieni,that was 14/10/1999...
Nimeipenda Sana maisha yako ya shule
 
Nilikuwa form four na graduation iliishia kukatwa. Wote tuliambiwa tumlilie mwasisivwa liccm.
 
Nastahili heshima zaidi... Nilikuwa Chuo Kikuu.
Heshima yako Mkuu, kama ulikuwa kidato cha sita, nakumbuka mm nilikuwa dalasa la saba, sikumbuki kama tulikuwa tumefanya mitahani ya kuhitimu au ilikuwa bado ila ilikuwa kwenye purukushani za kumaliza dalasa la saba, nakumbuka tukawa tunajazwa hofu ya kutokea vita kati ya TZ na Nchi Jirani! Dah long time sana Shule ya Msingi Mwenge Kasulu!
 
Nilikuwa form four na graduation iliishia kukatwa. Wote tuliambiwa tumlilie mwasisivwa liccm.
 
Nilikuwa masomoni Ukraine, jamaa mmoja akaja hosteli na kuniambia kuwa Mwalimu Nyerere amefariki, ilikuwa wiki ya huzuni kule kule ughaibuni.

Maisha ni mafupi, leo imepita miaka 20 tangu mchana ule.
 
Back
Top Bottom