umeme

  1. Hemedy Jr Junior

    JamiiForums Tanzania Tatizo la umeme Vingunguti Dar es Salaam, leo siku ya tatu umeme hakuna

    Umeme unapokosekana tambua pia maji yanakosa, maana hawa jamaa DAWASCO na TANESCO baba mmoja. Tunaomba mrejeshe umeme Vingunguti, mnakataje umeme siku 3 bila taarifa? Mnatukosea sana.
  2. kmbwembwe

    JamiiForums Tanzania Hivi hii TANESCO ya Maharage si walisema umeme wa grid umeshafika Kigoma?

    Naangalia taarifa ya habari ITV sasa hivi, nimestaajabu kumuona CEO wa TANESCO Maharage akisema umeme wa grid ndio uko asilimia 47 kuelekea Kigoma. Mimi labda siko Tanzania au sielewi. Nakumbuka kwa masikio yangu nimesikia tena sio mara moja kwamba umeme wa grid ulishafika Kigoma miezi kadhaa...
  3. FRANCIS DA DON

    JamiiForums Tanzania Je, karakana ndogo ya kuzalisha ‘transformer’ ndogo za umeme inaweza kuhutaji mtaji wa kiasi gani?

    Mfano karakana ya kawaida tu kama hiyo iliyopo kwenye video hapo, naweza kuikamilisha na ikaanza uzalishaji kwa milioni 50? Na je, wataalam kutoka VETA wapo nioweza kuwajiri na wakafanya huu uzalishaji? Na je, kuhusu soko, Tanesco bado wana sera ya kununua bidhaa za ndani kwanza kabla ya vya nje...
  4. Bams

    JamiiForums Tanzania Kutokuwepo kwa umeme kila siku asubuhi na jioni mpaka usiku, tatizo ni nini?

    Kuna mambo yanayoendelea mpaka unajiuliza, hivi nchi hii hatuna watu wenye akili, uwezo na dhamira safi ya kuendeleza Taifa? Nimesafiri na kukaa kati ya wiki moja hadi mwezi mmoja kwenye mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Mara. Yanaoendelea katika maeneo haya kuhusiana na nishati ya umeme ni...
  5. BARD AI

    JamiiForums Tanzania Serikali kushusha bei ya gesi kama uzalishaji umeme utakuwa mkubwa

    Serikali imesema iwapo mipango ya kuongeza uzalishaji umeme itakwenda kama inavyokusudiwa itasaidia kupunguza gharama za matumizi ya gesi kwa wananchi wa kipato cha kati na chini. Hayo yameelezwa leo Machi 15 na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda, Exaud Kigahe kwa niaba ya Waziri wa...
  6. Faana

    JamiiForums Tanzania TANESCO mnapokata umeme toeni taarifa in advance. Mafundi wenu hutumia mwanya huo kuiba mafuta ya transfoma

    Kichwa cha habari kinajieleza, inafaa mnapokata umeme mtoe taarifa kwa wakazi wa maeneo husika ili tutambue katizo hilo ni official, msipotoa taarifa mnakosa ushirikiano wa wananchi kuweka attention kwenye transforma zenu ambapo mara nyingi wengi huwa tunadhani mmekata kwaajili ya matengenezo...
  7. Stephano Mgendanyi

    JamiiForums Tanzania Ujenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme katika Mradi wa JNHPP Yafikia 92%

    Waziri wa Nishati, January Makamba amesema kuwa, Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inaendelea na utekelezaji wa mradi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Bwawa la Julius Nyerere hadi Chalinze pamoja na ujenzi wa Kituo cha kupoza umeme cha Chalinze ambapo ujenzi wa njia ya...
  8. J

    JamiiForums Tanzania Natoa siku 14 kwa viongozi wa Tanesco walioshiriki kuninyima umeme mbezi beach!

    Mimi kama "Jicho la Mganga" nafikisha ujumbe huu kutoka kwa Wilfred kwenda kwa viongozi wa Tanesco! Wilfred anasema! Takribani miezi miwili sasa Tanesco wananihangaisha! Uungwana wangu hauna maana kwao! Niliomba umeme pale tanesco tankibovu, kwa kufuata taratibu zote, wakaja kunipimia na...
  9. Allen Kilewella

    JamiiForums Tanzania Hayati Magufuli alidhibiti ukatwaji wa umeme au mazingira yalimbeba?

    Vyanzo vya maji kwa ajili ya Mabwawa makubwa matatu ya kuzalishia umeme, yaani Bwawa la Mtera, Kidatu, na Kihanzi, vyote kwa asilimia tisini (90%) vinategemena na sehemu kubwa vinatokana na vyanzo vile vile. Kwa mfano sehemu kubwa ya maji yanayojaza bwawa la Mtera na Kidatu chanzo chake ni kile...
  10. U

    JamiiForums Tanzania TANESCO wakata umeme mbele ya Mkutano wa Rais, Kilimanjaro

    Hali hii ya sintofahamu ilitokea siku ya leo katika ukumbi wa Kuringe Moshi, Ambapo Umeme ulikatika ghafla na kuleta taharuki ya kiusalama Ukumbini. Ni Vyema Uongozi wa juu wa TANESCO uwe unafanya maandalizi ya ukarabati na kuhakikisha umeme unakuwepo wakati wote pindi Kiongozi Mkuu wa Serikali...
  11. Debby the FEMINIST

    JamiiForums Tanzania Lindi: Wajawazito wajifungulia kwa tochi umeme ukikatika kituo cha afya rutamba

    Wakati dunia ikiadhimisha siku ya wanawake Duniani, wanawake wa kata ya Rutamba halmashauri ya manispaa ya Lindi wamelia na changamoto ya uchakavu wa miundombinu katika kituo cha afya cha Rutamba. Wamelalamikia hayo baada ya wafanyakazi wanawake kutoka Mashujaa FM kufika kituoni hapo...
  12. J

    JamiiForums Tanzania Waziri Makamba: Iwe Mjini au Kijijini Gharama wanayatumia Tanesco kumuingizia mtu umeme ni Tsh 800,000

    Waziri wa Nishati January Makamba amemshukuru Rais Samia kwa kuwapa tsh 500bil kwa ajili ya ukarabati wa Miundombinu ya Umeme, jumla ya Fedha inayohitajika ni zaidi ya tsh trillion 1. Makamba amesema iwe Mjini au Kijijini Gharama za kuunganisha Umeme wanazotumia Tanesco ni wastani wa tsh...
  13. S

    JamiiForums Tanzania Mradi wa nguzo za umeme za zege umeishia wapi? Nchi ina vituko hii!!

    Bila shaka vita ilikuwa kubwa Sana. Na hatimaye wenye mashamba ya miti wameshinda. Siku hizi nguzo za zege siyo tu hazisambazwi bali pia haziongelewi tena. Yule bwana alikuwa na % yake kwenye viwanda vya nguzo hizo. Alipokufa kafa navyo. #Tanzania yangu!
  14. J

    JamiiForums Tanzania Bila umeme wa uhakika, tunawezaje kunufaika na Teknolojia?

    Umeme ni hitaji la Msingi katika kufikia na kutumia Teknolojia, ikiwemo Intaneti Kama Mwananchi unayetumia au kutegemea Digitali kwa shughuli mbalimbali, unaathirika kwa kiwango gani unapokosa Umeme?
  15. Ahyan

    JamiiForums Tanzania Saa 12 bila umeme Lushoto

    Hii hali kwa sasa imekuwa ni zaidi ya kero, masaa 12 hakuna umeme. Mmeshawahi waza ni shughuli ngapi zinasimama kwa kutokuwepo kwa umeme? Na je mkawaza ni kiasi gani cha mapato kinapotea kwa wakati huo ambao umeme haupo? Kuweni serious hata kama ni marekebisho si kwa muda wa masaa 12. Mama...
  16. N

    JamiiForums Tanzania Umeme kusambazwa hadi kwenye vitongoji

    Serikali ya Rais Samia Suluhu inaendelea kuhakikisha umeme unafika katika kila kitongoji lengo ikiwani ni kuibua fursa zitokanazo na umeme, Rais Samia Suluhu alisema "Nishati ya uhakika ni uhuru" akimanisha kuwa kukiwa na nishati ya uhakika wananchi wanakua na uhuru wa kufanya shughuri zao za...
  17. N

    JamiiForums Tanzania Rais Samia amevipa vijiji kipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya umeme

    Serikali ya Rais Samia Suluhu inatekeleza miradi mikubwa mitatu ya kupeleka umeme zaidi vijijini miradi ambayo itagusa sekta ya kilimo, afya, maji, viwanda vidogo na madini. Ukamilishaji wa miradi hii ni December mwaka huu
  18. Black Butterfly

    JamiiForums Tanzania Tanzania yasaini makubaliano ya Ushirikiano na Indonesia kwenye Sekta ya Umeme na Gesi

    Ziara ya Waziri wa Nishati, January Makamba nchini Indonesia imemalizika kwa kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili katika sekta ya umeme, mafuta na gesi. Makamba kwa nyakati tofauti alikutana na Waziri wa Nchi anayeratibu biashara zinazomilikiwa na Serikali, Luhut Pandiaitan, Waziri wa...
  19. K

    JamiiForums Tanzania Rais Samia: Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere kujaribiwa mwakani

    Rais Samia Suluhu Hassan leo ameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya kuimarisha Gridi ya Taifa na usambazaji wa umeme Vijijini iliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023. Kwenye hotuba yake Rais Samia anasema wakati anakabidhiwa madaraka jambo lililokua linamuumiza kichwa ni...
  20. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Rais Samia ashuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa miradi mahsusi ya umeme. Vijiji vyote Bara kufikiwa umeme mwishoni mwa 2023

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishudia Utiaji Saini wa Mikataba ya Utekelezaji wa Miradi Mahsusi ya Umeme leo tarehe 14 Februari, 2023 Ikulu Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini REA, Hassan Said anazungumza Mikataba 14 ya Wakala wa...
Back
Top Bottom