Nigrastratatract nerve
JF-Expert Member
- Sep 4, 2019
- 1,395
- 3,901
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoani Kilimanjaro limeikatia umeme hoteli ya Aish hotel inayomilikiwa na Mbunge wa Hai (CHADEMA), Freeman Mbowe kwa madai kuwa wamebaini inatumia umeme wa wizi na kuisababishia Serikali hasara ya shilingi milioni 10.8.
Akiungumza, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kilimanjaro, Mahawa Mkaka, Shirika hilo limebaini jana Septemba 14 kuwa wamejiunganishia umeme na kuharibu miundo mbinu yake.
“Baada ya kupata taarifa kutoka vyanzo vyetu tulienda kwenye hoteli hiyo kufanya ukaguzi, tukabaini wameharibu mita na kujiunganishia umeme kinyemela. Hasara hiyo ya milioni 10.8 ni kwa tathmini ya awali na sasa hivi tunasubiri hesabu kutoka Tanesco makao makuu,” amesema Mkaka.