Mliomshambulia January Makamba njooni mumpongeze baada ya hali ya umeme kutengemaa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,338
9,766
Ndugu zangu watanzania,

Uongozi Unahitaji kuwa na ngozi ngumu, Unahitaji kuwa na msimamo, Unahitaji kuwa mvumilivu na mwenye Subira, Unahitaji kuwa na Nidhamu ya kimaamuzi, Unahitaji kutoyumbishwa na upepo uvumao, Unahitaji kujuwa unasimamia Nini, Unahitaji kujuwa kuwa huwezi ukawafurahisha watu wote kwa wakati wote.

Unahitaji kujuwa kuwa hata ungefanya mema mangapi bado kuna watu hawataridhika, inahitaji kujuwa kuwa hata ungetengeneza na ukafanya mabomba yatoe asali na maziwa katika kila Kaya bado kuna watu watasema mabomba yako yanaleta nzi na hivyo yatasababisha mlipuko wa kipindu pindu.

Inahitaji kujuwa kuwa Kuna watu kazi Yao na miaka yote huwa Ni wakupinga kila kitu ,kukosoa kila kitu ,kulaumu kila kitu na kila mtu na kila mtu hafai isipokuwa wao tu.

Kama siyo ujasiri wa Rais Samia, ushupavu wa Rais Samia, misimamo na umadhubuti wa Rais Samia, Ngozi ngumu ya Rais Samia, Hekima na Busara za Rais Samia, ukomavu na uzoefu wa kiuongozi wa Rais Samia kwa hakika kufika leo hii January Yusuphu Makamba asingekuwa Waziri wa Nishati na Wala asingekuwepo katika Baraza la mawaziri kwa namna ambavyo alishambuliwa na kutupiwa mawe.

Lakini Rais Samia alitambua Ukweli kwa kuwa yeye ndiye mkuu wa nchi na serikali anayejuwa na kuwa na kila aina ya taarifa mkononi pake iliyopo na inayo endelea hapa nchini kwetu hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa Rais Samia Ni mfuatiliaji Sana wa kila kitu kinachoendelea,kutokea na kufanyika serikalini kwake na nchini mwake.

Rais Samia alitambua Nini tatizo la kukatika katika kwa umeme na chanzo chake, akatoka hadharani akaongea ukweli kuwaeleza watanzania na kututaka Tuwe na subira na Hali iliyokuwa imetokea iliyokuwa imetokana na Hali ya ukame na kutuahidi serikali Yake kulishughulikia suala Hilo ili lisilete athari kubwa.

Kweli watanzania tukawa wavumilivu na wenye subira na tuliziona juhudi za serikali yetu kupitia Wizara ya Nishati katika kuongeza na kutumia vyanzo vingine Kama gas Asili kuzalisha umeme na wakati wote tukawa tunapewa taarifa.

Mh Makamba aliendelea kuwa mvumilivu na mstahimilivu juu ya mawe yote aliyotupiwa, na badala ya kuyaokota na kuwarushia waliomtupia yeye aliyaokota na kuyajengea msingi wake wa kiutendaji katika wizara yake, aliendelea kutoa majibu ya kiungwana na ukweli japo mchungu, aliendelea kuwa mtulivu na mwenye hekima na busara pasipo kuna wa na jazba na hasira, aliendelea kukidhibiti kifua chake kwa kutambua kuwa huo ndio uongozi na unapaswa kuvumilia lawama na maneno yote bila kuyumba kiutendaji.

Leo Hali ya Umeme imerejea katika Hali yake ya kawaida na Taifa linapata Nishati ya umeme saa 24 kila mahali Giza limetokomezwa mbali,Taa majumbani zinawaka muda wotee, hata kwa wasio na umeme wanapata mwanga wa umeme kupitia Taa za umeme za majirani zao.

Rai yangu kwa January Yusuphu Makamba ni kuchapa kazi kwa nguvu zake zote, kwa ubunifu wa Hali ya juu, kwa uaminifu na uadilifu, kwa weledi na kwa Nidhamu, ahakikishe anamheshimisha Rais wetu na kukidhi matarajio ya Rais katika kutimiza majukumu ya Wizara hiyo nyeti.

Ahakikishe anasimamia vizuri watendaji wote walio chini ya Wizara yake,Ahakikishe kuwa hakuna anayefanya kazi kwa mazoea,Ahakikishe watanzania wanapata huduma Bora na kuhudumiwa kwa ukarimu waendapo katika ofisi zote zilizo chini yake.

Ahakikishe kuwa Taarifa zinatolewa na mamlaka ya eneo husika endapo kutakuwa na matengenezo ya aina yoyote Ile,mfano zinatolewa taarifa siku moja au mbili kabla juu ya muda gani umeme hautakuwepo, siku gani, sababu gani na kwa saa ngapi, maeneo yatakayoathirika na muda wa kurudi kwa umeme.

Kusiwepo miungu watu katika wizara,Ahakikishe mikataba yote inayoingiwa chini ya Wizara yake inasainiwa baada ya tafakuri ya kina kwa kushirikiana na wanasheria na wataalamu wa Wizara, kuangalia namna Taifa letu litakavyo nufaika na kutojifunga kisheria katika maamuzi tunayojuwa yataleta madhara huko mbele ya safari.

Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa wafanyakazi kwa kujenga Ari ya kazi na utumishi uliotukuka,kila mtu aipende kazi na aiheshimu kazi.

January Makamba Nakuomba Sana umsaidie mama yetu na Rais wetu kwa kutimiza majukumu yako vyema, usimuangushe Rais wetu kwa Imani na heshima aliyokupatia na Wala usijisahau na wala usijiringanishe na Rais na pia utambue kuwa Rais huwa siku zote hazoeleki na yeyote yule maana hiyo Ni Taasisi kubwa.

Usimfanye akatukanwa na kusemwa Sana kwa ajili yako bali mfanye ajivunie uwepo wako katika wizara, fanya Sana kazi na kujituma kwa nguvu zako zote,usipoelewa omba ushauri mahali pengine palipo kisheria yaani kwa wataalamu walio katika wizara yako.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
 
Back
Top Bottom