Kipindi fulani, nikiwa ninafanyia shughuli zangu maeneo ya machimbo ya dhahabu, nilifahamiana na kijana mmoja kutoka mkoani Kigoma. Alikuwa anafanya vibarua machimboni.
Kuna wakati alinifuata kwa ajili ya kuniomba ushauri. Aliniambia kuwa alikuja machimboni kama njia ya kumtoroka babu yake...