uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. J

    JamiiForums Tanzania Dr. Bashiru: Mbinu na mikakati tuliyotumia kupata ushindi wa 99% kwenye Serikali za mitaa ndizo tutakazotumia uchaguzi mkuu 2020

    Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru amesema kuwa katika uchaguzi mkuu wa Octoba 2020 CCM itatumia mbinu, mikakati na ubunifu ule ule uliotumika kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Dr Bashiru amesisitiza kuwa yeyote atakayejipendekeza kugombea udiwani, uwakilishi, ubunge...
  2. JamiiForums Tanzania GE2020 CHADEMA kupoteza majimbo yafuatayo

    Kimahesabu, CCM ndio washindi wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 kabla hata ya mwenda kwenye Box la Kupigia kura. Ushindi huu wa CCM ambao umetokana na utekelezaji kabambe wa miradi mbali mbali chini ya serikali ya awamu ya tano. HESABU ZA KISIASA zinaonesha majimbo yafuatayo ya Upinzani yanakwenda...
  3. JamiiForums Tanzania Dkt Bashiru: Uchaguzi sio namba uchaguzi ni uamuzi wa umma

    Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewakumbusha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini maana halisi ya uchaguzi ni maamuzi ya Umma si kama ambavyo wamekuwa wakieleza kwa kupotosha kuwa, uchaguzi ni namba. Ameyasema hayo tarehe 13 Januari, 2020 alipokuwa akihutubia...
  4. JamiiForums Tanzania GE2020 Kuelekea Uchaguzi: Tafadhali wale wanasiasa wote ambao hampendi, mnateseka sana mkikosolewa au mnahisi kuvunjiwa heshima mnapokosolewa, Msigombee!

    Hello Wana JF, Tanzania ni nchi ya vyama vingi tangu 1992! Tulikubaliana wenyewe kwamba tuendeshe nchi yetu kwa taratibu za kidemokrasia kwa kuruhusu mfumo wa vyama vingi. Na kwa mantiki hiyo, kila mtawala anaeapa kwa mujibu wa katiba tuliyonayo anapaswa kuheshimu taratibu tulizojiwelea...
  5. JamiiForums Tanzania GE2020 Kwanamna uchaguzi wa serikali za mitaa ulivyoendeshwa je ni halali kuendelea na katiba inayozuia matokeo ya urais kupingwa mahakamani?

    Kwakweli sielewi hiki kipengele kinachozuia matokeo ya urais kupingwa mahakamani kina Nia njema ipi. Yani katika mazingira ya Tanzania ya Sasa yenye uvunjifu wa sheria zote pamoja na haki za binadamu bado kipengele kama hiki tukione kina nia njema kweli? Nitakuwa was mwisho kuamini . Vyama vya...
  6. JamiiForums Tanzania Mapokezi ya Katibu Mkuu wa Chadema Mh Mnyika yatikisa Kibamba, awaasa wanahabari kupigania Tume huru ya uchaguzi, Kabendera na Magoti watajwa

    Hii hapa video unaweza kuitazama mwenyewe, lakini kwa wasio na bando, Mh Mnyika leo amefika kwa mara ya kwanza kwenye jimbo analoliwakilisha la Kibamba tangu kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu na kupokelewa kwa kishindo na wapiga kura wake ambapo wamempongeza kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu...
  7. JamiiForums Tanzania GE2020 Vyama vya upinzani msipogomea uchaguzi 2020 bila tume huru tutawashinikiza sisi wanachama

    Vyama vya upinzani chondechonde msije mkakubali kuingia kwenye uchaguzi 2020 bila tume huru. Hulka na tabia ya jiwe na serikali yake mmeshaiona hawana aibu heshima staha Wala huruma kwenu Wala hawaifwati katiba. Kama jiwe ameweza kuchezea uchaguzi wa serikali za mitaa bila kufanywa lolote Wala...
  8. JamiiForums Kenya, JamiiForums Tanzania Kenya kufanya Uchaguzi Mkuu mwingine mwaka huu, Duh!

    Hawa jamaa wanajua kutupa pesa aisee, duh!
  9. J

    JamiiForums Tanzania GE2020 Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020 kutangazwa jijini Dodoma

    Tume huru ya Uchaguzi NEC imesema matokeo ya Uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi october mwaka huu yatatangazwa kutokea jijini Dodoma. Source: Habari Leo Maendeleo hayana vyama!
  10. JamiiForums Tanzania Isaya Mwita ni kikwazo cha CCM kuchota Pesa ya uchaguzi kwenye Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, ndio chanzo cha kuwekewa zengwe

    Wakuu hii ndio sababu kubwa ya CCM kutaka kumuondoa Meya wa Jiji la Dar es Salaam , hakuna sababu nyingine yoyote ile. Mwita anatuhumiwa kuzuia matumizi ya zaidi bil 5 ambazo ni mgawo kutoka UDART, Je, ni matumizi gani hayo yaliyotakiwa kufanywa na kwanini yamezuiliwa ? Hakuna mwanaccm...
  11. JamiiForums Tanzania Dar: Vurugu zatokea kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Jijini Dar cha kuamua hatma ya Meya wa Dar, Isaya Mwita

    Kikao cha Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania cha kujadili tuhuma zinazomkabili Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita kimesimama kwa muda baada ya jina la mjumbe wa Chama cha Wananchi (CUF) kusainiwa wakati hayupo ukumbini. Kikao hicho kinafanyikia ukumbi wa Karimejee jijini...
  12. JamiiForums Tanzania Tathmini ya kisayansi juu ya matokeo ya uchaguzi mkuu Novemba 2020

    Sayansi na Teknolojia vikitumika vizuri vina uwezo wa kutoa majibu ya wakati ujao,uliopo na uliopita kwa uhakika wa asilimia 99.9%. Katika andiko langu hili nitatumia taarifa za kisayansi zilizopo kuweza kutoa matokeo ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba 2020. Tathmini hii isitumike...
  13. JamiiForums Tanzania GE2020 Kuelekelea Uchaguzi mkuu 2020: Tupe tetesi na maoni yako, unapendekeza nani agombee wapi na nafasi gani?

    Amani iwe kwenu!! Tutumie thread hii kupendekeza wale wanaofaa kugombea 2020, Tetesi za watu watakaogombea Mimi naanza na Dr. Tulia, Huyu dada amekuwa msaada kwetu na jamii ya Wana Mbeya kwa ujumla kwani kawasaidia wakina Mama wengi kupata mikopo yenye riba nafuu na vijana wengi kwenda Shule...
  14. JamiiForums Tanzania Mwaka wa uchaguzi umefika, tusishangae sana

    Huu ndo mwaka ambao wanasiasa tutacheza nao draft, mpira na bao. Ni mwaka ambao wanasiasa watabeba ndoo kichwani. Ni mwaka ambao usishangae kumuona mwanasiasa akishinda kijiweni. Ni mwaka ambao ligi za mpira za hovyo nyingi tutaziona. Msishangae sana. Msishangae sana kukutana na mwanasiasa...
  15. A

    JamiiForums Tanzania GE2020 Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

    Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Je, serikali ina majibu ya kuwaeleza Watanzania ambao mpaka leo vijiji vyao havijapatiwa umeme nini sababu inayochelewesha ili hali kila siku tunahadithiwa kwamba hela zipo tutembee kifua mbele. Vipi mpango wa kunusuru kaya masikini unaendeleaje? Je...
  16. V

    JamiiForums Tanzania GE2020 Watanzania mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi mkuu, Tunachagua tena Rais pamoja na wabunge

    Watanzania mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi mkuu, Tunachagua tena Rais pamoja na wabunge. Ni mwaka ambao una changamoto kubwa sana katika uchaguzi mkuu hususa upande wa visiwani Watia nia ya kugombea nafasi za ubunge wengi wao wamesha jijua kilichobaki tu ni taratibu za kiofisi Wapinzani...
  17. JamiiForums Tanzania Dr. Bashiru Ally: CCM ni chama kinachoongoza kufanya siasa safi za kiungwana na kiustaarabu kitashinda kwa kishindo uchaguzi mkuu

    CCM YAAHIDI KUENDELEA KUHESHIMU MAAMUZI YA UMMA 02 Januari, 2020 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa, CCM mwaka 2020 itaongoza siasa safi za uchaguzi, ni mwaka wa kudhihirisha CCM inaongoza siasa safi na kuheshimu maamuzi ya Umma kama ilivyofanya mwaka 2019...
  18. J

    JamiiForums Tanzania GE2020 Kwa sasa Udiwani na Ubunge ni ajira, tutegemee changamoto kubwa kuelekea uchaguzi mkuu hasa ndani ya CCM

    Tunakumbushana tu kwamba kwa sasa hapa nchini siasa ni ajira hivyo wabunge na madiwani tegemeeni changamoto kubwa kutoka kwa toleo jipya. Ndio hao akina Harmonize, Diamond, Juma Kaseja, Mrisho Mpoto na wengine wengi wanaopiga jalamba muda huu. Changamoto itaikumba zaidi CCM kwani ndio yenye...
  19. JamiiForums Tanzania GE2020 Dkt. Bashiru: Wanaotegemea Tume Huru iwape ushindi wanajidanganya! Tume haipigi kura

    Binafsi nimeshindwa kumuelewa kabisa huyu bwana mkubwa wa CCM. Maneno aliyo yaongea na elimu aliyo nayo sidhani kama vinaendana. HOTUBA YA DR. BASHIRU KWA UFUPI CCM inatoa salamu za mwaka mpya 2020, niwahakikishie watanzania kuwa tutaongoza siasa safi,ni mwaka wa kuheshimu maoni na uamuzi wa...
  20. JamiiForums Tanzania GE2020 Ni Mwaka wa Uchaguzi Mkuu 2020: Kuthibitisha au Kutengua Maamuzi ya 2015?

    Mwaka 2020 ni mwaka wa kufanya uamuzi kuhusiana na utawala na mwelekeo wa taifa letu. Huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu, mwaka wa Uamuzi Mkuu. Watanzania wataitwa kutoa jibu la maswali makubwa mawili. Je, tuendelee na Rais yule yule aliyechaguliwa mwaka 2015 au tufikirie mtu mwingine? Na pili, Je...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…