Uchaguzi 2020 Vyama vya upinzani msipogomea uchaguzi 2020 bila tume huru tutawashinikiza sisi wanachama

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,926
Vyama vya upinzani chondechonde msije mkakubali kuingia kwenye uchaguzi 2020 bila tume huru.

Hulka na tabia ya jiwe na serikali yake mmeshaiona hawana aibu heshima staha Wala huruma kwenu Wala hawaifwati katiba.

Kama jiwe ameweza kuchezea uchaguzi wa serikali za mitaa bila kufanywa lolote Wala kutokea chochote msitegemee atakuwa mstaarabu octoba 2020.

Mkae mkijua kabisa Kama wakati wa JK kwa demokrasia ile tulishinda na bado tukahujumiwa vipi Sasa wakati wa dikteta jiwe?

Anzeni Sasa nawashauri mwezi huu wa kwanza usiishe kabla hamjaiambia dunia kuhusu ulazima wa kuwepo tume huru ya uchaguzi.

Bahati nzuri dunia nzima inamchukia jiwe na inamfahamu hulka yake sapoti itakuwa kubwa Sana na mwangwi wake utasikika Sana kuliko wakati wowote katika historia ya taifa letu.

Upinzani kumbukeni mnashindana na mtu asie na chembechembe ya ustaarabu hata kidogo Hilo mlijue.
JK alikuwa muungwana huyu ni kinyume chake ni mtu asie wa kawaida hivyo haitaji treatment ya kawaida.

Mkiingia kwenye UCHAGUZI bila kushinikiza tume huru mjue mmebariki suicide (mauwaji) maana ni sawa na kwenda kupigana na Askari mwenye smg wewe ukiwa na njiti ya chelewa Kama fimbo Kama silaha yako ya utetezi dhidi ya smg.

Upinzani kumbukeni watu wamechoka haya maisha wanasubiri mtu wa kumfunga paka kengele watoto wa mjini wanasema mtu wa kulianzisha au kukinukisha (kwa kufuata Sheria za nchi) mtapata sapoti kubwa mno.

Mpinzani wenu ambae ni CCM hakubaliki popote na jamii yoyote ya watanzania ila anatumia dola na propaganda kuwadanganya watu anakubalika kumbe sivyo.

Upinzani narudia Tena na Tena na Tena msije mkaingia kwenye ballot box mkitegemea favor itakuwa imekula kwenu.

Bashiru mmemsikia amesema wazi msitegemee tume huru Maana tume haipigi kura huu ni ujumbe tosha kwenu.

Polepole kawaambia wanaandaa mpango wa kutawala miaka 70 ijayo huo ni ujumbe kwenu upinzani akili kumkichwa.

Jiulizeni kwanini wanaanza kuweka mzinga/kuchonga mzinga wa mwewe (tiss) Zanzibar? Hio inapaswa kuwa alarm kwenu upinzani.

Kuna yanayofanyika gizani na hadharani kuandaa hujuma dhidi ya mazingira yoyote yatakayojiinua kuwabeba msije sema hatukuwaambia.

Kusoma hamuwezi hata picha hamuioni?

Narudia Tena upinzani mwezi huu wa January usiishe bila kutoa tamko Kali la kudai kisheria na kikatiba mabadiliko ya katiba.

Madai yenu mya file UNO/EUROPEAN UNION/ BALOZI ZOTE NK kwajili ya rejea na ufwatiliaji.

Narudia Tena mnapambana na mtu asie muungwana mkiwa soft atawaumiza mkiwa stiff atawaumiza.

Usiku mwema!!!!!
 
Kudai tume huru ya uchaguzi sio kosa kudai mabadiliko ya katiba sio kosa baada ya maumivu ya jiwe na CCM yake kwa miaka 5/10 hatuko tayari kabisa kumpata jiwe mwingine kwa miaka kumi ijayo !! Never shall that be allowed to happen!!! It is an oath!!!
 
Halafu wewe, eti na wewe unaweza kujiita think tank ya chama fulani 😢
1. Wakigomea uchaguzi unadhani watapata nini?
2. Wamegomea uchaguzi wa serikali za mitaa, wamepata manufaa gani zaidi ya kupoteza hata mitaa/vijiji/miji/wilaya walizokuwa wanaongoza? Nani amenufaika hapa?
3. Ukitaka kujadiliana na ccm ili kuleta change LAZIMA uwe una turufu ya aina fulani mkononi. Huwezi kwenda kwenye mjadala ukiwa mikono mitupu na umetanguliza '💯' yako tu ukategemea ccm will give a f**k!
Basi ngoja wagomee uchaguzi wasipate hata mbunge mmoja uone kama wataendelea kuwa hai kama vyama vya upinzani.
 
Wapinzani wadai Tume huru na Katiba mpya wakiwa kwenye mapambano ya uchaguzi.
Sikubaliani na wazo lako la kususia uchaguzi.
Kususia uchaguzi ni kutowatendea haki wapiga kura.
Hata kama kuna tishio la kuibwa kura bado wananchi wanahitaji kuchagua, angalau pawepo na hizo kura za kuibwa kuliko kuwaacha CCM wapate ushindi wa bure bure.
 
Kaa hakuna tume huru ya uchanguzi, then upizani mukatae kusiriki kweye 2020 uchanguzi, ile kitu kitamufanya jiwe aanguka ni SANCTIONS, na mataifa yanayotupatia misaada, hio ikifanyike jiwe hana nguvu tena, kaa hukubaliani na mimi kuhusu hili, soma kile kilimfanya raisi msaafu wa kenya hapo 1992 kuondoa ibara ya 2A katika katiba ya kenya
 
Kudai tume huru ya uchaguzi sio kosa kudai mabadiliko ya katiba sio kosa baada ya maumivu ya jiwe na CCM yake kwa miaka 5/10 hatuko tayari kabisa kumpata jiwe mwingine kwa miaka kumi ijayo !! Never shall that be allowed to happen!!! It is an oath!!!
Mkuu 'Superbug', soma #3 ya Mkuu 'UmkhontoweSizwe' hapo chini.

Achana na mambo ya kudai Katiba Mpya, huu sio wakati wake, itakuwa ni kupoteza nguvu bila manufaa juu yake.

Kudai Tume Huru ndio kazi yenyewe,; lakini nayo kwa hakika sasa hivi haiwezi ikapatikana. Tume Huru haina manufaa yoyote kwa Magufuli, kwa hiyo hana sababu ya kushughulika nayo.

Njia pekee inayoweza kuileta hiyo tume ni 'shurti' isiyo ya kawaida. Sasa anza kufikiria 'shurti' isiyo ya kawaida itatoka wapi. Hapa ndipo panapohitaji kutumia vichwa ili kutafuta njia za 'shurti' asizoweza kuzikataa Magufuli.

Wewe unalo pendekezo lolote juu ya hili?

Mimi nina pendekezo kwa Vyama vya Upinzani vyote nchini.

Tokea sasa, wajitahidi kadri iwezekanavyo kuwaanda na kuwahimiza wananchi wengi kwenda kupiga kura bila ya kukosa.

Pawe na wingi wa wapiga kura ambao nchi yetu haijapata kuuona tokea tuwe na siasa za vyama vingi

Kutokuwepo kwa 'Tume Huru" isiwe sababu ya wananchi kutokwenda kupiga kura, na badala yake ndicho kiwe kichocheo cha wapiga kura wengi kujitokeza kwenda kupiga kura.

Bila shaka, vyama vya upinzani watataka watu hawa waliowahimiza kupiga kura wawape kura zao.

Hili ndio tegemeo, lakini hata kama haitakuwa hivyo lakini zile kura zikaheshimiwa na Tume Huru kumpata mshindi bila ya mizengwe, hata kama ni Magufuli atakuwa amepewa kura hizo za haki haitakuwa nongwa, na nina hakika hata wapinzani watalikubali hilo.

Maana ya watu wengi kujitokeza kupiga kura ni kuwanyima 'Tume ya Uchaguzi' kuharibu kura chache za wananchi.

Natumaini hapa utanielewa ninachokisema hapa.

Lakini najua wapo watakaoendelea kung'ang'ana kuwa haijalishi ni watu kiasi gani wamepiga kura, bado Tume itachakachua!

Ni kipi bora, wachakachue za wachache wakijua hata wakileta purukushani itakuwa rahisi kuwadhibiti, au kura za wengi, ambao kwa wingi wao wakiongozwa na hao waliowapa kura zao kudai haki yao? Jaribu kunijibu swali hilo.

Kutoshiriki katika uchaguzi kwa vyama, na kwa wananchi kutokwenda kupiga kura huo ni ushindi mnono kwa CCM. Sote tumekwishalishuhudia hili.

Ya nini kurudia makosa yaleyale ya siku zote?
 
kuna mashirika wameshajitoa kutoa misaada.
Kuna mashirika yataendelea kutoa misaada kutimiza nia zao mbovu na faida kwa nchi zao.
Kuna mashirika watajitoa
Hadi sasa mataifa machache na mashirika machache yanatoa misaada..

Hivyo impact ya sanctions will be zero
Kaa hakuna tume huru ya uchanguzi, then upizani mukatae kusiriki kweye 2020 uchanguzi, ile kitu kitamufanya jiwe aanguka ni SANCTIONS, na mataifa yanayotupatia misaada, hio ikifanyike jiwe hana nguvu tena, kaa hukubaliani na mimi kuhusu hili, soma kile kilimfanya raisi msaafu wa kenya hapo 1992 kuondoa ibara ya 2A katika katiba ya kenya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna bora hapo kuchakachua ni kuchakachua tu.Wakijitokeza wengi itatengenezwa propaganda kwamba si unaona wananchi wanaunga mkono juhudi,ndo maana wamejitokeza kwa wingi kupiga kura.
Mkuu 'Superbug', soma #3 ya Mkuu 'UmkhontoweSizwe' hapo chini.

Achana na mambo ya kudai Katiba Mpya, huu sio wakati wake, itakuwa ni kupoteza nguvu bila manufaa juu yake.

Kudai Tume Huru ndio kazi yenyewe,; lakini nayo kwa hakika sasa hivi haiwezi ikapatikana. Tume Huru haina manufaa yoyote kwa Magufuli, kwa hiyo hana sababu ya kushughulika nayo.

Njia pekee inayoweza kuileta hiyo tume ni 'shurti' isiyo ya kawaida. Sasa anza kufikiria 'shurti' isiyo ya kawaida itatoka wapi. Hapa ndipo panapohitaji kutumia vichwa ili kutafuta njia za 'shurti' asizoweza kuzikataa Magufuli.

Wewe unalo pendekezo lolote juu ya hili?

Mimi nina pendekezo kwa Vyama vya Upinzani vyote nchini.

Tokea sasa, wajitahidi kadri iwezekanavyo kuwaanda na kuwahimiza wananchi wengi kwenda kupiga kura bila ya kukosa.

Pawe na wingi wa wapiga kura ambao nchi yetu haijapata kuuona tokea tuwe na siasa za vyama vingi

Kutokuwepo kwa 'Tume Huru" isiwe sababu ya wananchi kutokwenda kupiga kura, na badala yake ndicho kiwe kichocheo cha wapiga kura wengi kujitokeza kwenda kupiga kura.

Bila shaka, vyama vya upinzani watataka watu hawa waliowahimiza kupiga kura wawape kura zao.

Hili ndio tegemeo, lakini hata kama haitakuwa hivyo lakini zile kura zikaheshimiwa na Tume Huru kumpata mshindi bila ya mizengwe, hata kama ni Magufuli atakuwa amepewa kura hizo za haki haitakuwa nongwa, na nina hakika hata wapinzani watalikubali hilo.

Maana ya watu wengi kujitokeza kupiga kura ni kuwanyima 'Tume ya Uchaguzi' kuharibu kura chache za wananchi.

Natumaini hapa utanielewa ninachokisema hapa.

Lakini najua wapo watakaoendelea kung'ang'ana kuwa haijalishi ni watu kiasi gani wamepiga kura, bado Tume itachakachua!

Ni kipi bora, wachakachue za wachache wakijua hata wakileta purukushani itakuwa rahisi kuwadhibiti, au kura za wengi, ambao kwa wingi wao wakiongozwa na hao waliowapa kura zao kudai haki yao? Jaribu kunijibu swali hilo.

Kutoshiriki katika uchaguzi kwa vyama, na kwa wananchi kutokwenda kupiga kura huo ni ushindi mnono kwa CCM. Sote tumekwishalishuhudia hili.

Ya nini kurudia makosa yaleyale ya siku zote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaa hakuna tume huru ya uchanguzi, then upizani mukatae kusiriki kweye 2020 uchanguzi, ile kitu kitamufanya jiwe aanguka ni SANCTIONS, na mataifa yanayotupatia misaada, hio ikifanyike jiwe hana nguvu tena, kaa hukubaliani na mimi kuhusu hili, soma kile kilimfanya raisi msaafu wa kenya hapo 1992 kuondoa ibara ya 2A katika katiba ya kenya
Jaribuni tu kususa
Mlisusa serikali za mitaa,hakuna impact yoyote
 
Wapinzani wadai Tume huru na Katiba mpya wakiwa kwenye mapambano ya uchaguzi.
Sikubaliani na wazo lako la kususia uchaguzi.
Kususia uchaguzi ni kutowatendea haki wapiga kura.
Hata kama kuna tishio la kuibwa kura bado wananchi wanahitaji kuchagua, angalau pawepo na hizo kura za kuibwa kuliko kuwaacha CCM wapate ushindi wa bure bure.
Bila kuwepo tume huru, siwezi poteza muda wangu, sitoenda kupiga kura.
 
Vyama vya upinzani chondechonde msije mkakubali kuingia kwenye uchaguzi 2020 bila tume huru.

Hulka na tabia ya jiwe na serikali yake mmeshaiona hawana aibu heshima staha Wala huruma kwenu Wala hawaifwati katiba.

Kama jiwe ameweza kuchezea uchaguzi wa serikali za mitaa bila kufanywa lolote Wala kutokea chochote msitegemee atakuwa mstaarabu octoba 2020.

Mkae mkijua kabisa Kama wakati wa JK kwa demokrasia ile tulishinda na bado tukahujumiwa vipi Sasa wakati wa dikteta jiwe?

Anzeni Sasa nawashauri mwezi huu wa kwanza usiishe kabla hamjaiambia dunia kuhusu ulazima wa kuwepo tume huru ya uchaguzi.

Bahati nzuri dunia nzima inamchukia jiwe na inamfahamu hulka yake sapoti itakuwa kubwa Sana na mwangwi wake utasikika Sana kuliko wakati wowote katika historia ya taifa letu.

Upinzani kumbukeni mnashindana na mtu asie na chembechembe ya ustaarabu hata kidogo Hilo mlijue.
JK alikuwa muungwana huyu ni kinyume chake ni mtu asie wa kawaida hivyo haitaji treatment ya kawaida.

Mkiingia kwenye UCHAGUZI bila kushinikiza tume huru mjue mmebariki suicide (mauwaji) maana ni sawa na kwenda kupigana na Askari mwenye smg wewe ukiwa na njiti ya chelewa Kama fimbo Kama silaha yako ya utetezi dhidi ya smg.

Upinzani kumbukeni watu wamechoka haya maisha wanasubiri mtu wa kumfunga paka kengele watoto wa mjini wanasema mtu wa kulianzisha au kukinukisha (kwa kufuata Sheria za nchi) mtapata sapoti kubwa mno.

Mpinzani wenu ambae ni CCM hakubaliki popote na jamii yoyote ya watanzania ila anatumia dola na propaganda kuwadanganya watu anakubalika kumbe sivyo.

Upinzani narudia Tena na Tena na Tena msije mkaingia kwenye ballot box mkitegemea favor itakuwa imekula kwenu.

Bashiru mmemsikia amesema wazi msitegemee tume huru Maana tume haipigi kura huu ni ujumbe tosha kwenu.

Polepole kawaambia wanaandaa mpango wa kutawala miaka 70 ijayo huo ni ujumbe kwenu upinzani akili kumkichwa.

Jiulizeni kwanini wanaanza kuweka mzinga/kuchonga mzinga wa mwewe (tiss) Zanzibar? Hio inapaswa kuwa alarm kwenu upinzani.

Kuna yanayofanyika gizani na hadharani kuandaa hujuma dhidi ya mazingira yoyote yatakayojiinua kuwabeba msije sema hatukuwaambia.

Kusoma hamuwezi hata picha hamuioni?

Narudia Tena upinzani mwezi huu wa January usiishe bila kutoa tamko Kali la kudai kisheria na kikatiba mabadiliko ya katiba.

Madai yenu mya file UNO/EUROPEAN UNION/ BALOZI ZOTE NK kwajili ya rejea na ufwatiliaji.

Narudia Tena mnapambana na mtu asie muungwana mkiwa soft atawaumiza mkiwa stiff atawaumiza.

Usiku mwema!!!!!
Pambana kijana upate Tume Huru sijui utaitoa mbinguni?
 
Back
Top Bottom