Dr. Bashiru: Mbinu na mikakati tuliyotumia kupata ushindi wa 99% kwenye Serikali za mitaa ndizo tutakazotumia uchaguzi mkuu 2020

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,744
141,609
Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru amesema kuwa katika uchaguzi mkuu wa Octoba 2020 CCM itatumia mbinu, mikakati na ubunifu ule ule uliotumika kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Dr Bashiru amesisitiza kuwa yeyote atakayejipendekeza kugombea udiwani, uwakilishi, ubunge au urais kupitia Upinzani atakuwa ni halali ya CCM kwani KUSHINDWA ni demokrasia pia.

Dr Bashiru amesema hayo akiwa ziarani wilayani Korogwe mkoani Tanga

Source: Star Tv Habari

My take: Mnyika na Chadema watapata wakati mgumu sana mwaka huu. Chadema bila mbunge itaandikwa historia mpya.

Maendeleo hayana vyama!
 
johnthebaptist,
Huyo Katibu Mkuu Dkt Bashiru anaongea hayo hata aibu hana?

Hivi atawezaje kujivunia huo ushindi wa asilimia 99 wa uchaguzi wa serikali za mitaa, wakati hata mtoto mdogo anayesoma chekechea anajua kuwa nyinyi masisiem mlifanya wizi mkubwa sana katika huo mnaouita uchaguzi wa serkali za mitaa?
 
Endelea kukariri bwashee!
 
Kama kofia ya nafasi yake chamani inamruhusu kuongea hivyo, Natamani nisikie Mnyika nae anatuambia nini kuhusu uchaguzi mwaka huu.

Ni kosa kubwa Sana chama kimoja tu kusimamisha wagombea kwenye nafasi zote kwenye uchaguzi bila upinzani wowote.Ninapokaa mimi nimeonja joto ya kuchaguliwa kiongozi wa Mtaa. Hana uwezo wa kushauri au kutoa mwongozo wa jambo lolote na ni mtu mzima Sana mzee ambaye afya yake kimwili na kiakili si Salama.

Tutalia Sana kama Diwani, Mbunge na Raisi tutachaguliwa na Sisi tukakosa nafasi ya ushiriki kwenye uchaguzi
Amani inaanzia shinani kwenye kuchagua na kuchaguliwa na fujo inaanzia huko pia
 
Huyu Dr. naye laah, kwa hiyo mbinu ya kufunga ofisi za wasimamizi wa uchaguzi mmeona imewatoa na mnataka kuendelea nayo siyo!!

Sawa ila kuweni waangalifu msije mponza mwenzenu!!
 
Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru amesema kuwa katika uchaguzi mkuu wa Octoba 2020 CCM itatumia mbinu, mikakati na ubunifu ule ule uliotumika kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Dr Bashiru amesisitiza kuwa yeyote atakayejipendekeza kugombea udiwani, uwakilishi, ubunge au urais kupitia Upinzani atakuwa ni halali ya CCM kwani KUSHINDWA ni demokrasia pia.

Dr Bashiru amesema hayo akiwa ziarani wilayani Korogwe mkoani Tanga

Source: Star Tv Habari

My take: Mnyika na Chadema watapata wakati mgumu sana mwaka huu. Chadema bila mbunge itaandikwa historia mpya.

Maendeleo hayana vyama!
Kama wewe ni mtanzania mpenda nchi na maendeleo. Likitokea hilo unaloliombea hasara itakuwa ni ya nani?
 
Wajinga wengi wanafikiri kuua upinzani ni maendeleo kwa nchi, kumbe ni hasara kwa nchi na siyo kwa upinzani. Matunda ya uwepo wa upinzani ni ya nchi nzima. Viongozi walioko madarakani husukumwa watimize wajibu wao.
 
Back
Top Bottom