Tathmini ya kisayansi juu ya matokeo ya uchaguzi mkuu Novemba 2020

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Sayansi na Teknolojia vikitumika vizuri vina uwezo wa kutoa majibu ya wakati ujao,uliopo na uliopita kwa uhakika wa asilimia 99.9%.

Katika andiko langu hili nitatumia taarifa za kisayansi zilizopo kuweza kutoa matokeo ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba 2020.

Tathmini hii isitumike kuwabwetesha wale ambao tathmini itawaonesha wanaweza kushinda ila iwe chachu ya kuwafanya wafanye vizuri zaidi.

Pia kwa wale ambao itaonesha watashindwa nao iwe chachu kwao kujiandaa na kujitahidi kushinda katika maeneo ambayo wananguvu ya kushinda na endapo itatokea kushindwa, kushindwa huko kuwe kwa kiwango cha kawaida.

Lengo kubwa ni kuhakikisha tunakuwa na viongozi waliochaguliwa na wananchi kupitia mfumo ambao sote tumeuridhia wa demokrasia ya vyama vingi.

Mazingira ya tathmini hii, yamezingatia kuwa vyama vya upinzani vitaungana vyote nchini na kumsimamisha mgombea mmoja chini ya mwamvuli wa Muungano wa Vyama vya Upinzani Tanzania (MVUTA) dhidi ya chama tawala CCM.

Tukumbuke kuwa uchaguzi mkuu wa Octoba 2015 ulihusisha baadhi ya vyama vya upinzani (UKAWA).Pili tume ya uchaguzi ifanye kazi zake kwa uadilifu na umahiri mkubwa kuhakikisha uchaguzi ni wa amani,huru na wa haki.

Tathmini yangu ina anza na idadi ya Watanzania wanaokadiriwa kufikia milioni hamsini na nne nukta mbili (54.2 milioni).

Idadi hii ina asilimia 50% (27.1 milioni) ya watoto ambao ni chini ya umri wa miaka 18,na watu wazima wanaoruhusiwa kupiga kura asilimia 50% (27.1 milioni) ambao kati yao asilimia 70% (18.97 milioni) wanaoishi vijijini na wanajishughukisha na kilimo na ufugaji pamoja na uchuuzi.

Asilimia 30% ambao (8.13 milioni ) wanaishi mijini ambao wengi wanajishughulisha na kazi mbalimbali.

Kwa mantiki hii ni wazi kuwa chama ili kiweze kupata ushindi mkubwa kinatakiwa kijiimarishe zaidi vijijini ambapo kuna idadi kubwa ya watu ukilinganisha na maeneo ya mijini ambapo kuna idadi ndogo ya watu.

Kwa taarifa na takwimu zilizopo CCM imejiimarisha zaidi vijijini ukilinganisha na muunganiko wa vyama vyote vya upinzani.

Hii inatokana na mambo mengi,moja uwepo wa wajumbe wa nyumba kumikumi,uwepo wa ofisi za chama katika maeno ya vijijini, uwepo wa viongozi wa chama na wale wa serikali wanaojishughulisha na kazi za chama, uwepo wa sherehe mbalimbali kama mwenge, uchumi wa chama na kadhalika.

Katika maeneo ya mijini kwa mijibu wa takwimu na hali ya kisiasa kwa kipindi cha nyuma, wimbi kubwa la vijana hasa wachuuzi (kwa jina maarufu la wamachinga) walivutiwa na sera za upinzani.

Huku idadi kubwa ya kinamama na wazee ikiwa na msimamo wao na imani yao kwa CCM. Kwa baadhi ya vijana sera hizi ziliwavutia kutokana na kukithiri mambo mbalimbali ya kifisadi, kunyimwa fursa za kujipatia kipato kwa kuondolewa sehemu za mijini na kutowajibika kwa serikali kwa wananchi, mgawanyiko ndani ya CCM na kuhama kwa Mh. Edward Lowasa kutoka CCM kwenda UKAWA.

Kundi hili la vijana baada ya kuonekana ni tishio kwa CCM limekumbatiwa na linaweza kuwa na mchango mkubwa katika ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020.

Tangia siku ya kwanza ya Raisi Magufuli kuingia madarakani, makundi tofauti ya wanachi kuanzia wachuuzi, wafanyakazi, wakulima, vijana na kina mama wamepewa fursa na uhuru mkubwa wa kufanya kazi halali zinazowaingizia kipato.

Hivyo basi kurejesha imani yao kwa chama kupita uaminifu aliofanya Raisi wa kutekeleza ilani ya chama sawasawa.

Vile vile ili kuweza kupata idadi ya wapiga kura katika uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020 turejee takwimu za uchaguzi mkuu uliopita wa Octoba 2015 kama ifuatavyo.

Jumla ya idadi ya Wapiga kura nchi nzima walikua ni 23.3 milioni,kati ya hao asilimia 53% walikua wanawake na 47% ni wanaume.

Idadi kubwa ya wanawake nchini walimuunga mkono Raisi Magufuli ukilinganisha na ile ya wanaume.

Katika historia ya vyama vingi nchini Tanzania, ni uchaguzi mkuu wa Octoba 2015 pekee uliokuwa na hamasa kubwa kutoka kwa vijana wanaoishi mijini juu ya mabadiliko ya uongozi kutoka chama tawala CCM kwenda muungano wa vyama vya upinzani kwa jina la UKAWA.

Uchaguzi huu ulitoa matokeo ambayo kwa tahmini ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini ni ushindi mkubwa kwa upinzani ambao hautaweza kujirudia.

Figure 1. Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015

Viashiria vya kushindwa kwa vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa Novemba 2020 vinaonekana katika nyanja zifuatazo:-

1. Muundo wa serikali na mabadiliko katika utendaji wa watumishi wa umma.

Serikali ya awamu ya tano imeundwa na aina tatu za viongozi,ambazo ni viongozi vijana, viongozi wataalamu na wachapa kazi,viongozi waadilifu na wachamungu.

Tabia hizi za viongozi wa serikali zimesaidia kuleta matumaini makubwa kwa wananchi na kurejesha imani yao kwa serikali chini ya chama tawala.

Mh Rais amekuwa akisafisha mara kwa mara serikali yake bila kumuonea haya mtu yeyote kwa maslahi ya taifa. Utoaji wa huduma kwa wanachi umekuwa wa haraka na unaofuta maadili ya utumishi wa umma.

2. Maendeleo yanayoonekana katika awamu ya tano, kauli zilizokuwa zimezoeleka za serikali ipo katika mchakato zimeondoka na kauli zakiutekelezaji zimetawala.

Jambo ambalo limekua na matokeo mazuri katika miradi mbalimbali ya kijamii kama vile miundombinu, upatikanaji wa pembejeo, maji, uimarishaji wahuduma za afya na elimu, kukamilisha miradi ya kimkakati katika kuinua uchumi, kuanzisha viwanda na kuongeza ajira kwa watanzania.

3. Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.

Kubweteka na kupelekea kushindwa kukidhi masharti kwa wagombea wengi kutoka vyama vya upinzani na baadhi kutoka chama tawala kulipelekea wagombea wengi kuenguliwa katika nafasi za kugombea Uenyekiti wa serikali za mitaa.

Maandalizi makubwa yaliyofanywa na chama tawala yalipelekea kuwepo kwa idadi ndogo ya wagombea walio enguliwa katika mchakato hivyo kuipa ushindi mkubwa katika uchaguzi huo.

Viongozi wa serikali za mitaa wanomchango mkubwa katika kuipa ushindi CCM kwa kutoa matokeo mazuri katika kipindi hiki kabla ya uchaguzi mkuu 2020.

4. Upinzani kupoteza mwelekeo

Vyama vya upinzani vimepoteza mwelekeo na kutokua na sera mbadala za kimaendelo zitakazowavutia watanzania.

Viongozi wake wamekua wakipinga mema ambayo serikali inafanya kwa wananchi pamoja na kusukumwa na matukio.

Matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo inakadiriwa kuwa na idadi ndogo ya wapiga kura yamekua njia rasmi kwa wapinzani kuwafikia wananchi huku CCM ikijiimarisha miji na vijijini kupitia vikao na mikutano na wanchi kusikiliza na kutatua changamoto zao.

Idadi ya watumiaji wa Intenet inakadiriwa kufikia milioni 10 kati ya watumiaji hao ni watanzania milioni 6 tu wanafuatilia masuala ya siasa katika mitandao ya kijamii.

Hivyo basi kama mgawanyo wa watu utafuata upenzi wa vyama ni wazi katika watu milioni 6 ni watu milioni moja wanapinga juhudi za serikali katika kuletea wananchi maendeleo.

5. Ushahidi katika tafiti zingine

Tafiti zilizowahi kufanyika nchini na nje ya nchi zinaotoa majibu yafuatayo katika chaguzi mbalimbali:-

No Jina la Mtafiti na Eneo la Utafiti Jina la Utafiti Matokeo ya Utafiti

1 Twaweza 2014 Kuelekea Uchaguzi Mkuu Jumla ya Watanzaia 51% wataichagua CCM, 24% Chadema, 25 % hawajui.

2 Twaweza 2017 Sauti ya Wananchi Asilimia 84% ya wananchi wamesema watapiga kura katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2020 ikilinganishwa na asilimia 67% ambao walijitokeza katika uchaguzi wa mwaka 2015

Ushindi kwa CCM ni 63% hadema ni 17%

Hitimisho:
Uchaguzi mkuu ujao wa Novemba 2020 utaipa ushindi CCM kwa asilimia zaidi ya 87% huku muungano wa vyama vya upinzani ukiwa na asilimia 13%.

1.png
 

Attachments

  • internet.png
    internet.png
    5.4 KB · Views: 2
  • matokeo.png
    matokeo.png
    13.7 KB · Views: 2
  • table.png
    table.png
    18 KB · Views: 2
Uzi huu utandolea kama zile zangu ,maana jf imekuwa ya ukawa siku hizi....
.
USSR

Sent using Jamii Forums mobile app

Ww na huyo mwenzako mleta mada anayepiga propaganda za kizee, mwambie hakuna mwananchi anayejitambua atashiriki chaguzi za kishenzi chini ya tume hii. Kwa sasa chaguzi zetu chini ya awamu ya tano ni kipimo halisi cha ujinga wa mtu mweusi. Wananchi kwa sasa wanajitambua na wanajua fika hakuna uchaguzi bali uhayawani, ndio maana wengi tulisusia kuajindikisha kupiga kura uchaguzi wa SM. Na huo uchaguzi mkuu tunaojitambua hatutashiriki huo ushenzi, kama dalili ya kuwaonyesha hatuwakubali ccm. Kwa hiyo jiandaeni kukaa madarakani bila ridhaa ya umma bali kama mliopindua nchi, au serikali ya kijeshi. Huo utafiti mwambie akawakoge wasiojua lolote, kwani tunajua fika hamna uwezo tena wa ushawishi, wala kushinda kwa njia ya box la kura linaloheshimiwa.
 
Kuna figures na tables ambazo nimeziandika nashindwa namna ya kuziweka humu...ila nadhani kwa wafuatiliaji wa masula ya siasa mnaweza kupata hizo statistics online
 
Kuna figures na tables ambazo nimeziandika nashindwa namna ya kuziweka humu...ila nadhani kwa wafuatiliaji wa masula ya siasa mnaweza kupata hizo statistics online,

Ccm haina uwezo tena wa kushindana kisiasa, ukiona chama kinashangilia kushinda bila kupingwa, ujue hicho sio chama cha siasa, bali ni kikundi cha kijeshi kilichovaa koti la kisiasa. Usipoteze muda wako kwa tafiti za kupika.
 
Ww na huyo mwenzako mleta mada anayepiga propaganda za kizee, mwambie hakuna mwananchi anayejitambua atashiriki chaguzi za kishenzi chini ya tume hii. Kwa sasa chaguzi zetu chini ya awamu ya tano ni kipimo halisi cha ujinga wa mtu mweusi. Wananchi kwa sasa wanajitambua na wanajua fika hakuna uchaguzi bali uhayawani, ndio maana wengi tulisusia kuajindikisha kupiga kura uchaguzi wa SM. Na huo uchaguzi mkuu tunaojitambua hatutashiriki huo ushenzi, kama dalili ya kuwaonyesha hatuwakubali ccm. Kwa hiyo jiandaeni kukaa madarakani bila ridhaa ya umma bali kama mliopindua nchi, au serikali ya kijeshi. Huo utafiti mwambie akawakoge wasiojua lolote, kwani tunajua fika hamna uwezo tena wa ushawishi, wala kushinda kwa njia ya box la kura linaloheshimiwa.

Asante mchangiaji,hii ni miongoni mwa hoja muhimu sana wanayotumia wapinzani kuwafanya wanachama wao wasijiandikishe wala kujiandaa na uchaguzi wa Novemba 2020.Hali hii inapelekea hata pale viongozi wenu wakiamua twende kwenye uchaguzi wanakua hakuna aliyejiandaa kwa kujiandikisha.

Hakuna haki inayotafutwa kwa kukaa kimya au kususia,kama kweli upinzani una sera za kuwakomboa wanachi haziwezi kususia uchaguzi.
 
Baada ya kusoma andiko lako kabla hata cjamaliza nimepata jib la moja kwa moja kuwa wewe c mtafiti bali n mwanasiasa kama wanasiasa mwingine kwa nn kwasababu pale tu ulipoanza kuorozesha makundi yanayoukubalu utawala huu kwa kutaja kundi la wafanyakaz ambao toka aingie madarakan huyu mtawala kalitenga hilo kundi utazan Luna kitu lilimkosea hafu unasema no miongon mwa makundi yanayomwunga huyu mtawala. Sasa hakuna kundi ambalo liko ktk majonz kama kund la wafanyakaz ktk utawala huu hivyo mtoa poa hapo karudie tena kufanya tafit zao ktk hili kundi hafu urud tena,kwa mfano mm na kaka yangu ambae kastafu MWAKA Jana kule kijijn tuna kampen Kali sana inayoitwa mikono isambae tusikubar arut huyu mtawala mtaumia akirud tena;
 
Jenga hoja mwenzako amejenga hoja!
Hamna hoja hapo, nimesoma mpaka pale mleta mada alipothubutu kusema kuwa chaguzi za serikali za mitaa 2019, wagombea wengi wa upinzani walikuwa hawana vigezo....... Nikaachia hapo hapo,..
 
Asante mchangiaji,hii ni miongoni mwa hoja muhimu sana wanayotumia wapinzani kuwafanya wanachama wao wasijiandikishe wala kujiandaa na uchaguzi wa Novemba 2020.Hali hii inapelekea hata pale viongozi wenu wakiamua twende kwenye uchaguzi wanakua hakuna aliyejiandaa kwa kujiandikisha.

Hakuna haki inayotafutwa kwa kukaa kimya au kususia,kama kweli upinzani una sera za kuwakomboa wanachi haziwezi kususia uchaguzi.

Narudia tena, tumeona kwa macho yetu chaguzi chini ya awamu hii ya tano zikinajisiwa tena kwa uratibu kwa vyombo vya dola na tume ya uchaguzi. Hivyo hakuna mtu yoyote mwenye akili timamu anaweza kwenda kushiriki ushenzi wa aina hiyo. Hatuko tayari kuacha shughuli zetu na kushiriki chaguzi ambazo wapinzani watatiwa vilema, watauwawa huku vyombo vya dola vikiwa sehemu ya huo uhayawani, kisha wanaccm watangazwe washindi ili kuhadaa taifa na dunia kuwa ccm inakubalika.

Huo unaooita utafiti sio lolote, sio chochote bali ni kuhadaa umma kwamba ccm itashinda kwa hiyo tafiti yako. Kama mlitarajia kupata wapiga kura wengi ili muibe kura kisha mjifanye mnakubalika basi mmechemsha, tutahakikisha watu hawashiriki huo ushenzi uitwao uchaguzi.
 
Ww na huyo mwenzako mleta mada anayepiga propaganda za kizee, mwambie hakuna mwananchi anayejitambua atashiriki chaguzi za kishenzi chini ya tume hii. Kwa sasa chaguzi zetu chini ya awamu ya tano ni kipimo halisi cha ujinga wa mtu mweusi. Wananchi kwa sasa wanajitambua na wanajua fika hakuna uchaguzi bali uhayawani, ndio maana wengi tulisusia kuajindikisha kupiga kura uchaguzi wa SM. Na huo uchaguzi mkuu tunaojitambua hatutashiriki huo ushenzi, kama dalili ya kuwaonyesha hatuwakubali ccm. Kwa hiyo jiandaeni kukaa madarakani bila ridhaa ya umma bali kama mliopindua nchi, au serikali ya kijeshi. Huo utafiti mwambie akawakoge wasiojua lolote, kwani tunajua fika hamna uwezo tena wa ushawishi, wala kushinda kwa njia ya box la kura linaloheshimiwa.
Uwepo usiwepo mpige kura msipige cha msingi jembe jpm atashinda kwa kiwango cha 99.9


USAR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maskini mkubwa wewe 2015 mlisema hivihivi


USSR
Ccm haina uwezo tena wa kushindana kisiasa, ukiona chama kinashangilia kushinda bila kupingwa, ujue hicho sio chama cha siasa, bali ni kikundi cha kijeshi kilichovaa koti la kisiasa. Usipoteze muda wako kwa tafiti za kupika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwepo usiwepo mpige kura msipige cha msingi jembe jpm atashinda kwa kiwango cha 99.9


USAR

Sent using Jamii Forums mobile app

Hata wanaopindua nchi huwa wako madarakani, acha awe rais lakini sio kwa ridhaa ya wengi, bali kupitia matumizi mabaya ya madaraka. Kama mlitarajia aonekane anakubalika basi mmepoteza.
 
Hizi mvua zinazoendelea kunyesha, naona kama zinaanza kuleta madhara ya wazi kabisa hadi kwenye akili za baadhi ya watu.
Mleta thread wewe kinachokusumbua ni mafuriko au ni baridi inaanza kugandisha ubongo???.
 
Jenga hoja mwenzako amejenga hoja!
Hoja moja kubwa ni kuwa ongezeko lolote la wapiga kura siku zote huwa ni shindikizo la upinzani na sio chama tawala. Kwa hiyo kamq utafiti wake umegunduwa kuwa kutakuwa na ongezeko la.wapiga kura basi hiyo ina maana kutakuwa na ongezeko la kura za upinzani.
 
Sijasoma huo unaoita utafiti na nimekuonea huruma kupoteza muda mwingi kuandika nadharia ambayo kiuhalisia haupo. Kwa kifupi Tanzania tuko chini ya utawala wa mabavu ambao hautokani na ridhaa ya wananchi. Kwa hiyo huo "utafiti" is simply a waste of your time kwa kuwa matokeo yanajulikana tayari.
 
Back
Top Bottom