CCM ikishinda uchaguzi Serikali yake ifafanue kipengele kwa kipengele suala la Tundu Lissu kupigwa risasi

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,397
https://www.jamiiforums.com/attachments/1581526/

Kama tunavyofahamu tarehe ya uchaguzi 28/10/2020 ndio siku ya kuchambua kati ya mchele na pumba.

Hiyo siku ya uchaguzi itakuwa ni siku ya jumatano ambayo kikalenda ni siku nzuri sana kwa wale wapenda nyota.

Pia kwa zile sherehe za wenzetu wazaramo, siku ya Jumatano mpaka Alhamisi, ni siku za kuchambua mchele wakti mwali akiandaliwa huko ndani kwa kukandwa na kusafishwa kwa machicha ya nazi na kadhalika.

Sasa basi pindi uchaguzi utakapoisha ni budi serikali ya CCM endapo itashinda iweke wazi suala la Tundu Lissu kupigwa risasi na kujibu tuhuma zote ambazo serikali naamini ina imekusanya ushahidi kutoka sehemu kadha wa kadha.

Ni jana nilimsikia mzee Lenatus Mkinga nae akieleza kwamba Chadema walihusika na kupigwa risasi kwa Tundu Lissu ili kutengeneza mazingira ambayo anayatumia sasa kisiasa kunadi sera za Chadema.

Mzee Mkinga akaenda mbali zaidi aliposema kwamba sababu kubwa ya Tundu Lissu kupigwa risasi ni kuutaka uenyekiti wa Chadema.

Pia jambo hilo ambalo ni gumu kwake na mazingira hayo ya kupigwa risasi yanashibihiana na mazingira ya kifo cha Chacha Wangwe ambae nao alionyesha dhamira ya kuutaka uenyekiti wa Chadema.

Pia humu JF ipo sehemu ya maelezo ya mmoja wa wabunge walohamia CCM alitoa ushuhuda bungeni katika moja ya vikao vyake kwamba mipango ya kupigwa risasi Tundu Lissu ilifanywa na wenyewe Chadema.

Akiongea leo katika mkutano wa kampeni wa CCM huko Segerea mgombea wa CCM raisi John Magufuli alisema kwamba pamoja na matusi na shutuma na kejeli za Upinzani kwa yale aloyoyafanya na anayoyafanya kuhusu nchi hii, wao (CCM ) wameamua kuyapuuzia na kunyamaza kimya.

Endapo CCM itashinda uchaguzi wa mwaka huu jambo ambalo naamini litatokea, ni budi polisi na serikali kwa ujumla kupitia wizara ya mambo ya ndani kuanza kujibu tuhuma za Tundu Lissu kwa serikali ya CCM na raisi John Magufuli kwama wanahusika katika jaribio la kutaka kumuua kwa kumtwanga risasi 16.

Naamini ipo sababu ya serikali kupuuzia taarifa na maelezo ya Tundu Lissu lakini pia naamini kuwa serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama wa nchi hii wanazo taarifa zote na vielelezo vyote kuhusiana na tukio hilo lililotokea huko Dodoma mwaka 2017.

Ni muhimu pia kwa serikali ijayo ya CCM ikiwa itashinda uschuzi wa mwaka huu kuhakikisha kuwa msemaji wa serikali anakuwa na taarifa zote muhimu zinazoweza kuoanishwa na taarifa zozote ziziso rasmi.

Inafahamisha kuwa lengo la taarifa zisizo rasmi au kwa kiingereza " Fake news" ni kuleta taharuki kwa wananchi na mpasuko katika jamii.

Hivyo ni matarajio yangu kwamba Polisi chini ya IGP Sirro na vyombo vya usalama vitakuwa tayari kwa kujibu hoja ambazo kwa upande mwingine zinaonekana kuzishushia hadhi kwamba havina ubavu wa kujibu.
 
Kwa kuwa wakati ana nyeshewa mvua ya risasi serikali ilikuwa inaongozwa na chama cha Chauma?

Ahaa, unataka wajibu nini kesho ikiwa leo wanaishia kumwita anatumia na bebari, wanako agiza ndege?
Nani aliye lazimisha Lisu kwenda huko na leo ni kilema lakini yupo salama na imara zaidi?
 
Back
Top Bottom