BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,009
SUALA LA SIMU KWA MAWAKALA: TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI MSIHARIBU UCHAGUZI WA WATANZANIA!
Taarifa kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itazuia Mawakala wa Vyama kuingia na simu zao katika vituo vya kupigia kura imetushtua hata sisi viongozi wa Kanisa! Simu ina mambo mengi sana katika ulimwengu wa sasa ikiwemo kutunza kumbukumbu kwa njia mbalimbali.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi haiwezi kuwafanya mawakala kama 'tabula rasa' yaani watu wasioweza kuhifadhi kumbukumbu yo yote na hata kushindwa kuwasiliana. Mawakala wakiwa na simu wanaweza kupiga picha matokeo halisi ili kudhibiti wizi wa kura! Kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuzuia Mawakala kuingia na simu katika chumba cha kupigia kura ni sawa na kuandaa usiri utakaopelekea mazingira ya kuibiwa au kuchakachuliwa kwa kura!
Tunaitahadharisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuacha kutoa maelekezo au kutunga kanuni kwa lengo la kufanya Matokeo ya Uchaguzi Mkuu yasiheshimike na wananchi! Ili kuleta afya ni vizuri maelekezo na kanuni za Tume zikubaliwe na vyama vyote. Tume iepuke kutoa kanuni na maelekezo katika kipindi hiki kwa lengo la kuubeba upande mmoja na kuunyonga upande mwingine!
Sisi tumekwisha kutimiza wajibu wetu (Ezekieli 33:1-20).
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani