uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. S

    JamiiForums Tanzania Sisi tudai Tume mpya ya uchaguzi, If not ....!

    Nalisema hili isitokee kama wale wanaoshtukizwa na teuzi,tumesikia wakipashana kuwa wale wanaojipanga kwa nafasi ya Uraisi hapo 2025 wasahau !!! Hili la wanaojipanga kugombea 2025 waache tabia hio mara moja ,sijui mlilisikia na kulichukulia poa ila hilo ni lao ,huku upinzani ni lazima juhudi za...
  2. Miss Zomboko

    JamiiForums Tanzania Algeria: Upinzani watangaza kususia Uchaguzi wa Bunge

    Chama cha upinzani cha kisoshalisti nchini Algeria FFS kimetangaza kitasusia uchaguzi wa bunge wa mapema uliopangwa kufanyika mnamo Juni 12 kikisema mazingira ya kufanyika uchaguzi huo hayaridhishi. Baraza la Taifa la chama cha hicho limesema matayarisho kuelekea uchaguzi huo siyo rafiki na...
  3. B

    JamiiForums Tanzania TLS Yafafanua Mfumo wa Upatikanaji wa Viongozi Kuelekea Uchaguzi April 2021

    Tarehe 16 April 2021 ni siku ya uchaguzi mkuu wa viongozi katika Chama Cha Mawakili Tanganyika TLS (Tanganyika Law Society). Wagombea urais waliopitishwa kugombea urais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) hapo April 16 2021 ni wagombea watano ambao ni; Shehzada Walli, Albert Msando, Francis...
  4. Analogia Malenga

    JamiiForums Tanzania GE2020 ACT-Wazalendo wasema watashiriki uchaguzi mdogo jimbo la Muhambwe

    Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kitashiriki Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Muhambwe, ambalo liko wazi baada ya kifo cha Astashasta Nditiye ambaye alikuwa mbunge mteule wa jimbo hilo Wamesema hauwezi kusimamisha shughuli zote kwa sababu ya kusubiri jambo moja. Hivyo watashiriki Uchaguzi huku...
  5. K

    JamiiForums Tanzania ACT Wazalendo, Rais siyo Tume ya Uchaguzi

    ACT Wazalendo kusema watashiriki uchaguzi Kigoma kumpima Rais ni kuuadaa Umma wa Watanzania. Juzi wameshiriki uchaguzi Zanzibar, je walikuwa wanampima Rais? Je, Rais ni msimamizi wa uchaguzi? Ni vyema wawe na msimamo tu kwamba Kama walivyoshinda Zanzibar ndivyo watakavyoshiriki uchaguzi huko...
  6. Nyankurungu2020

    JamiiForums Tanzania Kama vyama vya upinzani vingekuwa vinasusia uchaguzi kwa kipindi chote kilichopita tungekuwa tumepata Katiba Mpya

    Huenda uchaguzi mkuu wa mwaka jana umeleta funzo kwa vyama vya upinzani. Maana sasa wanaonekana kupata funzo. Jambo ambalo wanatakiwa kutambua ni kuwa tume huru ya uchaguzi ambayo itaendesha chaguzi kwa uwazi na ukweli bila upendeleo inahitaka. Tangu mwaka 1995 walipaswa kususia uchaguzi kama...
  7. J

    JamiiForums Tanzania Chadema wako sahihi kutoshiriki uchaguzi kwa sababu wabunge wao wote 20 ni kama wako CCM

    Katika hili la kutoshiri uchaguzi mimi nakubaliana kabisa na Chadema kwamba wamefanya maamuzi sahihi. Kwani wale wabunge 20 wa Chadema mule bungeni wanafanya kazi gani yenye maslahi kwa upinzani. Wao muda wote wanarandaranda na viongozi wa CCM akina babu Tale. CHADEMA komaeni hivyo hivyo hadi...
  8. Nyankurungu2020

    JamiiForums Tanzania PLO Lumumba, kusema CCM ni chama kinachopigania kunyanyua maisha ya Watanzania maskini kwa kutumia vizuri rasilimali za Tanzania, unadanganya dunia

    Nimemsikiliza huyu Prof nguli wa sheria toka nchini Kenya akizungumzia juu ya uzalendo wa hayati JPM juu ya kuwa kiongozi aliyekuwa kada wa CCM. Na kwa mujibu wa Prof Lumumba anadai CCM ni chama kinamchomuenzi hayati Julius Nyerere ndio maana kinakuwa kinahakikisha kuwa rasilimali za taifa la...
  9. Miss Zomboko

    JamiiForums Tanzania CHADEMA wamesema hawatoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe

    Chama cha CHADEMA kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Muhambwe lililopo wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma. Jimbo la Muhambwe liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge Atashasta Nditiye kufariki dunia Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma alikokuwa...
  10. S

    JamiiForums Tanzania Kina Mbowe na wenzake wanazuka unapokaribia uchaguzi Mkuu tu

    Hili sina huruma nalo. Wananchi walio wengi huingizwa kwenye mkenge na viongozi hawa wa upande wa vyama vya upinzani na hata kuthubutu kuwaambia waandamane. Hivi sasa wamekaa kimya huwasikii kabisa na hata ukiwasikia sauti zao ni kama vile unatafuta station ya redio kwenye shortwave2...
  11. Linguistic

    JamiiForums Tanzania Tutarajie Uchaguzi mdogo Jimbo la Buhigwe baada ya Dkt. Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa JMT

    Mbunge akiteuliwa kuwa Makamu wa Rais anakoma kuwa mbunge. Hivyobasi, Dk. Philip Isidori Mpango atakapo apishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakoma kuwa mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Buhingwe lililopo Mkoani Kigoma, haya ni matakwa ya masharti ya Ibara ya 47 (6) ya...
  12. lee Vladimir cleef

    JamiiForums Tanzania Naendelea kuomba, CCM itatoka uchaguzi mkuu wowote ujao 2025

    Najua watu wenye Nia njema wamekua wakiomba kwa uwazi ama kwa kificho kuhusu haki mbalimbali za kisiasa hapa Tanzania.Mimi Ni mmojawapo niliyeomba kivyangu ili Mungu afanye mabadiliko bila vurugu Wala madhara. Mambo Ni hatua kwa hatua. Katika uchambuzi wangu pamoja na maombi naona yafuatayo...
  13. Y

    JamiiForums Tanzania Ninaomba vyama vya siasa viwe makini kupendekeza Mgombea Mwenza kwenye Uchaguzi Mkuu

    Katika mchakato wa kupata Rais wa JMT, katiba inaelekeza kuwa ni lazima kuwe na mgombea mwenza ambaye Rais akishinda uchaguzi then mgombea mwenza huyo anakuwa Makamu wa Rais. Nikiri kuwa sikuwahi kuchukua cheo cha Makamu wa Rais kwa uzito mkubwa. Mara nyingi niliona kuwa makamu wa Rais ni takwa...
  14. Shadow7

    JamiiForums Tanzania Uturuki yaonywa kuingilia uchaguzi wa Ufaransa

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametahadharisha juu ya Uturuki kuingilia kati katika uchaguzi wa rais nchini Ufaransa mwaka ujao. Ameituhumu serikali ya mjini Ankara kwamba inaeneza uwongo kupitia vyombo vyake vya habari. Akihojiwa na kituo cha televisheni nchini Ufaransa cha France 5, Rais...
  15. S

    JamiiForums Tanzania Tunachokitaka na kusisitiza ni uchaguzi wa haki na si jingine

    Marehemu Raisi Magufuli ameondoka na kaiwacha nchi katika sintofahamu ya manunguniko ya matokea ya uchaguzi ,tunaweza kusema ameiwacha nchi wananchi wake wakiwa ndani ya mgawanyiko mkubwa sana unaofukuta. Ninavyoamini hata kama uchaguzi usingekuwa na mizengwe bado CCM wangeibuka videdea kwa...
  16. Sam Gidori

    JamiiForums Tanzania Kiongozi Mkuu wa upinzani Congo-Brazzaville afariki kwa Corona siku ya uchaguzi

    Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kongo (Congo-Brazzaville) na mgombea wa kiti cha urais amefariki kwa COVID-19 ikiwa ni saa chache tu baada ya vituo vya uchaguzi kufungwa. Guy-Brice Parfait Kolelas alifariki akiwa kwenye ndege akipelekwa nchini Ufaransa kwa matibabu baada ya kuumwa. Saa...
  17. J

    JamiiForums Tanzania CHADEMA itashiriki uchaguzi mdogo kule Kigoma?

    Kigoma kuna jimbo moja la uchaguzi liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo ndugu Nditiye kufariki dunia. Kwa kuwa Rais mpya mhe. Samia Suluhu amesema tushikamane na tuache kunyoosheana vidole, ndio najiuliza Chadema watashiriki uchaguzi huo mdogo? Maendeleo hayana vyama!
  18. Erythrocyte

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi BAWACHA: Majina ya waliorejesha fomu za kugombea uongozi haya hapa

  19. Chagu wa Malunde

    JamiiForums Tanzania Taifa linalojali misingi ya demokrasia lazima litengeneze mazingira kuhakikisha Rais anashinda uchaguzi kihalali

    Lazima mfumo wa uchaguzi wa Rais kizamani ambao hauendani na misingi ya kidemokrasia usiwepo tena hapa Tanzania. Kama kuna mgombea Urais ambaye hajaridhika na matokeo basi kuwepo na utaratibu wa kupinga hayo matokeo mahakamani. Ili kuhoji uhalali wa aliyeshinda. Kuishi na taifa amabalo baada...
  20. Erythrocyte

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi wa Bawacha moto mkali, fomu zaanza kuchukuliwa kwa kasi kubwa, wazito waanza kujitokeza kwa kishindo

    Waliojitokeza mapema kabisa kutia nia ni pamoja na Kamanda Elizabeth Mwakipesile ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bawacha wa Mkoa wa Mbeya, Huyu yeye ametia nia kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara. Nako kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Bawacha Taifa amejitokeza mzito mwingine anayeitwa...
Back
Top Bottom