Uchaguzi wa Bawacha moto mkali, fomu zaanza kuchukuliwa kwa kasi kubwa, wazito waanza kujitokeza kwa kishindo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,377
217,441
Waliojitokeza mapema kabisa kutia nia ni pamoja na Kamanda Elizabeth Mwakipesile ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bawacha wa Mkoa wa Mbeya, Huyu yeye ametia nia kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara.

Elizabeth Mwakipesile (Mwakimomo) ametia nia ya kugombea nafasi ya makamu Mwenye ( 640 X 640 ).jpg

Nako kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Bawacha Taifa amejitokeza mzito mwingine anayeitwa Aisha Luja, Huyu kamanda mpaka tunaingia mitamboni yeye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati

Anaitwa Aisha Luja ametia nia ya kugombea nafasi ya  Mwenyekiti wa Bawacha Taifa ( 800 X 640 ).jpg

Taarifa zilizotufikia zinadokeza kwamba kuna Majina mazito zaidi na ya kushangaza sana yasiyotarajiwa kabisa ambayo yako mbioni kujitokeza kutia nia ya kuchukua uongozi wa Bawacha, endeleeni kutega sikio

Ikumbukwe kwamba mpaka hivi sasa Bawacha ndio Taasisi ya akina mama inayotajwa kuheshimika na kuwa bora zaidi barani Afrika.

Tutaendelea kuwaletea majina mengine ya watia nia wengine kwa kadri yanavyotufikia , endelea kubaki hapa hapa JF kwa taarifa za Uhakika
 
Matokeo ya rufaa mbona hayatolewi.

Matokeo ya rufaa mbona hayatolewi au mnatengeneza sinema tu kutusahaulisha rufaa ya akina Mdee.
 
Matokeo ya rufaa mbona hayatolewi

Matokeo ya rufaa mbona hayatolewi au mnatengeneza sinema tu kutusahaulisha rufaa ya akina Mdee.
Labda kwa faida yako na wengine ni kwamba rufaa ya wahusika inahusu kuvuliwa uanachama, si kuvuliwa uongozi, Kamati kuu kabla ya kuwavua uanachama kwanza iliwavua uongozi, halafu baadaye ikawavua uanachama.

Kwahiyo wao wamekata rufaa ya kupigania uanachama wao ili waendelee kuwa wabunge, hii ni kwa sababu wanaupenda ubunge kuliko uongozi wa Chadema maana katiba hii hii ya Tanzania inayolalamikiwa inamtaka mtu ili awe mbunge ni lazima adhaminiwe na chama cha siasa kwa maana ya kuwa mwanachama na kwa viti maalum ni lazima wapitishwe na chama chao kwanza, kumbuka hawa walijiteuwa wenyewe kwa msaada wa CCM, kuanzia aliyekuwa jela na waliokuwa uraiani.

Kuhusu kujadiliwa rufaa yao hili litafanyika bila shaka bali litafanyika baada ya kuitishwa kikao cha Baraza kuu na kwa mujibu wa Katiba ya Chadema Kikao hiki kwa mwaka kinaitishwa mara 1 tu, huwa kinapangwa na kinakuwa na ajenda nyingi, hiki si kikao cha dharula, muda ukifika kitaitishwa tu.

Nadhani kwa haya machache angalau umeelewa na hatutarajii urudie tena swali hili.
 
Labda kwa faida yako na wengine ni kwamba rufaa ya wahusika inahusu kuvuliwa uanachama , si kuvuliwa uongozi , Kamati kuu kabla ya kuwavua uanachama kwanza iliwavua uongozi , halafu baadaye ikawavua uanachama .

Kwahiyo wao wamekata rufaa ya kupigania uanachama wao ili waendelee kuwa wabunge , hii ni kwa sababu wanaupenda ubunge kuliko uongozi wa Chadema , maana katiba hii hii ya Tanzania inayolalamikiwa inamtaka mtu ili awe mbunge ni lazima adhaminiwe na chama cha siasa kwa maana ya kuwa mwanachama , na kwa viti maalum ni lazima wapitishwe na chama chao kwanza , kumbuka hawa walijiteuwa wenyewe kwa msaada wa ccm , kuanzia aliyekuwa jela na waliokuwa uraiani .

Kuhusu kujadiliwa rufaa yao hili litafanyika bila shaka , bali litafanyika baada ya kuitishwa kikao cha Baraza kuu , na kwa mujibu wa Katiba ya Chadema Kikao hiki kwa mwaka kinaitishwa mara 1 tu , huwa kinapangwa na kinakuwa na ajenda nyingi , hiki si kikao cha dharula , muda ukifika kitaitishwa tu .

Nadhani kwa haya machache angalau umeelewa na hatutarajii urudie tena swali hili
Ok.

Jambo la muhimu ni wao kuendelea kutuwakilisha vema bungeni!
 
Most likely scenario: Mara tu baada ya BAWACHA kumaliza mchakato wa kupata viongozi kuziba pengo la wale walioondolewa na kufukuzwa, Baraza Kuu litakutana na kuamua kuwasamehe wale akina mama ili wawe wanachama wa kawaida tu na wasaidie kujenga chama
 
Most likely scenario: mara tu baada ya BAWACHA kumaliza mchakato wa kupata viongozi kuziba pengo la wale walioondolewa na kufukuzwa, Baraza Kuu litakutana na kuamua kuwasamehe wale akina mama ili wawe wanachama wa kawaida tu na wasaidie kujenga chama
Umetunga uongo wa hatari sana!
 
nitaleta huo ujinga wako hadharani , kama ni ban ungekwisha tandikwa kitambo , tatizo la jf kabla ya ban za namna hii ni lazima kuwe na complain , na sisi wasomi na matajiri hatuwezi kumlalamikia kapuku kama wewe
Kwenye usomi wala utajiri haupo. Unaweza kuwa na vihela vya kula unavyohongwa na hao bwana zako kwenye chama.

Ninao uwezo mkubwa kukusoma kutokana na maandishi yako.
 
Back
Top Bottom