TLS Yafafanua Mfumo wa Upatikanaji wa Viongozi Kuelekea Uchaguzi April 2021

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,293
24,173
Tarehe 16 April 2021 ni siku ya uchaguzi mkuu wa viongozi katika Chama Cha Mawakili Tanganyika TLS (Tanganyika Law Society).

Wagombea urais waliopitishwa kugombea urais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) hapo April 16 2021 ni wagombea watano ambao ni; Shehzada Walli, Albert Msando, Francis Stolla, Dk. Edward Hoseah na Flaviana Charles.

Kuelekea mkutano mkuu wa na uchaguzi wa viongozi, Chama cha Mawakili Tanganyika kupitia Corporate Secretary wake msomi Mariam Othman, kimetoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa viongozi hao. Ufafanuzi huu ni kufuatia mabadiliko ya sheria TLS yaliyofanyika hivi karibuni.

Pia viongozi wa kanda saba watachaguliwa sambamba na kiongozi wa mawakili wachanga.

Source : Wakili TV
 
Kwahy ulichoandika ndo ufafanuzi wa kumpata kiongozi au ni kichwa cha mada.?
 
Mgombea wa tano ngazi ya urais ktk uchaguzi huo wa TLS tarehe 16 April 2021 ni Rais wa zamani wa chama hicho, Francis Stolla.
 
April 6, 2021

🔴#LIVE: MNYUKANO WA WAGOMBEA CHAMA CHA MAWAKILI (TLS)​

Moderator wa mnyukano ni mzee Hamza Kasongo pamoja na kituo cha WATETEZI TV huku wagombea watano wa nafasi ya urais ni; Shehzada Walli, Albert Msando, Francis Stolla, Dk. Edward Hoseah na Flaviana Charles.
Source : MwanaHALISI TV
 
Kuna majina ya zamani yamerudi kugombea huko hata sijui walisahau nini.
 
Tarehe 16 April 2021 ni siku ya uchaguzi mkuu wa viongozi katika Chama Cha Mawakili Tanganyika TLS (Tanganyika Law Society).

Wagombea urais waliopitishwa kugombea urais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) hapo April 16 2021 ni wagombea watano ambao ni; Shehzada Walli, Albert Msando, Francis Stolla, Dk. Edward Hoseah na Flaviana Charles.

Kuelekea mkutano mkuu wa na uchaguzi wa viongozi, Chama cha Mawakili Tanganyika kupitia Corporate Secretary wake msomi Mariam Othman, kimetoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa viongozi hao. Ufafanuzi huu ni kufuatia mabadiliko ya sheria TLS yaliyofanyika hivi karibuni.

Pia viongozi wa kanda saba watachaguliwa sambamba na kiongozi wa mawakili wachanga.

Source : Wakili TV

Hiki chama kimejidharaulisha Sana mbele ya jamii baada ya jaribio lake la kuvunja Baraza la mawaziri baada ya kifo Cha Magufuli, kwa kutafisiri ndivyosivyo katiba!!
 
15 April 2021
Arusha, Tanzania

2021 TANGANYIKA LAW SOCIETY AGM & ELECTION

Source : MwanaHALISI TV
 
15 April 2021

DK. NSHALA AMPA NENO MRITHI WA KITI CHAKE TLS

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), anayemaliza muda wake, Dk. Lugemeleza Nshala amesema, uchaguzi wa viongozi wa chama hicho 2021, umezungukwa na mchuano mkali, ikilinganishwa na chaguzi zilizopita. Dk. Nshala ametoa kauli hiyo jana Jumatano tarehe 14 Aprili 2021, wakati anazungumza na waandishi wahabari jijini Arusha. TLS kinatarajia kufanya uchaguzi wa rais, makamu wa rais na mweka hazina, Ijumaa tarehe 16 Aprili 2021. Akizungunzia uchaguzi huo, Dk. Nshala amesema, mchuano huo ni mkali kwa kuwa wagombea wake wana ushawishi mkubwa, sambamba na uchaguzi huo kufuatiliwa na watu wengi nchini. "Sasa kuna mchuano mkali, inaonesha TLS ina umihumu sana katika kuhakikisha nchi inaongozwa kwa misingi ya sheria," amesema Dk. Nshala.
Source : MwanaHALISI TV
 
Back
Top Bottom