Kiongozi Mkuu wa upinzani Congo-Brazzaville afariki kwa Corona siku ya uchaguzi

Sam Gidori

Verified Member
Sep 7, 2020
93
150
Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kongo (Congo-Brazzaville) na mgombea wa kiti cha urais amefariki kwa COVID-19 ikiwa ni saa chache tu baada ya vituo vya uchaguzi kufungwa.

Guy-Brice Parfait Kolelas alifariki akiwa kwenye ndege akipelekwa nchini Ufaransa kwa matibabu baada ya kuumwa. Saa chache kabla, mgombea huyo alionekana katika video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii akiwasihi wafuasi wake kumpigia kura akisema kuwa anapambania uhai wake kutokana na maambukizi ya corona.

Kolelas ni mmoja ya wapinzani 6 waliokuwa wakipambana na kiongozi wa nchi hiyo, Sassou Nguesso ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1979, isipokuwa kwa kipindi cha miaka 5 baada ya kushindwa uchaguzi wa mwaka 1992.

Sheria za uchaguzi za nchi hiyo hazibadilishi matokeo ikiwa mgombea mmoja atafariki. Congo-Brazzavile imeshuhudia visa 9,000 vya maambukizi ya virusi vya corona na vifo 130.

Chanzo: BBC
 

stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
4,132
2,000
Republic of Congo opposition candidate Guy-Brice Parfait Kolelas has died of Covid-19 as he was being transferred to France for treatment, his campaign director said Monday, the day after presidential elections in which he was the main challenger.

Kolelas was seen as the main rival to veteran leader Denis Sassou Nguesso, who was expected to win Sunday's vote.

The election was boycotted by the main opposition and under an internet blackout, with critics voicing concerns over the transparency of the polls seen as tilted towards Sassou Nguesso.

Kolelas "died in the medical aircraft which came to get him from Brazzaville on Sunday afternoon," his campaign director Christian Cyr Rodrigue Mayanda told AFP.

The 60-year-old tested positive for Covid-19 on Friday afternoon, and was unable to host his last campaign meeting in Brazzaville.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom